Madiwani watatu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoani Iringa wamejiuzulu

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,287
Madiwani watatu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoani Iringa wamejiuzulu nafasi zao na kukihama chama hicho kwa kile wanachodai kuwa viongozi wao ngazi wametawaliwa na rushwa na ubaguzi dhidi ya baadhi ya madiwani.

Akiongea kwa niaba ya wenzake Baraka Kimata diwani wa Kitwiru amesema ameamua kufanya maamuzi hayo magumu ili hali anatambua kuwa wapo watu watachukizwa na maamuzi hayo lakini hana jinsi kwa kuwa amevumilia mambo mengi ndani ya chama hicho.

"Najua wapo watu wataumia kutokana na maamuzi haya lakini sina jinsi imebidi nifanye maamuzi magumu kwani kuna wakati watu mnafanya vikao hafikii maamuzi kutokana na mabishano mpaka muda mwingine mnatishiana maisha sasa tunaendelea kutafakari hichi chama ambacho kimewaaminisha Watanzania kuwa chama mbadala kikachukua dola kitawaletea Watanzania nini" alihoji Baraka

Diwani huyo aliendelea kufafanua mambo mengine mengi mtazame hapo chini



Chanzo: EATV
 
Hela za Bwana Slow hazitowaacha Madiwani Walafi walioko CDM salama.......!!!!
 
Baada ya kuiangamiza CUF nguvu inaelekezwa CDM.

Hadi 2020 mtu anapita bila kupingwa.
 
Back
Top Bottom