Madiwani watano CHADEMA waomba radhi

tamko la kamati kuu ndiyo inayosubiriwa, ila nadhani watafanya lobbying kwanza mpaka madiwani wote waandike barua za kuomba radhi, abaki Mallah peke yake ndiyo afukuzwe kama mbwa koko. kuna kila dalili inaonyeshwa huyu bwana kapewa mlungula na Magamba. hata mahali anaishi ni karibu sana na meya wa kichina Gaudence Lyimo, wametenganishwa na barabara, inawezekana wameongea kichaga wakayamaliza pale pentagon
 
Mnasifia nini hapo? Slaa alikupuka na kutoa vitisho bila kujua umaarufu wake umesimamiwa na kusemewa vizuri na madiwani. Alisema atawafukuza. Hao walioomba radhi hata hawakushitakiwa mnamdanganya nani waliotishiwa wote wamesimama imara kauli yao wanamtaka slaa atoe ushahidi wa yale aliyowatuhumu. Hana ushahidi, nao hawaombi radhi.
 
Hongera Mzee Slaa wewe ongoza chama na usitawale kama CCM wanavyo tutawala na kutuibia .Nakuamini na mzozo wa Arusha unakuzwa na wachovu .You have my support .Imarisheni Chama.
 
mallah simama kidete tupo nyuma yako, sisi ndio tuliokuchagua, hata wakikufukuza utarudi kwa tiketi chama kingine.

Join Date : 26th July 2011

Posts : 2
Rep Power : 0

Mdanganye hivyo hivyo!
 
Join Date : 26th July 2011

Posts : 2
Rep Power : 0

Mdanganye hivyo hivyo!

Mkuu usiangalie ID hapa watu wana ID zaidi ya moja, inawezekana kwenye ID yake amepigwa ban kaanzisha nyingine. mi mwenyewe nafurahi kuwa na ID nyingine, kwenye ile nyingine nimepigwa ban
 
Mnasifia nini hapo? Slaa alikupuka na kutoa vitisho bila kujua umaarufu wake umesimamiwa na kusemewa vizuri na madiwani. Alisema atawafukuza. Hao walioomba radhi hata hawakushitakiwa mnamdanganya nani waliotishiwa wote wamesimama imara kauli yao wanamtaka slaa atoe ushahidi wa yale aliyowatuhumu. Hana ushahidi, nao hawaombi radhi.
Hivi unauhakika na unayosema au almradi uonekane umeandika.
 
Hongera Mzee Slaa wewe ongoza chama na usitawale kama CCM wanavyo tutawala na kutuibia .Nakuamini na mzozo wa Arusha unakuzwa na wachovu .You have my support .Imarisheni Chama.
Unajua Mkuu kuna watu humu walikuwa wanafurahia huu mgogoro nikawaambi hiki ni cha mtoto tu kwa Chadema wala hakiwasumbui maana chama kimeshapita kwenye matanuru makubwa zaidi ya hili. Ajabu hata wanachama wanaojulikana walikuwa wanashadidia uhuni huu na utovu wa nidhamu wa madiwani kujifanyia maamuzi bila kufuata taratibu za chama kwa kisingizio cha kunyimwa uhuru wao, binafsi nilikuwa nawashangaa sana na nitaendelea kuwashangaa maana uhuru bila utaratibu ni kuleta fujo ndani ya chama.
 
Mimi kwa upande wangu sishabikii upande wowote. Ninachokipendekeza katika kulipatia ufumbuzi suala hili ni kuhakikisha kwamba taratibu na kanuni za chama zinafuatwa ipasavyo. Mwenye makosa ashughulikiwe pasi ya kuwa na uonevu wala upendeleo wowote.

Napingana na watu wanaodai kuwa busara zitumike katika kumaliza mgogoro huu. Suala la kutumia busara ndo limefanya CCM wamefika hapa walipo leo. Chama kina katiba, kanuni na taratibu zake ambazo hupaswa kufuatwa kikamilifu wakati wote. Viongozi wakubwa kama madiwani wanayajua hayo.

Kama itatokea kuwa mtu atahama chama eti kwa sababu Chama hicho kinazingatia maadili yake, huyo aachwe aende. Vile vile hata suala la Shibuda nalo limalizwe kwa kuzingatia taratibu hizo na wala sio busara.
 
Haki Yetu umeniongezea shule kidogo kwamba wafuate taratibu na kanuni na si busara umeeleweka.
 
mallah simama kidete tupo nyuma yako, sisi ndio tuliokuchagua, hata wakikufukuza utarudi kwa tiketi chama kingine.

Swala sio kumfukuza Mallah,swala ni kufanya maamuzi kama chama.Kama amekwenda kinyume na makubalio ya chama ni bora aondolewe hata kama atahama chama na kushinda akiwa chama kingine.HATA KAMA UNAUPENDA SANA MGUU WAKO,UKIPATA KANSA NA DOKTA AKAKUSHAURI UKATWE MGUU HAUNA NAMNA LAZIMA UKATWE KWA AJIRI YA AFYA YAKO.
 
mallah simama kidete tupo nyuma yako, sisi ndio tuliokuchagua, hata wakikufukuza utarudi kwa tiketi chama kingine.
ndio mliomchagua???m-kigoma na arusha wapi na wapi.. ndo wale wale wa kudakia mambo
 
KATIBU Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa, amesema madiwani watano wa chama hicho kati ya 11 waliodai kuhusika na uingiaji mwafaka na CCM, wamewasilisha barua za kuomba radhi ofisini kwake.

Hatua hiyo imekuja huku kukiwa na barua ya kukata rufaa iliyowasilishwa na Mwenyekiti wa madaiwani hao, Estomi Mallah, kupinga uamuzi wa kamati kuu wa kutengua maridhiano yaliyofikiwa na madiwani hao.

Dk Slaa alisema tayari amepokea barua kutoka kwa madiwani watano kati ya 11 waliokuwa wameorodheshwa kwenye barua ya kukata rufaa.“Baada ya uamuzi kutolewa na kamati kuu, niliwaandikia barua za kuwataka wajiuzulu nyadhifa zao ndani ya siku tatu, lakini wao wakapinga hatua hiyo na mwenyekiti wao akawasilisha barua ya kukata rufaa,” alisema Dk Slaa.

Alisema barua hiyo iliyowalishwa kwake, ilikuwa na upungufu kutokana na kuorodhesha majina ya madiwani wote 11 wa chama hicho, huku sahihi zikikosekana kwa baadhi ya majina.

Alisema kufuatia upungufu huo, alimtaka mwenyekiti huyo kuwasilisha ushahidi utakaobanisha madiwani walivyohusika katika kikao cha kupinga uamuzi wa kamati kuu na msimamo wa chama.

“Mimi bado sijapata ushahidi kutoka kwa mwenyekiti huyo hadi sasa, nilichopokea ni barua tano kutoka kwa baadhi ya madiwani walioshiriki mwafaka huo za kuomba radhi,” alisema Dk Slaa bila kutaja majina ya madiwani hao.

Kuhusu hatua za kinidhamu, Dk Slaa alisema: “hapa hakuna siri hilo linasubiri vikao vya chama.” Alisema Chadema kina taratibu za kufanya uamuzi kupitia vikao na vitakapopangwa, wananchi watajulishwa.

Mgogoro wa Chadema ulianza kujitokeza pale kamati kuu ya chama hicho ilipotangaza kutotambua mwafaka baina ya CCM, Chadema na TLP kumaliza mgogoro wa umeya Arusha, baada ya madiwani kugoma kujiuzulu wakitaka chama kiwasafishe na tuhuma za rushwa zilizotolewa dhidi yao.

Januari 5, mwaka huu watu watatu akiwamo raia wa Kenya waliuawa kwa kupigwa risasi na polisi wakati wa maandamano ya kupinga uchaguzi wa umeya, huku viongozi wakuu wa chama hicho wakifikishwa mahakamani kujibu mashtaka mbalimbali kuhusu maandamano hayo.

Mbaya hapa ni kutaka kutumia vyombo vya habari!
Si wayamalize kwanza ndo waje kwenye vyombo vya habari.Hivi vyombo vya habari ndo vinaleta shida siku zote.
 
Hahahaha kumbe watu WA ban tuko wengi.....mood bora hata usimpige mtu ban maana haisaidii kitu...angalia malaria sugu anA id 63 mimi nimefikisha 4 na wengine ndio usiseme hahaha hii imekaa vizuri kweli

mkuu usiangalie id hapa watu wana id zaidi ya moja, inawezekana kwenye id yake amepigwa ban kaanzisha nyingine. Mi mwenyewe nafurahi kuwa na id nyingine, kwenye ile nyingine nimepigwa ban
 
mallah simama kidete tupo nyuma yako, sisi ndio tuliokuchagua, hata wakikufukuza utarudi kwa tiketi chama kingine.
Yani umetumwa jamvini leo na umeanza na UPUPU.
Sisi hatukumchagua akafanye huo ujinga.
Lakini anaweza pia kufarijika kama akisikia kuna angalau mjinga mmoja wa kumsapoti.
 
mallah sijui atatoka na mlango wa nyuma ama dirishani, kwa katiba ya chadema hawa jamaa inatakiwa wa mwagwe bila kuchelewa
 
Back
Top Bottom