Madiwani watano CHADEMA waomba radhi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Madiwani watano CHADEMA waomba radhi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Quinine, Jul 27, 2011.

 1. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #1
  Jul 27, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,908
  Likes Received: 12,066
  Trophy Points: 280
  KATIBU Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa, amesema madiwani watano wa chama hicho kati ya 11 waliodai kuhusika na uingiaji mwafaka na CCM, wamewasilisha barua za kuomba radhi ofisini kwake.

  Hatua hiyo imekuja huku kukiwa na barua ya kukata rufaa iliyowasilishwa na Mwenyekiti wa madaiwani hao, Estomi Mallah, kupinga uamuzi wa kamati kuu wa kutengua maridhiano yaliyofikiwa na madiwani hao.

  Dk Slaa alisema tayari amepokea barua kutoka kwa madiwani watano kati ya 11 waliokuwa wameorodheshwa kwenye barua ya kukata rufaa."Baada ya uamuzi kutolewa na kamati kuu, niliwaandikia barua za kuwataka wajiuzulu nyadhifa zao ndani ya siku tatu, lakini wao wakapinga hatua hiyo na mwenyekiti wao akawasilisha barua ya kukata rufaa," alisema Dk Slaa.

  Alisema barua hiyo iliyowalishwa kwake, ilikuwa na upungufu kutokana na kuorodhesha majina ya madiwani wote 11 wa chama hicho, huku sahihi zikikosekana kwa baadhi ya majina.

  Alisema kufuatia upungufu huo, alimtaka mwenyekiti huyo kuwasilisha ushahidi utakaobanisha madiwani walivyohusika katika kikao cha kupinga uamuzi wa kamati kuu na msimamo wa chama.

  "Mimi bado sijapata ushahidi kutoka kwa mwenyekiti huyo hadi sasa, nilichopokea ni barua tano kutoka kwa baadhi ya madiwani walioshiriki mwafaka huo za kuomba radhi," alisema Dk Slaa bila kutaja majina ya madiwani hao.

  Kuhusu hatua za kinidhamu, Dk Slaa alisema: "hapa hakuna siri hilo linasubiri vikao vya chama." Alisema Chadema kina taratibu za kufanya uamuzi kupitia vikao na vitakapopangwa, wananchi watajulishwa.

  Mgogoro wa Chadema ulianza kujitokeza pale kamati kuu ya chama hicho ilipotangaza kutotambua mwafaka baina ya CCM, Chadema na TLP kumaliza mgogoro wa umeya Arusha, baada ya madiwani kugoma kujiuzulu wakitaka chama kiwasafishe na tuhuma za rushwa zilizotolewa dhidi yao.

  Januari 5, mwaka huu watu watatu akiwamo raia wa Kenya waliuawa kwa kupigwa risasi na polisi wakati wa maandamano ya kupinga uchaguzi wa umeya, huku viongozi wakuu wa chama hicho wakifikishwa mahakamani kujibu mashtaka mbalimbali kuhusu maandamano hayo.
   
 2. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #2
  Jul 27, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Malah leo ndio anaona umuhimu wa kutumia vikao mbona awali aliita waandishi wa habari alidhani watamsaidia,
  halafu anataka kuwalazimisha na wengine waliokwisha omba radhi yeye aendelee na sarakasi zake za kujipima ubavu na kamati kuu.
   
 3. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #3
  Jul 27, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Dr. Slaa big up. Sasa naona kuna dalili za kukomaa zaidi katika uongozi. Nilipingana nawe kipindi kile hapa JF kuhusu suala la kumsimamisha kiongozi wa Chadema ngazi ya wilaya kule Nzega, ingawa hukukubaliana na maoni yangu lakini nimefurahi umeyafanyia kazi. Ni faraja kwangu kwamba leo unatamka wazi kwamba maamuzi yanasubiri kikao cha chama. Maadui wa Chadema na wewe walikuwa wanasubiri ukurupuke na kutangaza kuwasimamisha hao madiwani bila kikao cha Chama ili wawe na hoja ya kukushika, lakini wamepiga chini.

  Keep it up
   
 4. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #4
  Jul 27, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Hapa ndipo patamu ni mtego yaani walete hadidu za rejea za kikao walichokaa kupinga maamuzi ya kamati kuu, kama hatabaki Malah pekee mtaniambia.
   
 5. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #5
  Jul 27, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,673
  Trophy Points: 280
  Source!
   
 6. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #6
  Jul 27, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Safi sana Dr! Na hata hao ambao bado hawajajisalimisha watakuja tu. Peopleeeeeeeee Powerrrrrrrrrrrrrrrrr!!!!!
   
 7. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #7
  Jul 27, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,275
  Trophy Points: 280
  Quinine, kuna mtu anataka chill source na tomato source, usisahau kumuekea na chips na mayai ya mbuni.
   
 8. m

  mkigoma JF-Expert Member

  #8
  Jul 27, 2011
  Joined: Jul 26, 2011
  Messages: 1,182
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  mallah simama kidete tupo nyuma yako, sisi ndio tuliokuchagua, hata wakikufukuza utarudi kwa tiketi chama kingine.
   
 9. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #9
  Jul 27, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  katika hao madiwani watano yupo Nanyaro Ephata?
  1. Sabina Francis
  2. Viola Lazaro
  3. Isaya Doita
  4. Chrispin Tarimo
   
 10. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #10
  Jul 27, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,674
  Trophy Points: 280
  Hiyo nzuri sana,inatakiwa wote waombe radhi sisi sio magamba bwana!
   
 11. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #11
  Jul 27, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Ni baada ya kupata ushauri nasaha kutoka kwa mzee mtei ndo amegundua kwamba njia aliyokuwa anaipitia siyom yenyewe, sasa kaamua kupitia njia sahihi.
   
 12. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #12
  Jul 27, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  lete ushahidi kwamba hawa ndio wameandika barua za kuomba radhi.
   
 13. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #13
  Jul 27, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  Wakishatambua makosa yao hawana budi kuomba radhi. Chadema siyo sehemu ya Mipasho, Mallah akae akijua.
   
 14. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #14
  Jul 27, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  we hata Arusha huijui kaa kimya
   
 15. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #15
  Jul 27, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  mkuu source tunayo, ila nilikuwa nafanya utafiti kujua huyo diwani wa tano, kama siyo Elibariki Malle basi atakuwa ni Nanyaro. Kuna lobbying ilikuwa inafanyika kuwagawa madiwani, kama unakumbuka kuna thread ilikuwa inaelezea kugawanyika kwa madiwani.
   
 16. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #16
  Jul 27, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,329
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Huyu Mallah anaonekana ana uchu wa madaraka. Aligombea ubunge mara mbili akakosa, nadhani akaona udiwani utampatia umeya. Ccm walipochakachua, akaona angalau unaibu meya, sasa anaona chama kinambania tena. Huu ni uchu wa madaraka na kwa cdm ataangukia pua!
   
 17. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #17
  Jul 27, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,673
  Trophy Points: 280
  Kumuekea! Du!! Zao la shule za kata
   
 18. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #18
  Jul 27, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Diwani Nanyaro hakushiriki kwenye muafaka, na tangu mwanzo alishaupinga, sasa aombe radhi kwa kipi??
   
 19. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #19
  Jul 27, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Na kwakuwa ni mtu mwenye historia nzuri ya kuhama hama vyama si ajabu kuwa anajiandaa kurudi alikotoka kama atafanikiwa kuivuruga chadema Arusha.
   
 20. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #20
  Jul 27, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Shule za kata ambazo magamba mnajivunia!!!
   
Loading...