Madiwani wa CHADEMA Dodoma kujiunga na CCM

Madiwani wa CHADEMA Dodoma kujiunga na CCM

Kama wataingia mkenge wa kuvua gwanda na kuvaa gamba kabla ya kulipwa chao itakuwa imekula kwao. Waulize wenzao wa Shinyanga hadi leo wanapigwa chenga.
 
Kwani na nyie chadema ruzuku mnayo wakinunua mtu na nyie mnanunua! CCM ni kama Real Madrid kila mwanasiasa anataka kuchezea, pamoja na padri slaa.
 
Wakazi wa Dodoma hawajui chama kingine zaidi ya ccm!!! Acheni kusema Dodoma kuna chadema ili kupata sifa!!!
Chadema itatoa wapi madiwani ndani ya himaya ya ccm???

Ndo mana mtakuwa ombaomba maisha yenu yote
 
Bora wale bata ukiwa cdm kumbe uko kama almasi kweli vile mbona wccccm hawanunuliwi au cdm njaaa kali sana;;;; kuwa cdm kumbe dili.

kizuri chajiuza, kibaya chajitembeza
 
Kwani na nyie chadema ruzuku mnayo wakinunua mtu na nyie mnanunua! CCM ni kama Real Madrid kila mwanasiasa anataka kuchezea, pamoja na padri slaa.

Kumbe ruzuku ya ccm ni kwa ajili ya kununua watu? Huku kwetu CDM,ruzuku ni kwa ajili ya kutoa na kusambaza elimu ya uraia tu na si vinginevyo na ndio maana huwa tunasema hakuna nafasi ya wachumia tumbo huku cdm
 
ukinunuliwa ndo umekwisha>kwa kizazi hiki cha kupenda ishara na miujiza tafuteni wasaliti waliishia wapi!LAMWAI anasumbuka,WALID ndo huyo,
 
CHADEMA YAENDELEA KUHUJUMIWA,MADIWANI WAKE WAKE DODOMA WANUNULIWA KUJIUNGA NA CCM.

Wakuu hii habari sio tetesi tena ,naiweka hapa jukwaani kama habari kamili.


Madiwani wa CHADEMA mkoani Dodoma wamedaiwa kunuliwa na CCM ili kuisaliti CHADEMA siku yoyote kuanzia sasa,madiwani hao 3 wanaotajwa kutoka ji,bo la Mtera na 1 hajatajwa anatokea jimbo wala kata gani ndani ya mkoa huo, mpango huo unaoendelea kuratibiwa na viongozi wa CCM mkoa Dodoma kwakwa ushirikiano wa karibu na viogozi wa ACT pamoja na aliyekuwa mgombea wa CHADEMA jimbo la Mtela mwaka 2010 bwana John Lameck Robote/Lugose,mpango ulioratibiwa kwa mda wa takribani mwezi 1 sasa.


Kwa mujibu wa chanzo cha taarifa hii,awali wasaliti hao walikuwa wamepanga wajiuzuru baada ya mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan,kutokana na mpango huo haramu kugunduliwa na intelegensia ya CHADEMA,wameamua kuuharakisha na sasa hautasubiri mwezi mtukufu uishe na mda wowote kuanzia sasa wataitisha mkutano wa waandishi wa habari,ama watarudisha kadi kwenye mkutano wa hadhara unaoandaliwa na CCM Dodoma ,mkutano utakaofanyika mda wowote kuanzia sasa na wamependekeza Jk awepo.


Kwa mujibu wa chanzo cha taarifa hii kilichopo miongoni mwa waratibu wa mpango huo muovu dhidi ya CDM,kinadokeza vikao vya awali vilifanyikia katika mikoa ya Daressalam,Morogoro na sasa waratibu wa mpango huo, wapo mkoani Dodoma wakiendelea na uratibu huo kikao kilichoandsliwa kufanyikia Dodoma Hotel,


Mpango huu unaratibiwa na Samwel Malichela (Mtoto wa John Samwel Malichela ambaye anaungwa mkono na viongozi wa CCM jimbo la Mtera na Dodoma katika jitihada zake za kuhakikisha mbunge wa sasa jimbo la Mtera Livingstone Lusinde”kibajaji”anang’olewa kwenye kiti cha ubunge uchaguzi ujao) kwa kushirikiana na viongozi wa CCM mkoa Dodoma kupitia kwa katibu mwenezi wa mkoa, katibu mkuu wa CCM mkoa wa Dodoma bwana Mgumba ambaye mpaka sasa ndiye alieidhinisha malipo ya kugharamia nauli ya kuwaleta madiwani wa CDM kutoka jimboni Mtera,gharama za ukumbi, malazi jumla ya fedha hiyo ni shili Laki 4 na elfu 70(470,000)


Na miongoni mwa magari yaliyotumiwa katika safari za kuratibu shughuli zote hizo za kutaka kuihujumu CDM ni gari namba T 645 CUG aina ya NADIA, Nyaraka zinaonesha mmliki wa Gari hilo ni bwana Kyamani Elpidius, ambaye hadi sasa haijulikani anajishughulisha na nini, Hata hivyo, mtoa taarifa anaendelea kupasha kuwa CCM hadi sasa wameingizwa mkenge kwani mpango uliopo ni kuwa, madiwani hao watajiunga na CCM kwa muda tu, baadae watarudi kujiunga na Chama kipya cha ACT wakati wa uzinduzi wake mwezi wa 9 mwaka huu.

Na mwisho wa siku wameahidiwa kupewa pesa yote ambayo wangelipwa kama madiwani kwa kipindi cha kuanzia siku watakayojiudhuru mpaka mwakani,pia katika sakata hili kuna mtu mmoja anatajwa kwa majina ya Gwakisa Burton anatajwa kuwa nyuma ya mpango huu.

  • :angry:

Kwenye msafara wa Mamba, Kenge nao wamo.Haishangazi!!!
 
Kila mara tuna sema, iliyokuwa CHADEMA imejengwa kwa misingi ya kibaguzi na kilaghai. Kama baadhi ya wanachama au viongozi wanapogundua kuwa ndani ya CHADEMA kuna ubaguzi na ulaghai basi ni haki yao kuondoka kwa amani kama baadhi yao wanavyofanya kwa sasa. Vile vile ni haki yao kuwaeleza wananchi kuhusu ubaguzi na ulaghai unaoendelea ndani ya CHADEMA.

Kwa hiyo unataka kuwaaminisha wanaJf kuwa viongozi wa CHADEMA wananunulika kwa maana nyingine, viongozi wa iliyokuwa CHADEMA wanatumia jina CHADEMA kama bargaining platform.

Chama chenye Itikadi na Sera zinazowaleta na kuwaunganisha wanachama na viongozi wenye malengo yatokanayo na Sera na Itikadi hakiwezi kutumika kama jukwaa la manunuzi ya wananchama na viongozi.

Haishangazi sana kwa sababu hata katiba ya CHADEMA kwa sasa imechakachuliwa na baadhi ya waliokuwa viongozi wakuu ili waendelee kuwepo madarakani ambapo matokeo yake kwa sasa wameamua kukimbia vivuli vyao na kujificha kwenye kikundi kinachoitwa UKAWA.
Well put. Ingawa vyama vyote vya siasa ni bargaining platform ya wanasiasa duniani.
 
Kwanza jaribu kuheshimu majina ya watu kabla hujaanza kumwaga pumba zako, pili, hata kama wewe ni mke wa Ritz hukustahili kumjibia yeye kwani kijembe hicho yeye binafsi amekipokea kwa raha mstarehe!
Wewe ni ke au me? Mh. Kikwete ana mke au unataka kuwa mke mdogo nini? Gwalihenzi



Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Mkuu tenende, nimecheka sana hayo mambo Mnyika na Slaa si walikanusha? Mbona hamueleweki nyie? Ndo akili kubwa hii?
Jumababu, Katika wote uliowataja hakuna aliyesema taarifa hiyo haina UKWELI ila walisema siyo CHADEMA iliyoweka mitandaoni. Hizo bilioni 3.6 zilirushwa bila umakini kwani karibu nusu ya wafuasi wake hawakuwa na dhamira ya dhati ya kumtumikia. Amini usiamini kuna watu wanne kati ya hao wafuasi wanazo meseji za mgao wa fedha hizo hadi leo sawa sawa na details za waraka husika. Hivyo USIMTETEE MSALITI!...
Kama huamini onana na wafuasi hao mmoja baada ya mwingine utapata taarifa!.. Wakikuruhusu chunguza meseji za tarehe hii.
Tarehe 25/2/2012 saa 10:09 asubuhi, ZZKaliwatumia shilingi 150,000/= wafuasi wa kundi lake:

  • Juliana Shonza
  • Habib Mchange
  • Mtela Mwampamba
  • Gwakisa Burton
  • Eddo Makata
  • Greyson Nyakarungu
  • Deogratius Kisandu
  • Adams Chagulani
  • Exaud Mamuya
  • Ben Saanane
Baada ya hapo saa 10:32 asubuhi hiyohiyo ZZK kupitia namba yake ya simualiwatumia shilingi 200,000/=
Mkumbo Kitila na
John Shibuda
 
kumbe wanaumwa halafu ccm ndio inawasaidia kuwatibu..hongera sana chama cha mapinduzi ...Ni Heri Kutawaliwa na Wakoloni Weusi (CCM) Kuliko Wakoloni WEKUNDU (Chadema) - DR. KITILA MKUMBO.
Acha unafiki, nani alisema demokrasia ni kuhama kutoka CCM au vyama vingine na kwenda CDM peke yake? Mbona Dr. Slaa alitoka CCM akaenda CDM, mbona Tindu Lissu alitoka NCCR akaenda CDM? Kwa nini kila anayetoka CDM kwa akili yako finyu unaamini kuwa amenunuliwa na siyo demokrasia?
Sasa hapa si unaiharibia CDM kwa wanadodoma wote? Au CDM haitaki kura za Dodoma?
Waraka wa usaliti unasemaji kuhusu bosi wenu na nyie wasaliti wengine? Soma:

Udhaifu wa tunayemtaka:


  • Maneno yake mara nyingine hayazingatii anayazungumza katika mazingira gani na hivyo kuwasha masikio ya wanataasisi jambo linalompunguzia kukubalika kwake taratibu.
  • Kama ilivyo kwa maneno, kuna matendo pia ambayo mara nyingine huyafanya bila kuzingatia mazingira na wasikilizaji wake na hivyo kupunguza imani ya wana taasisi kwake.
Kuoa mtoto wa mfalme
  • Katika taasisi zetu hizi ni muhimu sana kuepuka kufanya mambo yote wazi wazi hata kama ni mema ama ni haki ya mhusika ama si makosa katika jamii tuliyomo.
  • Kuna mambo ambayo ni haki ya mtu mfano mahusiano binafsi ya kimapenzi, kuwa na marafiki wa damu kutoka upande mwingine wa utawala, nk.
  • Lakini mambo hayo ni muhimu wakati mwingine ama kwa kiwango fulani yakafanywa kwa siri kuepuka mitazamo potofu kwa unaowaongoza.
VIKAO NJE YA NCHI!
  • Vikao vyetu na yeye vitafanyika mara chache sana na mahali pa faragha kupita kiasi ikiwezekana hata nchi jirani.
DINI
  • Kwa kuwa ni mwislamu. Hii ni fursa katika kupata kuungwa mkono na wanachama waislamu ambao wamekuwa na kigugumizi wakidhani waislamu hawatakiwi katika uongozi wa taasisi yetu.
 
Inaonesha hujui alichosomea slaa. Unadhani anaitwa dk wa nini?

Umewahi kusoma waraka wa usaliti?
Kililichokupeleka ACT ni ni kama si maneno haya ya kitila?
Kwa kuwa ni mwislamu. Hii ni fursa katika kupata kuungwa mkono na wanachama waislamu ambao wamekuwa na kigugumizi wakidhani waislamu hawatakiwi katika uongozi wa taasisi yetu.
 
Kama kuna hata watu waliomsaliti Bwana Yesu, sembuse Chadema? acha watumikie tamaa ya nafsi zao!


I like it

A%20S%20109.gif
 
Inaonesha hujui alichosomea slaa. Unadhani anaitwa dk wa nini?

Si kwamba sijui!... Naelewa saana!... Hoja yako hapa unajitambulisha UISLAMU wako na CHUKI yako dhidi ya wakatoliki full stop!
 
Back
Top Bottom