Madiwani wa CHADEMA Dodoma kujiunga na CCM

Madiwani wa CHADEMA Dodoma kujiunga na CCM

Kwa nini ukimbilie kusema wanunuliwa badala ya kusema kuwa wameshtuka kuwa misukule.

kama ni kushituka kuwa misukule kwa nini wafanye vikao vya siri na viongozi wa magamba na walipwe hizo laki 470,000? Hizo pesa za kazi gani wakati wanao uhuru wa kuchagua chama wakipendacho? Hayo ndiyo matumizi ya bil 2 za ruzuku wazipatazo ccm @ mwezi? Mtahangaika sana na CDM na hamtaiweza! Mi naona bora wameondoka mapema hawa wachumia tumbo kuliko kuja kununuliwa wakati wa chaguzi au kuuza kata na majimbo kwa kujiengua dk za mwisho.Wanaondoka wawili,maelfu wanajiunga na kununua kadi za cdm.
 
Ujinga kama huu hawawezi kuufanya mijini kwa watu wenye akili....... Watakimbilia vijijini mahali mtu anaona shilingi laki tano ni Mungu.... Nawaambia maccm hao watu wakijitambua sijui mtaficha wapi sura zenu nyie manyang'au!

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Hana jeuri hiyo... Thubutu, hata siku moja.


Sent from my iPhone using JamiiForums

kwani suala la ccm kununua watu limeanza leo? Mbona kila mahali ndio utamaduni wa magamba? Mtahangaika sana lakini hamna uwezo wa kutununua wote,mtaishia kuwanunua wachumia tumbo wenzenu tu!
 
Hana jeuri hiyo... Thubutu, hata siku moja.


Sent from my iPhone using JamiiForums

unanii fluence ili niuweke hapa,bt nitauweka hapa kwa wakati sahihi,na sio kwa shinikizo lako,kwa sasa nimeweka ushahidi wa namba za gari na jina la mmiliki
 
Ujinga kama huu hawawezi kuufanya mijini kwa watu wenye akili....... Watakimbilia vijijini mahali mtu anaona shilingi laki tano ni Mungu.... Nawaambia maccm hao watu wakijitambua sijui mtaficha wapi sura zenu nyie manyang'au! Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
Zitto, Kitila, na Mwigamba mnaosema ------------ na CCM nao walikuwa vijijini?
 
wewe Mwanadiwani endelea kuwa vuvuzela,nafikiri hasira za Lowassa zinakungoja,wait and see
Vijana wa BAVICHA mna shangaza na kufurahisha sana. Mmepewa kazi ambayo iko juu ya uwezo wenu kihoja.

Umeanzisha mada kuhusu Ulaghai na ubaguzi wa CHADEMA, kwa sasa unataka tuache kuchangia katika msingi wa mada yako na tujikite tena kwenye mada nyingine kuhusu vuvuzela na hasira za Lowassa.

Jikite kwenye hoja yako!.
 
Wakazi wa Dodoma hawajui chama kingine zaidi ya ccm!!! Acheni kusema Dodoma kuna chadema ili kupata sifa!!!
Chadema itatoa wapi madiwani ndani ya himaya ya ccm???
 
unanii fluence ili niuweke hapa,bt nitauweka hapa kwa wakati sahihi,na sio kwa shinikizo lako,kwa sasa nimeweka ushahidi wa namba za gari na jina la mmiliki
Mkuu Nicholaus Kilunga "Unanii fluence"????? Sijui unamaanisha nini mkuu, lakini kama nikukulazimisha sijakulazimisha ila kuna haka ka-msemo "no research no right to speak." Hizo namba za gari ndo ushahidi tosha??? Mnakasha wako umekaa kimajungu majungu. Acha janja janja hii nchi ni ya kidemokrasia madiwani wanahaki zao za kuhama chama wakati wowote ule muhim wasivunje sheria.



Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
kwani suala la ccm kununua watu limeanza leo? Mbona kila mahali ndio utamaduni wa magamba? Mtahangaika sana lakini hamna uwezo wa kutununua wote,mtaishia kuwanunua wachumia tumbo wenzenu tu!

Mkuu bujash Kama kununua rahisi na nyie kanunueni basi mchukue madiwani wote na wabunge wote na ikulu iwe yenu.



Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Sasa kama viongozi wenu wananunulika kirahisi hivi itakuwaje mkipewa nchi, si mtatuuza au?
Ndugu, waeleze hawa vijana wa BAVICHA.

Kwa lugha nyingine wanatuambia viogozi wa CHADEMA ukiwawekea pesa mezani hawazikatai kwa sababu chama kiko katika ulingo wa kisiasa kutimiza malengo ya viongozi wakuu kimaslahi. Ndiyo maana wengine wanachukua kila mwezi bila kikomo pesa ya chama inayoingia kutoka serikalini kama ruzuku kwa madai kuwa wamekikopesa chama. Viongozi wengine wanakikopa chama bila uwepo wa kanuni na pia ni kinyume cha maadili ya chama.
 
Mkuu bujash Kama kununua rahisi na nyie kanunueni basi mchukue madiwani wote na wabunge wote na ikulu iwe yenu.



Sent from my iPhone using JamiiForums

Sisi hatuna pesa za kunua watu bali za kusaidia kutoa na kusambaza elimu ya uraia kwa watz wote.Wao wana EPA,pesa za Escrow acount, mabilion ya Uswis, za ujangili,za biashara ya sembe hivyo hayo ndiyo matumizi yake.Pesa haramu na matumizi yake haramu pia
 
Last edited by a moderator:
Hao hawajanunuliwa bali wamejitambua

Kwa nini ukimbilie kusema wanunuliwa badala ya kusema kuwa wameshtuka kuwa misukule.

Kwa sababu hata kiongozi wa wasaliti alishanunuliwa kama wao ili aitumikie CCM kupitia tawi lake la ACT.
Ushahidi wa Kitila huu hapa:
Kuhusu mwenendo wa MM kuanzia sasa:
Ni maoni yetu pia kwamba kuanzia sasa MM aenende katika mwenendo ambao utarahisisha ushindi. Mfano tunapendekeza afanye yafuatayo kuanzia sasa:

  • Apunguze ukaribu na viongozi wa serikali na wa chama tawala na awe crical zaidi na utendaji wa serikali nje na ndani ya bunge.
  • Ashiriki kikamilifu katika shughuli za taasisi yetu zikiwamo vikao vyote vinavyomhusu, operesheni mbalimbali, chaguzi ndogo, nk.
  • Aendelee kushusha ‘nondo' ndani ya chombo chetu cha uwakilishi na kuendelea kuwa juu ya wawakilishi wengine katika hoja mbalimbali zenye maslahi ya kitaifa.
Vikao vyetu na yeye vitafanyika mara chache sana na mahali pa faragha kupita kiasi ikiwezekana hata nchi jirani.
 
Ndugu, waeleze hawa vijana wa BAVICHA.
Kwa lugha nyingine wanatuambia viogozi wa CHADEMA ukiwawekea pesa mezani hawazikatai kwa sababu chama kiko katika ulingo wa kisiasa kutimiza malengo ya viongozi wakuu kimaslahi. Ndiyo maana wengine wanachukua kila mwezi bila kikomo pesa ya chama inayoingia kutoka serikalini kama ruzuku kwa madai kuwa wamekikopesa chama. Viongozi wengine wanakikopa chama bila uwepo wa kanuni na pia ni kinyume cha maadili ya chama.
Muulize huyu:
Mazungumzo yao ndani ya chumba hiki yalianza maramoja, akianza Mr Ighondu kueleza sababu za wao kumuita Zitto, kikubwa ilikuwa ni "bwana Zitto, serikali (ikulu) inakutaka uache kuibana na kuishurutisha hasa kwa hili suala la Buzwagi". Tunaomba kujua shida yako kubwa ni nini?" Ighondu alihoji, Katika majibu yake Zitto anajibu, "Mimi napigania haki za watanzania, nimechaguliwa na wanakigoma na watanzania wameniamini ni wawakilishe hivyo", Lakini mashambulizi ya ushawishi yalipozidi Zitto alilegeza msimamo wake.
 
CHAGADEMA wanatapatapa.

Zitto, Kitila, na Mwigamba mnaosema ------------ na CCM nao walikuwa vijijini?

Nicholaus Kilunga, hivi chuo cha SAUT kina kozi ya umbea au tetesi???

Mkuu bujash Kama kununua rahisi na nyie kanunueni basi mchukue madiwani wote na wabunge wote na ikulu iwe yenu.

Haya, chimbuko la usaliti wenu ni hili:
Uchunguzi umeonyesha kuwa pesa ile aliyokabidhiwa ndugu Zitto, ilitoka katika akaunti Namba 0J56708968923 yenye jina la Shani Maya, ambapo inaonyesha kuwa akaunti hii ilifunguliwa CRDB tawi la azikiwe tarehe 25/6/2008 saa 10:14 asubuhi, kisha tarehe 27/6/2008 iliingizwa kiasi cha pesa za kitanzania milioni 400. Na tarehe 30/6/2008 pesa hizo zilitolewa zote na akaunti hii ilifungwa.

SEHEMU YA PILI 2009
Mnamo Jumatatu ya tarehe 30/11/2009 saa 04:30 asuhuhi wakati wa maandalizi ya uchaguzi wa mkuu wa 2010, idara ya ujasusi ya ccm ilikutana kwa siri pale Moven Pick/SERENA Hotel, ndani ya idara hii wakiwamo Jack Zoka, Wilson Mkama, Kingunge Ngombale Mwiru, Jakaya Kikwete, Nape Nnauye, Fred Kimati, Steven Wasira, Ramadhani Ighondu, Martin Palakyo, Mwigulu Nchemba, Ahamed Msangi na Abdalla Punja. Katika kikao hiki yalijadiliwa mengi sana, lakini kubwa lilikuwa nikukabiliana na vyama vya upinzani hususani CHADEMA, zilipangwa mbinu nyingi sana juu ya Chadema, Mbinu hizo ni kama ifuatavyo:

  • Kuwanunua wagombea ubunge na Udiwani (Mtakumbuka wagombea wetu kadhaa walikuja kununuliwa na chama kina ushahidi kwenye hili).
  • Kuwanunua VIONGOZI wajuu wa CHADEMA.
  • Kutumia TISS kutisha wagombea na wanachama wa Chadema (Hii ilikuwa ni kuwakamata au kuvuruga mikutano).
  • Kuwaua baadhi ya wafuasi wa Chadema, viongozi wa Chadema na wabunge.
Lakini walitilia mkazo zaidi njia ya kwanza ,ya pili na ya tatu ambapo kikao kilijiridhisha kuwa mmoja wa VIONGOZI wa Chadema ambae ni Zitto Kabwe ni mtu wao ambaye wamesha anza kumtumia, kikubwa liandaliwe fungu tu kwa ajili yakuanza mikakati yao, Waliafikiana mambo mengi kwaajili ya uchaguzi wa mwaka ambao ungefuata, na wakakubaliana mambo kadhaa ambayo walimuagiza Mr Zoka akamwambie Zitto nini cha kufanya ili kupunguza nguvu ya upinzani.
Kwa upande wake Zoka alikiambia kikao kuwa Zitto amemthibitishia kuwa yeye anawafuasi wakutosha ndani ya chama ambapo watamuunga mkono kwa lolote hivyo kikubwa ni pesa tu.
Lakini kwanza kikao hicho kilimtaka
Mr Zoka amwambie Zitto kuwa taarifa zote zinazoihusu Chadema na za kila vikao vya ndani vya chama zinatakiwa pia ziifikie timu hiyo ya kijasusi ya ccm, pili walitaka Zitto apunguze ushiriki katika majukwaa ya chama na shughuli nyingine za chama. Baada ya kikao sasa ulikuwa ni utekelezwaji wa maadhimio yao.
Maandishi mekundu anathibitisha Kitila kuwa ni kweli, soma hapa chini:

Kuhusu mwenendo wa MM kuanzia sasa:
Ni maoni yetu pia kwamba kuanzia sasa MM aenende katika mwenendo ambao utarahisisha ushindi. Mfano tunapendekeza afanye yafuatayo kuanzia sasa:

Apunguze ukaribu na viongozi wa serikali na wa chama tawala na awe crical zaidi na utendaji wa serikali nje na ndani ya bunge.
Ashiriki kikamilifu katika shughuli za taasisi yetu zikiwamo vikao vyote vinavyomhusu, operesheni mbalimbali, chaguzi ndogo, nk.
Aendelee kushusha ‘nondo' ndani ya chombo chetu cha uwakilishi na kuendelea kuwa juu ya wawakilishi wengine katika hoja mbalimbali zenye maslahi ya kitaifa.
 
Hawajitambua bali wamechagua tumbo kuliko mabadiliko

Ni madiwani wangapi hao waliogharamiwa laki nne na elfu sabini (470,000/=)!!!??? Watanzania tuna matatizo ya kiakili. Tunawezamchagua mtu anaywewza kutelekeza uwakilishi wa wananchi kwa 470,000/=???
 
Back
Top Bottom