Fukara
JF-Expert Member
- Dec 28, 2013
- 1,624
- 930
Kata zao zakosa watia nia, Wasema wanasubiri kauli yake, kikao cha kamati ya siasa chaitishwa kwa dharura leo.
Mh.Edward Lowassa.
Kasi ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuomba nafasi za udiwani na ubunge katika Jimbo la Monduli, inasuasua na tayari chama hicho kimeitisha kikao cha dharura cha Kamati ya Siasa kitakachokutana leo kukuna vichwa kutafuta ufumbuzi wa hali hiyo.
Katibu wa CCM Wilaya ya Monduli, Elisante Kimaro, alisema jana kuwa kusuasua kwa wanachama kuchukua fomu za kuomba kugombea nafasi hizo kunatokana na kushuka kwa morali ya wanachama baada ya Mbunge wa zamani, Edward Lowassa, aliyekuwa akiwania kuteuliwa na chama chake kugombea urais, kukatwa jina lake.
Alizitaja kata hizo kuwa Engaruka, Engutoto, Esilalei, Lepurko, Loksale, Majengo, Makuyuni, Meserani, Nalalani, Lemooti, Moita, Monduli Juu, Monduli Mjini, Mfereji, Mswakini, Mto wa Mbu, Migungani,
Chanzo: Nipashe