Madiwani 10 wa CCM na UDP wajiunga na CHADEMA

Madiwani 10 wa CCM na UDP wajiunga na CHADEMA

Subiri ocotober 25 utajua kama hawana mvuto

hapa bariadi hao wote hawana mvuto na walijua wasingechaguliwa ndo maana wamekimbilia huko na CHADEMA kuwasimamisha kwenye udiwani ni sawa na hawajasimamisha watu.
 
Huko ndio kukuwa kwa uhuru wa siasa nchini lakini mimi nashangaa wakiama wa CCM kwenda vyama vingine vya siasa inakuwa poa tu yani doho tabu lakini wakiama wa vyama vingine especially wa chadema unaitwa usariti au inakuwa ni bifu lakini em samahani nisaidieni maana ya neno msariti?
 
kuna uzi humu magamba yalikuwa wanamsapoti msaliti mmoja nashangaa hapa hata kuchangia maoni yao wanaona aibu
 
Watanzania jawa wanajitambua, ccm ni adui wa mafanikio ya watanzania
 
Jamani UKAWA tunaomba msamaha hatutarudia tena babaaaaa!
 
Napenda kuwapa onyo chadema kuhusu madiwani wa ccm wanaojiunga kwa wingi na chama hicho katika kipindi hiki cha kutafuta wagombea wa udiwani na ubunge.

Kuwadokeza tu Madiwani hao wametumwa kurahisisha ushindi wa CCM katika maeneo yao. Cinema itakuwa hivi baada ya kuwa wamepitishwa na chadema na kuthibitishwa na Tume ya uchaguzi watajiengue chadema na kurudi tena ccm hivyo kufanya wagombea wa ccm katika maeneo yao kupita bila kupingwa ama kwa ushindi mwepesi na laini;

kaaeni macho huo ni mpango mkubwa unaoratibiwa nchi nzima kuhakikisha chadema inapata madiwani wachache sana hivyo kushindwa kuongoza halmashauri
 
CHADEMA chama cha watanzania ni vizuri ikachukua tahadhali hiyo. Kipindi hiki kuna wimbi kubwa la wanachama wa CCM watakimbilia CDM kwa mission maalumu. Wengine watakuja kuhujumu chama hata baada ya uchaguzi.

Wanaohamia kipindi hiki wawe ni wananchama wa kawaida tu. Ila mamvi asikaribishwe asilani kwani ana mikono michafu, akiingia tutamkimbia!
 
Hapa umenena wengine wamelipwa pesa ktk mkakati huo.shibda na matata wa mwanza ni somo tosha.
 
Hawajaja huku kuomba uongozi kwani huko kwao waliuacha. Msiogope
 
Ccm kazi wanayo.Huo ni mwanzo tu,watahamia wengi.Watanzania wengi wanajitambua
 
Kampeni Piga mbizi imeanza mapemaaa.Lubuva mkate makomeo
 
Wakati zoezi la uchukuaji fomu za kugombea nafasi za ubunge na udiwani kwa ajili ya uchaguzi mkuu mwaka huu likiwa limepamba moto katika vyama mbalimbali vya siasa hapa nchini,waliokuwa madiwani wapatao 10 kutoka katika vyama vya CCM na UDP wilayani Bariadi mkoani simiyu wamevihama vyao vyao na kujiunga na chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA.

Wametangaza uamuzi wa kuvihama vyama vyao katika mkutano wa hadhara wa chama hicho uliofanyika katika kijiji cha Dutwa.

Katibu mwenezi wa chama hicho wilaya ya Bariadi, Martin Moga amesema kujiunga kwa madiwani hao kutakiongezea nguvu chama hicho hasa ukizingatia kwamba sasa hivi wanaelekea katika uchaguzi mkuu.

Katika hatua nyingine mwenyekiti wa mkoa wa chama hicho Wilson Mshuda amesema chama hicho kimechukizwa na mbinu chafu zilizofanywa na aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Andrea Chenge la kuzuia jimbo hilo lisikatwe wakati kuna wilaya hapa nchini zina wakazi wachache majimbo yao yamekatwa na kwamba kufanya hivyo ni kuwanyima wananchi kupata huduma za msingi huku mwenyekiti wa baraza la vijana mkoa huo mark malulu akiwataka vijana wa mkoa huo kutojenga uoga katika kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi.
 
Back
Top Bottom