Madiwani 10 wa CCM na UDP wajiunga na CHADEMA

Madiwani 10 wa CCM na UDP wajiunga na CHADEMA

mpalu

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2010
Posts
2,521
Reaction score
876
Madiwani%2Bwa%2BCCM.JPG

Baadhi ya madiwani muda mfupi baada ya kukabidhiwa rasmi kadi za CHADEMA.

Bariadi%2Bmadiwani.JPG

mASUNGA.JPG
Aliyekuwa diwani kata ya Sakwe Masunga Ngagani (UDP) (Kushoto) akihutubia mamia ya wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa michezo Dutwa wakati wa kutambulishwa kwao kujiunga na Chadema. Kulia ni diwani wa kata ya Nyakabindi Benjamini Matondo.

Vyama viwili katika wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu CCM pamoja na UDP vimepata pigo kubwa baada ya madiwani wake wapatao 10 kutimkia katika Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa madai ya kuchoshwa na uongonzi wa vyama hivyo.

Akiwataja majina madiwani hao Katibu Mwenezi Chadema wilayani Bariadi Martine Mogani, alisema kuwa kati ya hao, watatu ni kutoka CCM na saba kutoka UDP ambao ni Benjamini Matondo (UDP) Nyakabindi, Shiwa Danhi (UDP) Sapiwi na Gulya Nyembe (UDP) Ihusi.

Wengine ni Ruta Mahagija (CCM) Dutwa, Nhandi Madede (UDP) Ikungulipu, Matalu Mongobusia (UDP) Mwaubingi, Andrea Henoka (UDP) Nkindwabiye, Juma Nengelo (CCM) Somanda pamoja na Masunga Ngagani (UDP) kutoka kata ya Sakwe.
Seni%2BSilanga.JPG

Mtia nia nafasi ya Ubunge katika jimbo la Bariadi Magharibi Seni Silanga kupitia Chadema, akiongea na mamia ya wananchi katika kata ya Dutwa wakati wa kutambulishwa kwa madiwani 10 waliojiunga na chama hicho.

Chanzo: Simiyu News
 
Ahahahahaaa Mzee cheyo kwisha habari yake. Walimwambia waziwazi mwaka huu huchomoki,akasema eti kama hawamtaki yeye basi wachague ccm, wakmwambia huwezi kutuchagulia.
 
Sidhan kama watakuwa wavumilivu na kuiacha bila kuifuta
 
Karibuni sana Makamanda tuunganishe nguvu kuikomboa Tanzania yetu tuitakayo.
 
Wanakimbia ushindani kule cdm watapata namba kirahisi

wamepima matokeo ya serikali za mtaaa wakaona uhakika wa kutoboa oktoba hamna ....salama ni kujisalimisha...Mzee Cheyo ana kazi nzito sana
 
Hahahaaa eti kanda ya ziwa yote wanamkubali Magufuli!

Walahi magufuguli ndoa atakuwa mgombea urais wa kwanza wa CCM kushindwa. aibu ya miaka 55 ya uhuru.

Aikimbie aibu hii ajitoe mwenyewe badala ya kutolewa na wapiga kura.
 
Back
Top Bottom