uthibitisho wa kawaida tu juu ya ufikiriaji mdogo wa mtu mweusi: Mtu amezaliwa kwenye jamii masikini ya kutupwa, akalelewa na kusomesha ndani ya jamii hiyo hiyo masikini, na pengine hiyo jamii ilimsaidia yeye kwa namna moja au nyingine kuvuka malengo yake, akafanikiwa. Baada ya muda anaomba ridhaa kwenye jamii hiyo hiyo ili aiongoze akijinasibu kwa ahadi lukuki kuwa atatatua matatizo ya jamii hiyo na kuivusha sehemu fulani. Hatimaye wanamwamini na kumpa uongozi, kinyume na matarajio ya wanajamii, yule mtu anageuka mdhalimu wa kutupwa juu ya jamii ileile masikini, ambayo imemlea, kumkuza, kumsomesha, kumuamini, na kumpa wadhifa wa uongozi, yule mtu anakuwa mnyanga,anyi wa rasilimali, mwizi, jeuri, kiburi, mkandamizi, mtukanaji wa watu wake. Kama hiyo haitoshi yule mtu anataifisha kila mali ya jamii husika kwa walowezi kwa manufaa ya tumbo lake, anaingia makubali ya ajabu-ajabu na walowezi isiyo na tija yoyote kwa jamii yake, anazidi kuididimiza jamii yake umasikini zaidi. Je huyu mtu utasema IQ yake nzima kwel