Madhara ya wanaume watulivu

MAHEPE

Member
Joined
Mar 10, 2011
Posts
88
Reaction score
30
Mke wa Frankhuwa anajivunia mume wake kuwa ni mtulivu. Hashindi Bar na si msaliti wandoa. Akitoka kazini huenda kucheza basketball na hurudi nyakati za dinner.

Siku moja mkeweakamuhurumia. Akajiuliza 'Mtu gani asiyependa starehe hata kidogo? Akamlazimisha outing,Frank akagoma. Hajatulia mara taxi ikafika, kumbe Mkewe alikuwaalishamwita. Gari vuuuuuu ikafunga breki ROZANA NIGHT CLUB.

Walipofika mlangoni tu,mlinzi akaita, “Mambo Frank!”. Frank akajibu “Poa”. “Nilidhani huwa huji club,inakuwaje mlinzi anakufahamu?” Mke akauliza

Frank akajibu “Yulemgambo, mchana analinda ofisini kwetu, usiku anapiga part time hapa”.

Wakachagua meza. Ilekukaa tu tayari mhudumu ameshaleta castle lager. Akamuuliza 'Mama anakunywanini? Mhudumu alipoondoka mama akauliza, “Amejuaje unakunywa Castle kama hakufahamu?”Wakati Frank anajikanyaga aanze vipi kujitetea, mhudumu wa vyumba akawa amefikana kuuliza, “Mkuu kama kawaida nimekuandalia namba tano, nendeni tu vinywaji
nitawaletea huko huko”

Kufikia hapo mama akawahana simile tena. Akanyanyuka akitukana kama chizi. Akatoka nje mbio na kuingiakatika taxi iliyokuwepo pale. Wakati anapatana bei na dereva, Frank nayeakaingia. Mama akaporomosha matusi kibao na kilio juu.

Alipovuta kamasi nakupiga kwikwi akamsikia dereve anasema, “Duh! Eeee bwana Frank! Huyu malayauliyeokota leo balaaaaaaaaaaaaaaa!”

Mamaaakazimiaaaazzzzzzzzzzzzzzzzzz

 
Huna siri mkuu, mbona siku ile tulipatana vizuri tu usiitoe siri bhana.
 
Watulivu wa kweli hawana madhara hayo. Huyu wa kwenye thread kaonewa tu kuitwa mtulivu.
 
hadithi ya kutunga iyo.. Hashindi Bar na si msaliti wandoa. Akitoka kazini huenda kucheza basketball na hurudi nyakati za dinner
sasa anapata wapi huo mda wa kufanya umalaya na kunywa pombe.......
 
Chukua like yako mkuu!very emotional and logic

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Umekosea kumwita mtulivu, huyo jina linalo mfaa ni msaliti
 
ingepaswa kuitwa..mbwa mwitu ndani ya ngozi ya kondoo
 

Hadithi nzuri kakufundisha nani?
 
Hakuna malaika kwenye hii makitu!! Ila tu huwa twajipa moyo..........! Kwi kwi kwi!
 
Kwa hiyo watulivu wote tabia zako ziko hivi? Generalization hii inanipa mashaka!
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…