Madhara ya utumiaji wa Tumbaku/sigara

Llio 002

JF-Expert Member
Jul 14, 2015
1,615
2,031
Kila sekunde nane, mtu mmoja hufariki kutokana na utumizi wa tumbaku. Imebainika kuwa saba kati ya wavutaji sigara kumi, huanza uraibu huu wakiwa wangali watoto. Wanaoendelea kuvuta sigara kwa muda mrefu hufupisha maisha yao kwa miaka 20 hadi 25. Sababu ni kuwa sigara ina kemikali zaidi ya 4,000 ambazo zina uwezo wa kudhhuru afya ya binadamu. Madhara yanayosababishwa na uvutaji sigara ni mengi na yamesambaa mwilini kote. Yafuatayo ni baadhi tu ya maradhi yatokanayo na utumiaji wa tumbako

1: Kung'oka kwa nywele
Uvutaji sigara hudhoofisha kinga ya mwili na kisha kudhuru mizizi ya nywele . hii husababisha kung’oka kwa nywele mapema.

2: Magonjwa ya macho.
Wavutaji sigara hupata magonjwa ya macho mara nyingi kuliko wasiovuta. Sehemu ya macho inayopitisha mwangaza inaweza kufichwa kama vile wingu linavyoficha jua(yaani kwa ikimombo) na kusababisha upofu. Ugonjwa huu husababishwa kwa njia mbili. Kwanza moshi wa sigara huwasha macho na pili kemikali zilizo ndani ya sigara hupita kwenye mishipa , damu na hatimaye kudhuru macho. Sigara pia husababisha kudhoofika kwa sehemu ya kati ya macho(retina) na hivyo kupunguza uwezo wa macho kuona vizuri na hata kutofautisha .

3: Saratani ya ngozi.
Uvutaji sigara unasababisha saratani ya ngozi. Kemikali za sigara husababisha vidonda kwenye ngozi na ambavyo haviponi kwa urahisi. Baada ya muda hugeuka kuwa saratani.

4: Magonjwa ya mapafu
vutaji wa siagara ndio sababu kubwa zaidi ya saratani ya mapafu. Pia husababisha kupasuka kwa vibofu vya hewa safi na kutoa harufu mbaya mwilini. Wavutaji pia hupata saratani ya koromeo na kuziba njia ya hewa na hivo basi inabidi kutobolewa kwa kishimo kwenye shingo hili kuwezesha mwadhiriwa kupumua.

5: Magonjwa ya moyo.
Sigara ndio sababu kubwa zaidi ya magonjwa ya moyo. Inasababisha moyo kupiga kwa kasi zaidi na hivyo kuongeza msukumo wa damu mwililni( high blood pressure). Mwishowe husababisha mshtuko wa moyo na hata kifo.Moja kati ya kila vifo tatu ulimwenguni hutokana na magonjwa ya moyo na huua zaidi ya watu milioni moja kwenye nchi za Afrika.

Tunakumbushana tu jamani haya ndio baadhi ya madhara ya uvutaji wa sigara faida zake sizijuwi kwa hiyo usije kuniuliza kuhusu faida zake. Sigara ni miongoni mwa bidhaa zinazopitishwa na TBS ilihali madhara yake yanajulikana kwa hiyo kuwa na afya nzuri ni jukumu lako mwenyewe.

Huo chini hapo ndio mwili wa mvutaji wa Sigara.

Mchana mwema
Mwili_wa_mvutaji_sigara.jpeg
 
Back
Top Bottom