Madhara ya modern life

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
58,636
Reaction score
220,438
Maisha ya mjini ni modern life kula mayai na sausage asubuhi pamoja na chai yenye maziwa na sukari bila kusahau mkate au chapati.

Mchana utakula pilau, chips kuku, kiepe na mengineyo na jioni kwakuwa ulikuwa sana ugali boarding school umeamua kuupa mgongo sikuhizi jioni unakula pizza.

Unajua calories ulizoweka mwilini tangu umeamua asubuhi?
Mayai mawili ya kuchemsha na ndizi moja mbivu pamoja na kikombe cha chai bila sukari ni chaguo bora kwa kufungua kinywa.

Madhara hasa ya kuwa na excess fat kiunoni ni kusumbuliwa na type 2 diabetes. High cholesterol inasababisha mafuta kuzunguka moyo kushindwa kufanya kazi vizuri, kupelekea heart failure.
Uncontrolled Diabetes type 2 na heart failure vinaambatana, moyo unaposhindwa kupump damu madhara yake ni miguu kuvunja na kukaa maji.

Moyo kufanya kazi ya ziada ya kupump damu linaweza kusababisha kupasuka kwa mishipa ya damu inakoleta haemorrhage stroke.

Mabonge ya damu yenye mafuta kuziba mishipa ya damu na kusababisha ischemic stroke

Sukari unayopata kwa kula ugali na staple foods nyingine inakutosha kwa mahitaji yako ya mwili. Chai ya sukari tuwaachie watoto na vijana.
 
Si ndio mnayofanya hayo nyie wanawake Siku hizi!
Eti mnakula "salad" Sijui mpunguze vitambi!
Ndio maana operations Siku hizi haziishi!

Ratiba ya zamani ilikuwa hivi;
Asubuhi: chai Na mkate wa ngano ya asili ile nyeusi

Mchana; Ugali Mkubwa+Maharage ya mbeya & mchicha

Usiku;Ugali + mboga au maharage tena

Ubwabwa Siku za sikuku [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Ubwabwa ulikuwa na heshima, ukipakuliwa watoto mnazunguka sinia mnawekewa ukoko kwenye chujio la nazi
 
Sky
kwani wewe una uzito gani kati ya hizi?!
45 - 55; 55 - 65; 65 - 75; 75 - 85; 85 - 95; 95 - 105.
 
Bibie mbona sasa hujataja madhara?
Au umekosea kichwa cha habari?
 
Sky
kwani wewe una uzito gani kati ya hizi?!
45 - 55; 55 - 65; 65 - 75; 75 - 85; 85 - 95; 95 - 105.
Mhh mkuu thi is too personal but my aim is to get down to 75kg. I’m only 5.6”
 
Napenda mwanaume anaekula haswaa Ile kula ya kiume ila Asijiachie akapasuka na kuwa na mwili wa kihasara na kupata kitambi..

Smart911
Wanaume wanao taji calories nyingi kulilo sisi lakini mazoezi yanapendeza zaidi
 


Dawa yake ni a lot of sex!
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…