Madhara Ya Mapenzi Ya Aina Hii,.

Madhara Ya Mapenzi Ya Aina Hii,.

chakii

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2013
Posts
21,367
Reaction score
27,772
Habari Za Mwanzo Wa Wiki Wana-MMU!!

Ndugu zangu napitia katika wakati mgumu sana katika ulimwengu huu wa mapenzi,..

Takriban miezi nane iliyopita nilikuwa na mahusiano na msichana ambaye tulikuwa tukisoma wote chuo kimoja Jijini Dar,.

Huyu msichana katika mahusiano yetu hatujawahi kushiriki mapenzi kwa muda niliokaa naye kutokana na yeye kunizungusha na kunipiga mizinga ya hapa na pale ukizingatia sisi wote tulikuwa ni wanafunzi hivyo hali ya kiuchumi isingeruhusu mimi kumtimizia mahitaji yake yote hivyo nikaamua kuachana naye,.

Baada ya mwezi mmoja kupita wakati naelekea nyumbani nikiwa katika daladala nikakutana na rafiki wa yule msichana wangu wa zamani ambapo nilifanya naye mazungumzo kidogo maana sijawahi kupata wasaha wa kuwa naye karibu kwa kuhofia kuharibu mahusiano yangu na ya rafiki yake niliyemwacha,.

Mazungumzo yetu yalikuwa ya kufahamiana tu na pia nilifanikiwa kuchukua namba zake za simu na kumlipia nauli tukaahidiana kukutana siku iliyofuata chuoni,.


Wakati huo tulikuwa katika kipindi cha mitihani hivyo tuliamua kupeana muda kwanza wa maandalizi ya kumalizia mitihani ya muhula,.

Baada ya kumaliza mitihani tulipata wasaa zaidi wa kukaa pamoja na kujuana pia kusomana tabia za kila mmoja wetu,..

Katika kipindi cha kusomana tabia huyu msichana aliniuliza swali hili '' Je ushawahi kuwa na mpenzi kabla??'' mimi nilimjibu hapana lakini baadae alikuja kuniuliza mbona rafiki yake alimwambia kwamba mimi nilishamtongoza? Mimi nikamjibu kwamba hapana yule alikuwa rafiki tu sema kaamua kunichafulia tu kwako,.

Huyu msichana alikubaliana na mimi na kumpuuzia yule rafiki yake,.

Katika kipindi cha kuendelea kufahamiana na huyu binti alinismulia kwamba akiwa mdogo alibakwa ingawa mama yake alimuwahisha hospitalini ili apewe kinga endapo aliyembaka alikuwa na maambukizi ili asipate, hali yake ya afya ni njema na alishapima UKIMWI mara kadhaa yupo salama,.

Kwa kipindi kifupi nilichokaa na huyu msichana nimebaini siyo mtu wa makuu na anajali sana tofauti na yule wa mwanzo,.

TATIZO

1.Nimekuja kugundua kwamba huyu msichana niliye nae sasa sikumpenda kutoka moyoni ila ilitokea tu kuwa naye baada ya kukorofishana na rafiki yake niliyekuwa naye mwanzo,.

2.Huyu msichana inaelekea ananipenda kuliko ninavyompenda mimi na kabla sijawa nae ailiniambia kwamba alinipenda kabla hata ya mimi kukutana nae,.

3.Huyu msichana katika mazungumzo yetu tumekuwa tukizungumzia masuala ya kujenga familia siku zijazo,..


Wakuu naombeni mnisaidie ni njia gani sahihi niyaitumia kumuacha huyu msichana bila kumuumiza maana sitaki kumuumiza hata kidogo na mimi sipo tiyari kuwa naye tena!!!
 
Kua kwanza, naona mapenzi yanakuchanganya. Ila kumbuka, mkataa pema . . .
 
^^
Mwache polepole tu usimuumize maana binti mkweli kama huyo ni zawadi inayomfaa mwanaume mwenye uhitaji sio wewe usiejua unahitaji nini.
Usimwache ghafla ukamuumiza dada mtaratibu. Mwambie Maisha yatalipa upendo aliopoteza kwako
^^
 
^^
Mwache polepole tu usimuumize maana binti mkweli kama huyo ni zawadi inayomfaa mwanaume mwenye uhitaji sio wewe usiejua unahitaji nini.
Usimwache ghafla ukamuumiza dada mtaratibu. Mwambie Maisha yatalipa upendo aliopoteza kwako
^^

nimeona siyo chaguo langu mkuu!!
 
nimeona siyo chaguo langu mkuu!!

^^
Ulipotimiza haja zako..kesho ukimpata aliyechezewa kupita kiasi uje ulete mada hapa na sisi tutakushauri kwa kukuonea huruma bila kujali ulivyotenda wengine.
Anyway Mungu ni Mwema huyo Dada atapata mfariji mwema..Nenda salama na utakaempata akupende pia
^^
 
Una umri gani na unasoma kozi gani?
 
Mshukuru Mungu wanawake wengi ni wavumilivu...utamuacha ataendelea na maisha yake!ingekuwa wewe ndo huyu binti ungefanyaje????
Siku zote ulikua wap?
 
sikuzote mapenz ni kuridhiana na kupendana ikatokea kuwa mmja wenu hampend mwenzie mapenz kutakua hamna.mm,.ninacho kushauri ni mueleze yale yote ambayo yapo mwoyon mwako,,kuwa haumpendi ili akae akijua
 
sikuzote mapenz ni kuridhiana na kupendana ikatokea kuwa mmja wenu hampend mwenzie mapenz kutakua hamna.mm,.ninacho kushauri ni mueleze yale yote ambayo yapo mwoyon mwako,,kuwa haumpendi ili akae akijua

ahsante mkuu ndiyo nataka kujua namna gani nitamuelezea anielewe bila kumuumiza,..
 
Upendo unajengwa mara nyingine....alikuamini ndio maana amekushirikisha yaliyomtokea huko nyuma.
 
Upendo unajengwa mara nyingine....alikuamini ndio maana amekushirikisha yaliyomtokea huko nyuma.

kweli mkuu ndiyo maana akanishirikisha tatizo lililompata sema nitakuwa najilazimisha na italeta shida baadae,..
 
Ningekuwa sijampata mama yako mdogo hapa ningekuomba pande,nizoeane na huyo binti ,nimjenge kisaikolojia na ajue maana ya kupendwa ili awe wa kwanza kukuacha apate mume anayeheshimu wanawake na asiyependa kuona machozi ya kuumizwa!
Wee kijana vipi,kutwa tunashauri wenzio wanaotaka wenzi wa maisha wee unamtumia binti wa watu kisha unataka tupoteze mudas wetu adhimu kukufundisha namna ya kumwacha?
 
Sasa kwa nn uliruhusu ukaribu wakat wewe hukuwa na utayari? Je unadhan historia ya kubakwa ndo imechangia kwa wewe kumtoa thaman? Mapenzi hayaanzi kwa kupenda wewe ila yanachangizwa na mambo mengi. Kumbuka ulishaweka ushawishi kwa binti hivyo hata kama utaamua kumwacha bado utamuumiza
 
siwezi kugawa namba ya mtu bila ihari yake mkuu,..

Iloo! bado unamtaka!!!
Kujishembedua tu! lol!
...
Ebbos! Kwani nitamuambia kama nö umenipa wewe?
Au mi jambazi?
...
Nitajifanya nimekosea namba!
Alah! Wewe haumtaki tupe tunaomtaka ili tumliwaze!
Chezea Mashaxizo weyee!
 
Back
Top Bottom