Madhara ya limbwata

Madhara ya limbwata

Somoe

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2010
Posts
754
Reaction score
282
Shangazi yangu aliniambia ukimtilia mwanaume Libwata usha uua, yaani atakufa mapema, na kukuacha na watoto peke yako. Au ndio usha mlemaza akili, hawezi kuwa mwanaume kamili, na atashindwa kufanya majuku yake, na umasikini ndio usha ukaribisha hivo.

Washirikina wote kwenye koo yangu ni masikini sana, kuliko wote. Wengine kama wamelaanika hivi na watoto wao hawabarikiwi, wanaishi kwa maumivu maumivu. Magonjwa na maradhi ya ajabu ajabu.

Nilikuwa na rafiki wa kike kutoka Tabora, kuna siku aliniambia yeye anaenda kwa mganga wa kienyeji kuchukua chukua dawa ya mapenzi ili mumewe hasimuache, hasiwe na mchepuko, na awe anamuachia pesa nyingi.

Kuna siku yule mumewe akanifuata na kunitaka kimapenzi, nilishangaa na kujiuliza dawa zote zile hazifanyi kazi?Nilifikiri zile dawa ni majani ya mpapai tu ama kisamvu, kumbe ni sumu jamani.Miaka 7 baadae nikaletewa meseji na binamu yangu, yule mume wa rafiki yangu amefariki dunia. Nikakumbuka akiosema shangazi yangu limbwata sio zuri, kumbe ni kweli.

Nimekutana na marafiki wengi sana wananishawishi tuende kwa waganga, nawaambiaga namuamini mungu tu.Kama mtu hakupendi au anatabia mbovu mbovu bora kuachana nae kuliko kulazimisha akupende, kwa madawa.
Na wanaume mujue wanawake wa Dar hatari, wapo kimaslay yao tu. Musidandie dandie kila mwanamke, wengine hawamjui mungu, wanamjua shetani tu.

Babu yangu alikuwa Tabibu, mfuga majini, msoma albadili, na wengi walio kula dawa ya huyu mzee sio wazima kiakili, wasema ovyo. Hadi mama yangu walimtilia madawa alikuwa msema ovyo, mgonjwa na haeleweki.

Msile sile tu madawa ya waganga, mtaweuka akili. Jamaa mmoja alisema nitilie tu Limbwata nikikupenda sana ndio vizuri, utakufa.
 

Tena Dar wangefanyia mkazo, kwa sababu watu wengi wanaharibika na haswa wanaume. Utakuta wengi washachanganyikiwa akili, pesa wametapeliwa na mwanamke, limbwata linamsumbua kichwani anaongea ongea ovyo. Serikali na wazazi wa hawa watu wamepata hasara kumsomesha, kila mganga wa kienyeji. Na dar wangepiga fain kwa watoa libwata na walisha limbwata
 
sidhani kama kuna mwanamke anapenda kulazimisha mapenzi wanaume ndio wanaofanya wanawake kuwa mashetani
mtu kakutoa bikra kakuzalisha watoto 4 halafu ndo anaanza kula maisha wewe hata sura wala shape huna tena
unamuona na totoz mpya kila siku hata matunzo na watoto shida
lazima alipuliwe tu
 
Wanawake wenye mawazo finyu na mgando ndio wanaokimbilia kwa mganga..!
 
Hiyo inayoitwa limbwata haifanyi kazi.

Ni moja ya imani nyingi tu zilizo potofu.
 
yaani mpaka rafiki zako wanakufuata muende kwa waganga kupata limbwata maana yake huwa mnaenda kwa ajili ya mambo mengine

yaani unaonekana ni mtu wa hovyo hovyo
 
yaani mpaka rafiki zako wanakufuata muende kwa waganga kupata limbwata maana yake huwa mnaenda kwa ajili ya mambo mengine

yaani unaonekana ni mtu wa hovyo hovyo

Unashida ya kuelewa, sehem gani nimeandika rafiki au marafiki zangu wananifuata tuende kwa waganga?
 
Interesting.....

Unalishwa limbwata na mkeo
unalishwa na michepuko labda mitatu

ukienda kwa mama ntilie nae kuna uchafu anaweka 'kuvutia' biashara

basi ili mradi 'tunalishwa' takataka za kila aina
Kuna hata ndugu wanatengeneza ndugu zao waongeze huduma. Ukiongeza na hiyo basi mvurugano
 
Nimeyaona sana haya.

Kama mmeo ana fedha nyingi na wewe ni mama wa nyumbani, ukimlisha limbwata jiandae kuwa mtafutaji ktk familia maana mmeo ndo umeshampoteza hivyo.
 
sidhani kama kuna mwanamke anapenda kulazimisha mapenzi wanaume ndio wanaofanya wanawake kuwa mashetani
mtu kakutoa bikra kakuzalisha watoto 4 halafu ndo anaanza kula maisha wewe hata sura wala shape huna tena
unamuona na totoz mpya kila siku hata matunzo na watoto shida
lazima alipuliwe tu
Kuanzia leo sitakaa nikupm tena
 
Hizi mambo hazina faida yeyote zaidi ya kuongeza umasikini tu
 
Interesting.....

Unalishwa limbwata na mkeo
unalishwa na michepuko labda mitatu

ukienda kwa mama ntilie nae kuna uchafu anaweka 'kuvutia' biashara

basi ili mradi 'tunalishwa' takataka za kila aina
wanaume wanakula uchafu sana maana hilo limbwata mpk likolee lingine unaambiwa uweke nyama sehemu za siri halafu aile,lingine usugue taka za mwili ndo ale,lingine mate au ndonya la kimakonde bass tu mradi tupu!!

Mungu asaidie tuu!!!
 
1472306681850.jpg
 
Back
Top Bottom