Madhara ya kufanya tendo la ndoa hovyo hovyo!

Madhara ya kufanya tendo la ndoa hovyo hovyo!

Hata saratani ya kishingo ya kizazi kwa mwanamke!
Wataalamu wanasema kuwa, ile saratani huwa inambukizwa kutoka kwa mwanamme, akikuambukia unaweza kukaa miaka hata 20 ndio kitu kinalipuka, hivyo hiyo chovya chovya mwanamke waweza kukutana na mwenye hivyo virusi
 
Wana MMU habari za majukumu?

Leo naomba tuangalie madhara ya kufanya tendo la ndoa hovyo hovyo, nikisema hovyo hovyo nina maana ile tabia ya kutaka kuzini na kila mwanamke au mwanaume unayemtamani.

Kufanya tendo la ndoa na kila mwanamke au mwanaume kuna madhara mengi sana,Leo ntataja machache.

1. Hushusha heshima ya mtu husika.
Kufanya tendo la ndoa hovyo hovyo huitwa zinaa, zinaa husababisha mfanyaji aonekane ni mtu asiheshimika wala kuaminiwa na jamii.

2.Huharibu mahusiano kati ya mtu husika na Mungu.

3. Humuweka muhusika mbali na Mungu

4. Hujenga mazoea ya kutotulia na mwanamke au mwanaume mmoja hata baada ya kuoa au kuolewa.

5. Hupelekea kupata magonjwa ya zinaa kama vile ukimwi,gono , kaswende na kadharika.

6. Hupelekea mwili kuchoka na kuzeeka haraka.

Hayo ni baadhi tu ya madhara ya zinaa.

Geuka acha zinaa , mrudie Mungu wako.
Unawezaje kukaa na silaha bila kuifanyia mazoezi
 
Back
Top Bottom