Madhara ya bunge kujaa WanaCCM yameonekana

Sexless

JF-Expert Member
Mar 11, 2017
21,563
50,407
Madhara ya bunge
(a) Kujaa wanaccm,
(b) Kuwa chombo cha kuimba nyimbo za sifa badala ya chombo cha kuisimamia na kuikosoa serikali,
.....yamedhihirika katika sakata la tozo za miamala. Rais anaanza SSH ameanza kupata tabu.

Wakati wa vikao vya bunge kujadili bajeti 2021/2022, wabunge wengi walijikita kutoa sifa kwa rais badala ya kuangalia mijadala iliyopo mezani na kuichambua ipasavyo.

Sasa Rais Samia amelazimika kuagiza tozo hizo ziangaliwe upya wakati kulikuwa na zaidi ya watu 365 waliolipwa posho nene kufanya kazi hiyo.

Ndugai ameboronga, tena amebutua ajitafakari ktk hili kisha ajiuzulu.
.
 
Twambie kipindi kina Lissu wamejazana bungeni waliwahi kuzuia nini kisipitishwe?
 
Twambie kipindi kina Lisu wamejazana bungeni waliwahi kuzuia nini kisipitishwe?
At least walikuwa wanapiga kelele kuonyesha concern na kupinga lakini likija suala la kupiga kura wanazidiwa kwa kuwa wabunge wengi wanakuwa ni chama cha mboga mboga AKA nzi wa kijani.

Sasa hivi hakuna hata mbunge mmoja aliyeonyesha kuwa upande wa wananchi kwenye hii issue ya tozo hizi za kibaradhuli, wabunge wamekuwa watetezi wa serikali na wala si watetezi wa wananchi.

Labda kwa sababu waliwekwa na serikali kwani honestly hawakuchaguliwa na wananchi hence wako sahihi kutojali maslahi ya wananchi.
 
Kabisa mkuu. Angalia hivi Sasa eti mtu mmoja tu (rais) anatamka kutengua maamuzi ya bunge lililokaa kwa miezi 3 na posho wamelipwa. Sasa kama rais anafuta maamuzi ya bunge, uwakilishi wa wabunge kwa wananchi uko wapi?
Huyu maza ni mnafiki balaa, budget inaanzia kwenye baraza la mawaziri
 
Back
Top Bottom