VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,140
- 18,004
Hali ni tete katika Mizani ya Mailimoja Kibaha,Pwani ambapo madereva wa malori wamefunga barabara. Kufungwa kwa barabara hiyo kwa makusudi kunasababisha adha kubwa kwa magari na abiria wanaosafiri kutoka au kwenda Dar es Salaam kupitia Mizani hiyo ya Kibaha. Madereva wa malori ya kusafirisha mizigo kwenda nchi jirani kama Rwanda,Burundi,Zambia na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Mgomo huo umefuatia kupunguzwa ghafla na bila taarifa kwa uzito unaostahili kupita kiuhalali katika Mizani hiyo. Taarifa toka eneo la tukio ambapo nilikuwepo zinaonesha kuwa Serikali imepunguza uzito kwa mizito inayopimwa hapo. Hatahivyo,madereva wote na matajiri yao hawakuujua uamuzi huo na hivyo kujikuta leo wakionekana kuwa wamezidisha uzito. Hii ni karibu kwa kila lori.
Taarifa zinaonesha kuwa kwa sasa,muda si mrefu, Serikali imetangaza na kuamuru barabara ya Morogoro ifunguliwe haraka iwezekanavyo. Madereva wa malori walioyazima kwa kuziba barabara hawapatikani. Hakuna wakuyaendesha. Wamegomea uamuzi wa ghafla wa Serikali kwa kupunguza uzito unaoruhusiwa kisheria.
Taarifa zinaonesha kuwa kwasasa foleni ya magari iko Ubungo,Dar es Salaam na Ruvu Sekondari,mkoani Pwani. Mamia ya wananchi wanatembea kwa umbali mrefu leo kurejea makwao. Ni adha kuu. Ni hatari. Hali si vutizi. Ni ya kuogofya.
Kwanini mambo haya? Waziri Mwakyembe na Waziri Magufuli mko wapi?
Mzee Tupatupa(safarini kwa pikipiki kurudi Dar)