Nimefanya kazi kama school bus driver shule ilikuwa mbezi chini,
Route yangu ni Tegeta, mashamba ya jeshi, madale, Mivumoni
Kipindi hicho hamna barabara ya lami na kila mtu sheria ya shule ni umchukulie nyumbani kwao, na humrudishe kwao plus usumbufu wa wazazi mbona umechelewa kumleta mtoto au umechelewa kumrudisha mtoto!
Matokeo yake kulinda ajira zao hao madereva wanatembea hivyo!
Suluhisho madereva wa mabasi ya shule wawe na
Mikataba ya ajira atleast hata kwa miaka 3 renewable.
Kuwa na mda wa kutosha kutoa huduma atleast masaa 3-4 kwa asubuhi na jioni. Yaani kama kuanzia saa 11- 2 asubh na kwa jioni 9-12:30.
Kuwa na mda maarumu wa kupitiwa kwa mtoto gari ikifika hujamuaandaa heri wa waondoke, utampeleka mtoto mwenyewe.
At least tutapunguza hizi changamoto kwa kiasi kikubwa.