Madereva bajaji, bodaboda waonywa kushiriki maandamano yasiyo na vibali

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Madereva wa pikipiki, maarufu kama bodaboda na wale wa bajaji, wameonywa kujiingiza katika maandamamo yasiyo na vibali kutoka polisi katika kipindi cha kampeni za uchaguzi.

Onyo hilo lilitolewa jana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Wilbroad Mutafungwa, wakati wa kikao cha pamoja na madereva hao kwa lengo la kuwatahadharisha juu ya wanasiasa ambao wanalenga kuwatumia vijana vibaya katika kufanya siasa zao.

Alisema katika kipindi cha hivi karibuni, kumezuka tabia ya baadhi ya wanasiasa kuwarubuni madereva wa vyombo hivyo kwa kuwanunulia mafuta kisha kuwaingiza katika maandamano yasiyo na vibali.

“Hakikisheni hamshiriki katika maandamano ya kisiasa ambayo hayana kibali maalumu kutoka polisi kwani kufanya hivyo ni kinyume cha sheria kwa sababu watawanunulia mafuta lita moja kisha mkajiingiza katika vitendo vya uvunjifu wa sheria,” alisema Mutafungwa.

Aliwataka madereva hao kufanya kazi zao kwa kuzingatia sheria na endapo watatakiwa kusafirisha makada wa vyama kwenda katika mikutano ya siasa, wahakikishe hawajiingizi katika vitendo vya uvunjifu wa amani.

Kwa upande wao, madereva hao waliliomba jeshi hilo kusimamia sheria bila upendeleo hasa wakati huu ambao nchi inaelekea katika uchaguzi mkuu na kubaini wahalifu ambao wanalenga kuichafua kazi yao.

Walisema katika kipindi hiki cha kampeni, baadhi ya watu ambao si waaminifu hujitokeza na kufanya vurugu kwa kutumia pikipiki au bajaji, kitendo ambacho walisema kinachafua taswira ya kazi wanayoifanya.
 
Hawa mapolisi inabidi watupatie tafsiri ya neno wanasiasa.

Ina wezekana kuwa wanasiasa ni wale wa upande wa upinzani tuu. Ila wale wa fisiem wao ni watumishi wa serikali ambao hata wakiandamana wako kwenye majukumu yao ya kikazi.

In short hawa wapolice ndo adui wakubwa wa democracy ya nchii hii.

Kila inapofika wakati wa uchaguzi utaona wanawakaripia vijana na kutoa matamko ya ajabu ajabu ambayo yanadumaza watu kushiriki kwenye shughuli za kuchagua viongozi wanao wataka.
 
Huyu jamaa alifeli wakati wa janga la moto ambapo ndugu zetu wengi waliteketea lakini kwa makusudi amelindwa, na yeye anajua, hivyo hataweza kutulia lazima aseme chochote.
 
Back
Top Bottom