Madenge ajipanga jimbo la Iringa Mjini

Madenge ajipanga jimbo la Iringa Mjini

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Posts
15,860
Reaction score
5,803
JANUARY 16, 2013


MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Manispaa ya Iringa, Mahamoud Madenge ameanza kazi ya kufa na kupona itakayowasaidia kulirejesha mikononi mwao jimbo la Iringa Mjini katika Uchaguzi Mkuu ujao.

Jimbo hilo ambalo toka uchaguzi uliohusisha vyama vingi vya siasa uanze mwaka 1995 limekuwa likiongozwa na CCM, hivi sasa linaongozwa na Mchungaji Peter Msigwa wa Chadema.

Madenge ambaye pia ni mfanyabiashara anayemiliki kiwanda cha maji aina ya Ndanda ameainisha kazi kubwa nne zikazowasaidia kufikia lengo hilo.

Kazi hizo ni pamoja na kukagua uhai wa chama kuanzia ngazi ya shina hadi wilaya na kuwakumbusha wanachama na wapenzi wa chama hicho misingi, madhumuni na itikadi ya chama hicho.

"Nimeanza kutembelea wanachama wetu katika ngazi ya shina, tawi na kata na kwa kushirikiana na viongozi wenzangu tunatoa darasa ili waifahamu itikadi ya chama, misingi na madhumuni yake,"
alisema.

Alizitaja kazi zingine kuwa ni kuhakikisha watendaji katika ngazi mbalimbali za serikali wanatekeleza Ilani ya CCM kama ilivyoelekezwa.

"Nitahakikisha mafanikio na changamoto zake naziwasilisha katika kikao cha Halmshauri Kuu ya Taifa ili hatua zinazostahili zichukuliwe," alisema.

Alisema kazi ya nne itakuwa kufanya mikutano ya hadhara na ya ndani na makundi mbalimbali ya jamii ili kueleza utekelezaji wa Ilani na kusikia changamoto zinazowakabili wananchi ili zifanyiwe kazi.

Alisema chama hicho mjini hapa kitaanza kujibu mapigo ya wapinzani wao wakubwa wa kisiasa ambao ni Chadema kwa kuzindua rasmi mikutano yake ya hadhara kwa kuwaalika viongozi mbalimbali wa CCM wa ngazi ya Taifa.

"Tarehe 26 mwezi huu wa kwanza tutaanza na Makamu Mwenyekiti wetu Mzee Phillip Mangula, na baadaye tutaleta wengine wengi kwa kuzingatia mapendekezo ya wanachama na wananchi," alisema.

Alisema wanaendelea pia kujipanga kulifikia kundi la vijana wa matabaka mbalimbali ili kusikiliza vilio vyao na hatimaye kwa pamoja waje na mapendekezo yatakayolenga kuboresha hali zao.

Madenge alichaguliwa kuwa mjumbe wa NEC katika Uchaguzi Mkuu wa chama hicho uliofanyika mwishoni mwa mwaka jana baada ya kuwashinda Vitus Mushi ambaye ni Diwani wa Kata ya Mtwivilla mjini hapa na mfanyabishara Michael Mlowe.


Source; IRINGA YETU


 
Oh... MCHUNGAJI kapata MPINZANI toka CCM; Mmiliki wa KIWANDA!!!
 
mkuu ... yule masalia wa UK Chris Lukosi nae analitaka hilo jimbo ....

he is barking at flying birds .... haa haaaaa

LOL CHRIS LUKOSI anatakiwa arudi bongo then; Sababu hajui MAENDELEO yakoje huko IRINGA MJINI... Anasifia LAMI DAR ARUSHA... Anahitaji kuongea na WanaIRINGA MJINI...
 
Madenge hapo juu hajasema kwamba atagombea yeye ubunge. Anasema anafanya kazi ya chama kulirudisha jimbo CCM.

Jimbo hilo litakuwa moto 2015 maana hata Mwakalebela bado yupo.
 

LOL CHRIS LUKOSI anatakiwa arudi bongo then; Sababu hajui
MAENDELEO yakoje huko IRINGA MJINI... Anasifia LAMI DAR ARUSHA... Anahitaji kuongea na WanaIRINGA MJINI...
Haya sasa ya Sioi kule Arumeru Mashariki. Mwishowe kaolewa.............. Haaaaah haaaaa!!!!!!!!!!!!!!!!

Alikuwa akishindwa hata kutaja vijiji vya Arumeru.
 
Uhuru wa kuchagua na kuchaguliwa, 2015 mgombea binafsi lazima nikachukue jengo la magogoni
 
Oh... MCHUNGAJI kapata MPINZANI toka CCM; Mmiliki wa KIWANDA!!!

Mkuu nakuaminia kazi uliyo nayo ni Ngumu sana, naona unabidii ya hali a Juu, kila thread unao anzisha ni lazima uchangie kwanza mwenyewe hii ni kama ya tatu naona unakomaa kwanza, kuvutia watu
 
Uhuru wa kuchagua na kuchaguliwa, 2015 mgombea binafsi lazima nikachukue jengo la magogoni


Katika DEMOKRASIA ya DUNIA hii... hata NCHI wanayosema ina DEMOKRASIA kupita zingine DUNIANI INDIA hawana MGOMBEA BINAFSI... sababu ina-UBINAFSI...

Hata USA wana so called INDEPENDENT CANDIDATES for Congress and SENATE lakini wakiingia BUNGENI lazima wawe affiliated na CHAMA either REPUBLICAN or DEMOCRAT's caucases...

Kwasababu USA wanaona a INDEPENDENT PRIVATE CANDITATE inaleta MGAWANYIKO; UBINAFSI na PIA kusababisha RUSHWA sababu kwenye UPIGAJI KURA kwa MASUALA MBALIMBALI kama sio AFFILIATED na chama chochote UNAWEZA kuharibu DEMOKRASIA...

*** HAKUNA NCHI YENYE PRIVATE CANDIDATE DUNIANI... TANGANYIKA itakuwa ya kWANZA na hapo ndipo HAYO MAKABILA 139 na ZAIDI yataanza kubaguana... TUCHUNGE TUNACHOTAKA KIBINAFSI; KITATUDHURI KIBINAFSI...
 
Mkuu nakumania kazi uliyo nayo ni Ngumu sana, naona unabidii ya hali a Juu, kila thread unao anzisha ni lazima uchangie kwanza mwenyewe hii ni kama ya tatu naona unakomaa kwanza, kuvutia watu

Kwasababu HOJA ninazoweka napenda KUZIJADILI na NINAHITAJI Msaada kuhusu HOJA; kwahiyo Napenda kuchangia kuonyesha MSIMAMO wangu kuhusu hizo HOJA ninazopost... Iwe ya KISIASA au MICHEZO
 
Mh. Madenge atatusaidia wana iringa.. karibu sana Mbunge mtarajiwa, lukosi hatumjui
 
Kuna watu wako Huku yaani hawa juu hata historia. Mfano kuna mandishi mmoja anaitwa Dennis Luambano alikuwa o level nikia A level pale Tosa aliandika kwenye masala yake Kuwa Mbowe hawezi kupewa nchi Kwa sababu hajawahi Kuwa hata balozi wa nyumbani kumi. Nikamwambia ( nikamfundisha Kuwa alikuwa mbunge wa hai 2000-2005) akashangaa. Sasa Leo nasoma hapa nngu007 ameandika eti jimbo la Iringa mjini limekuwa chini ya CCM tangu 1995 hadi lilipochukuliwa Na mchungaji Msigwa. Uongo wa dhahiri. 1995 mbunge Mfwalamagoha Kibasa wa lNCCR alikuwa mbunge hadi 2000 lilipochukuliwa Na gamba Monica Mbega.
 
Jimbo la Iringa liliwahi kuwa chini ya NCCR mwaka 1995,hivo Nngu acha upotoshaji kwamba Ira imekuwa ya ccm tangu 1995
 
mkuu ... yule masalia wa UK Chris Lukosi nae analitaka hilo jimbo ....

he is barking at flying birds .... haa haaaaa
Sasa sijui CCM tutamteua nani, maana kila mtu anataka kugombea, tulisikia Christ Lukosi(Masalia-mbeba box) akitangaza nia na sasa Madenge naye tena, hapo hapo Mama Monica Mbega hajakata tamaa 2015 atajaribu tena bahati yake lakini David Mwakalebela kashasema 2015 lazima aingie kwenye kinyang'anyiro na CCM wasipomteua patachimbika!!
 
Nimemsikiliza jana redio ebony fm nkaona hana jipya sana hasa pale aliposema ccm hakuna mafisadi kabisa,nkafunga redio
 
Mama Kabati la vyombo nae si analitaka jimbo hili!
 
huyu jamaa hajakata tamaa ya Ubunge tu?mwaka 1995 akiwa NCCR Mageuzi aligombea Ubunge la Isimani kama sijakosea,akapoteza.Mwaka 2000 akagombea Jimbo la Kawe kwa tiketi ya TLP,akaangukia pua.
 
Nimemsikiliza jana redio ebony fm nkaona hana jipya sana hasa pale aliposema ccm hakuna mafisadi kabisa,nkafunga redio

kama ulitegemea Madenge achukizwe na ufisadi ulikosea sana, huyu jamaa proffessional yake ni "Uhalifu wa Silaha",ana damu nyingi mikononi mwake.
 
Back
Top Bottom