Madenge ajipanga jimbo la Iringa Mjini

Madenge ajipanga jimbo la Iringa Mjini

kama ulitegemea Madenge achukizwe na ufisadi ulikosea sana, huyu jamaa proffessional yake ni "Uhalifu wa Silaha",ana damu nyingi mikononi mwake.
Butola,,, haumfahamu vizuri nadhani, ni mwanaharakati mzuri na mpigania haki
 
Iringa ni ya wana-iringa bhana,, mushi aende kwao
 
mkuu ... yule masalia wa UK Chris Lukosi nae analitaka hilo jimbo ....

he is barking at flying birds .... haa haaaaa
Kutangaza nia ni haki ya kila mtanzania,
Wakati utakapofika ndio tutajua nani mwenye nia nzuri na nani anayekimbilia mjengoni kufuata posho na shangingi
Chilisosi ataanza kwa vitendo na kumalizia kwa maneno, wengine wataanza na mikutano na kumaliza kwa mikutano na ahadi nyingi.
Dawa ni kutimiza hata kabla hujaahidi
 
JANUARY 16, 2013


MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Manispaa ya Iringa, Mahamoud Madenge ameanza kazi ya kufa na kupona itakayowasaidia kulirejesha mikononi mwao jimbo la Iringa Mjini katika Uchaguzi Mkuu ujao.

Jimbo hilo ambalo toka uchaguzi uliohusisha vyama vingi vya siasa uanze mwaka 1995 limekuwa likiongozwa na CCM, hivi sasa linaongozwa na Mchungaji Peter Msigwa wa Chadema.

Madenge ambaye pia ni mfanyabiashara anayemiliki kiwanda cha maji aina ya Ndanda ameainisha kazi kubwa nne zikazowasaidia kufikia lengo hilo.

Kazi hizo ni pamoja na kukagua uhai wa chama kuanzia ngazi ya shina hadi wilaya na kuwakumbusha wanachama na wapenzi wa chama hicho misingi, madhumuni na itikadi ya chama hicho.

“Nimeanza kutembelea wanachama wetu katika ngazi ya shina, tawi na kata na kwa kushirikiana na viongozi wenzangu tunatoa darasa ili waifahamu itikadi ya chama, misingi na madhumuni yake,”
alisema.

Alizitaja kazi zingine kuwa ni kuhakikisha watendaji katika ngazi mbalimbali za serikali wanatekeleza Ilani ya CCM kama ilivyoelekezwa.

“Nitahakikisha mafanikio na changamoto zake naziwasilisha katika kikao cha Halmshauri Kuu ya Taifa ili hatua zinazostahili zichukuliwe,” alisema.

Alisema kazi ya nne itakuwa kufanya mikutano ya hadhara na ya ndani na makundi mbalimbali ya jamii ili kueleza utekelezaji wa Ilani na kusikia changamoto zinazowakabili wananchi ili zifanyiwe kazi.

Alisema chama hicho mjini hapa kitaanza kujibu mapigo ya wapinzani wao wakubwa wa kisiasa ambao ni Chadema kwa kuzindua rasmi mikutano yake ya hadhara kwa kuwaalika viongozi mbalimbali wa CCM wa ngazi ya Taifa.

“Tarehe 26 mwezi huu wa kwanza tutaanza na Makamu Mwenyekiti wetu Mzee Phillip Mangula, na baadaye tutaleta wengine wengi kwa kuzingatia mapendekezo ya wanachama na wananchi,” alisema.

Alisema wanaendelea pia kujipanga kulifikia kundi la vijana wa matabaka mbalimbali ili kusikiliza vilio vyao na hatimaye kwa pamoja waje na mapendekezo yatakayolenga kuboresha hali zao.

Madenge alichaguliwa kuwa mjumbe wa NEC katika Uchaguzi Mkuu wa chama hicho uliofanyika mwishoni mwa mwaka jana baada ya kuwashinda Vitus Mushi ambaye ni Diwani wa Kata ya Mtwivilla mjini hapa na mfanyabishara Michael Mlowe.


Source; IRINGA YETU




Alie tu, kama amekosa ukuu wa wilaya kwa JK, asitegemee kupata hata uenyekiti wa mtaa 2015 kupitia ccm
 


Katika DEMOKRASIA ya DUNIA hii... hata NCHI wanayosema ina DEMOKRASIA kupita zingine DUNIANI INDIA hawana MGOMBEA BINAFSI... sababu ina-UBINAFSI...

Hata USA wana so called INDEPENDENT CANDIDATES for Congress and SENATE lakini wakiingia BUNGENI lazima wawe affiliated na CHAMA either REPUBLICAN or DEMOCRAT's caucases...

Kwasababu USA wanaona a INDEPENDENT PRIVATE CANDITATE inaleta MGAWANYIKO; UBINAFSI na PIA kusababisha RUSHWA sababu kwenye UPIGAJI KURA kwa MASUALA MBALIMBALI kama sio AFFILIATED na chama chochote UNAWEZA kuharibu DEMOKRASIA...

*** HAKUNA NCHI YENYE PRIVATE CANDIDATE DUNIANI... TANGANYIKA itakuwa ya kWANZA na hapo ndipo HAYO MAKABILA 139 na ZAIDI yataanza kubaguana... TUCHUNGE TUNACHOTAKA KIBINAFSI; KITATUDHURI KIBINAFSI...
what is your argument? maana hauwezi kuwa senator or member of congress bila kuchaguliwa. Kuhusu affiliation thats after election. what is your point?
 
what is your argument? maana hauwezi kuwa senator or member of congress bila kuchaguliwa. Kuhusu affiliation thats after election. what is your point?

My Point Is there is no PRIVATE Candidate for either Member Of Parliament Or Senate
 
Kama haujui historia yake ya "Uhalifu" basi haumjui Madenge.

Si vibaya kama ungetueleza moja ya matukio yake ya uhalifu; hivi sasa tunapata wakati mgumu kuamini maneno yenu; kama hoja ni uhalifu chunguza safu yako ya wabunge wapo wengi tu ndani ya Chadema au unataka kutuambia safu yako ina watakatifu?

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Iringa ni ya wana-iringa bhana,, mushi aende kwao

Yameshakuwa hayo tena ya kubaguana? Kuna kina Mushi wamezaliwa Iringa hata huko Machame hawakujui sasa wakagombee wapi?

Chama
Gongo la mboto DSM
 
francis kazi unayo,kweli wewe anti msigwa damu,sijawahi kukusikia ukimsifu hata afanye jema,haya bwana fanya kazi yako vizuri binadamu watakulipa
 
Yameshakuwa hayo tena ya kubaguana? Kuna kina Mushi wamezaliwa Iringa hata huko Machame hawakujui sasa wakagombee wapi?

Chama
Gongo la mboto DSM
Ndo ivo, Natives Chama, c WAO wamesimamia sera ya majimbo? Ukanda ukanda tu kwa sasa
 
Si vibaya kama ungetueleza moja ya matukio yake ya uhalifu; hivi sasa tunapata wakati mgumu kuamini maneno yenu; kama hoja ni uhalifu chunguza safu yako ya wabunge wapo wengi tu ndani ya Chadema au unataka kutuambia safu yako ina watakatifu?

Chama
Gongo la mboto DSM

Mkuu wangu sana,mie sio Chadema na mpaka sasa sijaona jambo kubwa alilolifanya Msigwa pale Iringa litakalonifanya nimsikitike akiangushwa 2015,hapana.


Na ninaamini bado kuwa CCM ni chama kikubwa na ndani yake kina watu wengi wenye uadilifu wa kushika nafasi ya Ubunge.


Hofu yangu ni CCM kuzembea sana sikuhizo na kupelekea kuwapa uongozi watu ambao uadilifu wao ni wa mashaka makubwa,ni fedhea na ukosefu wa umakini kwa chama tawala.
 
Oh... MCHUNGAJI kapata MPINZANI toka CCM; Mmiliki wa KIWANDA!!!

Wewe si ndiye yule mwandishi uliyekuwa ukitumiwa kupeleka habari za CDM,wakati ule wapo Iriinga kabla ya kifo cha Mwangosi, na uliyepanga na watu wako kuwa Msiba wa Mwangosi usiwe wa Kisiasa na wakati ulishachukua Ml 1 toka kwa wenzio kuzuia Cdm wasihusike na msiba, vipi uko kazini tena?
 
Wewe si ndiye yule mwandishi uliyekuwa ukitumiwa kupeleka habari za CDM,wakati ule wapo Iriinga kabla ya kifo cha Mwangosi, na uliyepanga na watu wako kuwa Msiba wa Mwangosi usiwe wa Kisiasa na wakati ulishachukua Ml 1 toka kwa wenzio kuzuia Cdm wasihusike na msiba, vipi uko kazini tena?

??? Sielewi Unachokisema... Una Maanasha MWANDISHI au MIMI?
 
Back
Top Bottom