Madawa ya Kulevya na aibu ya Tanzania - Yatosha sasa!

Ndugu wana jf nimekaa kutafakari nimegundua kua hii ishu iliyo vuma sana ya madawa ya kulevya ni kama serikali inacheza na akili zetu tunaambiwa siku zote kwamba serikali inajukumu la kuwalinda raia wake dhidi ya majanga yeyote lakin hapa imekua tofauti mimi nilitegemea kwamba wauza unga wangeanza wao kupiga kelele kwamba unga hauwezekaniki kuingia nchini kwasababu serikali imedumisha ulinzi wa kutosha katika mipaka yake yote lakini ninapata mashaka kuona serikali ambayo ndio inamiliki mipaka yote ambayo ndio madawa hupitishwa wao ndio wanalalama asa ninajiuliza hivi hawa wanao ingiza haya madawa hua wanamiliki baadhi ya mipaka ya nchi yetu?. Na je tunahaki ya kuiwajibisha serikali kwa kuwa imeshindwa kutekeleza jukumu lake dhidi ya raia wake? Au wameamua kuwaruhusu waingize afu waanze kutafutwa na kuchafuliwa ambao hawahusiki? Na je serikali inapo laumu kuhusu suala hili sisi wananchi tumlaumu nani?
Naomba kuwasirisha
 
Wana jamii

Salaam

Katika vita ya kupambana na madawa ya kulevya ingekua vyema ikageukia kwa watumishi wote wa umma ili kulinda afya zao na mustakabali wa familia zao kwa ujumla, Aidha ili kuleta ufanisi zaidi katika maeneo ya utumishi ni bora sasa watumishi wote wa umma wapimwe na kutoa ushirikiano, Madawa ya kulevya hapo katika makundi mengi Kama vile Mirungi,Bangi, Heroine, Cocainne, Madrax na mengine mengi.
Huo ni ushauri kutoka halmashauri yangu ya kichwa tu
 
Inawezekana Makonda ana makosa mengi mojawapo ni kutaja majina ya watuhumiwa kama wakosaji bila mahakama kutoa hukumu bila shaka. Lakini kiongozi gani ana guts za kutaja viongozi au watu mashuhuri wenye mahusiano na matumizi ya madawa ya kulevya? Ni Makonda tu, ingawa leo kashindwa kutaja watu mapapa katika phase three lakini bado Makonda ana dhamira nzuri sana ambayo Mheshimiwa Rais Kaiboresha!!!
 
Ile story aliyotupigia mzee makonda ya jinsi madawa yanavyo ingia hata mtoto wa darasa la pili anaweza leta story nzuri zaidi. Ilikua ni ya kutunga na mtunzi hakukaa kufikiria vizuri. akaja na misamiati ambayo hata yeye mwenyewe hajui maana yake eti GPRS badala ya GPS.

Sijui anatuonaje watanzania, hadi kuja na hadithi za abunuwasi badala ya kukaa chini na kuweka Sera za kuwasaidia watu hapa mjini.

Nitaimiss sana hii movie.. ni zaidi ya bongo movie zile ambazo jambazi linavua viatu linapo ingia nyumba ya MTU kuiba.
 
Ndugu wana jf nimekaa kutafakari nimegundua kua hii ishu iliyo vuma sana ya madawa ya kulevya ni kama serikali inacheza na akili zetu tunaambiwa siku zote kwamba serikali inajukumu la kuwalinda raia wake dhidi ya majanga yeyote lakin hapa imekua tofauti mimi nilitegemea kwamba wauza unga wangeanza wao kupiga kelele kwamba unga hauwezekaniki kuingia nchini kwasababu serikali imedumisha ulinzi wa kutosha katika mipaka yake yote lakini ninapata mashaka kuona serikali ambayo ndio inamiliki mipaka yote ambayo ndio madawa hupitishwa wao ndio wanalalama asa ninajiuliza hivi hawa wanao ingiza haya madawa hua wanamiliki baadhi ya mipaka ya nchi yetu?. Na je tunahaki ya kuiwajibisha serikali kwa kuwa imeshindwa kutekeleza jukumu lake dhidi ya raia wake? Au wameamua kuwaruhusu waingize afu waanze kutafutwa na kuchafuliwa ambao hawahusiki? Na je serikali inapo laumu kuhusu suala hili sisi wananchi tumlaumu nani?
Naomba kuwasirisha
vita hii kimitazamo ni kubwa kwa savabu unagusa moja kwa moja vyombo vya kiusalama kwa namna moja au nyinge kutokana nq hali halisi hivyo basi wakitaji kupambana mabadiliko lazima yafanyike ila viapo tu aitoshi pesa inakiwa inanguvu sana kuliko kingne Je ? wameboreshewa mazingira mazuri yanayowapelekea kuipiga rushwa sauti yako sheria ila pesa inakiwa ina nguvu kuliko sheria kwa ujumla najua mtakuwa mnajua hata takukuru wanajua sababu zinazopelekea mtu kupokea rushwa ni zipi ninachomanisha na kukizungumza ni sababu moja wapo . inafika wakati unauliza nani wakulaumiwa ? katika hilo
 
List 2 za awali zimejaa wapinzani tu, wachache sana watu wa upande wa mtajaji, je ni ni coincidence au ndio dhamira kuu?
  1. Mwanasiasa mkuu wa chama pinzani!!!
  2. kiongozi wa dini mpinzani!!!
  3. Mmiliki wa radio pinzani!!
  4. Mwenyekiti wa timu pinzani!!
  5. Msanii wa kundi pinzani!!
Katika maisha ya kiintelijensia ni muhimu sana kuangalia patterns, sisemi kuwa list sio sahihi ila kuna pattern ya kuitazama!
 
Mkuu hii operation ililenga kuwadhalilisha wapinzani. Kwa bahati; kuujibu hii operation, zimetumika njia zilizojipanga kwa mapenzi ya Mungu.

1. Gwajma kasemehe

2. Mbowe kakataa kwenda polisi kaenda mahakamani

3. Manji ndiyo hivyo tena

4. Wasanii wametumiwa kama chambo.

Sasa tujiulize kama si udikteta uchwara ni nini?

Kibaya zaidi wanejiumbua hakukuwa na uongozi wa tume inayohusika. Uthibitisho wa wazi wa ujinga na upumbavu wao.

Mimi naona reaction zitakuwa za pole pole lakini zenye madhara kwa watawala na chama dola. Ni rahisi sana kwa sababu hakuna action isiyo na reaction. Ni kanuni ya maisha
 
Kujenga viwanda kunahitaji pesa ya kigeni ambayo hatuna, jamani tushindwe hata kupambana na madawa ya kulevya? aaaaa jamani are we serious? hebu tujaribuni kwa pamoja tuone tutafika wapi kabla ya 2020!!
 
Pamoja na mambo mengine, vita ya konda ililenga pia kupunguza dola za marekani kwenye mzunguko. Ameona wajanja wengi siku hizi wanatunza hela zao kwenye dola kutokana na kasi ya kuporomoka kwa shilingi.

Alidai maduka ya fedha za kigeni yana dola nyingi kuliko maelekezo ya BoT. Mengine yanafanya transactions za hadi dola milioni 1 kwa siku.

Kwa kisingizio kwamba yanatumiwa na watu wa ngada anataka ayadhibiti maduka hayo yasibadilishe zaidi ya $100000 kwa siku, kiasi kingine watunze benki kuu, ambako kuzitoa lazima wawe na sababu za msingi za kuridhisha watawala.

Kama ambavyo walichukua fedha za serikali na kuzificha BoT na kuacha hali ngumu mtaani wanataka sasa kukusanya dola za bureau de change na kuziweka BoT kwa kisingizio kwamba wanawatunzia.

Kilichomponza Gwajima ni pale aliposema akitoka nchini analipwa dola 1000 kwa saa, konda akamuweka kwenye list ili apate nafasi ya kumsachi na kumdadisi anakotoa na anakotunzia dola. Nasikia anataka kumfungulia kesi ya utakatishaji pesa wakati ni jasho lake.

Yamkini Manji ameponzwa na masuala hayo pia.

Inaelekea kuna upungufu wa fedha za kigeni BoT, hivyo konda (kwa maelekezo toka juu) anataka kupunguza dola kwenye mzunguko wakidhani kwamba malipo yote yakifanyika kwa shilingi thamani ya shilingi itapanda. Kumbe kwa kufanya hivyo dola itaadimika zaidi na bei yake itapanda.

Chanzo cha hali ngumu ni ukiukwaji wa demokrasia uliopelekea ukosefu wa pesa kwa serikali, na ikaamua kupunguza pesa mtaani na kukwapua misaada ya wahisani. Sasa inawanyanyasa wafanyabiashara wakubwa ili ikwapue hela zao. Kusaka walioficha hela sio suluhisho.

Serikali haitakuza uchumi kwa dhuluma na ubabe, iache soko huria litamalaki, nayo ikusanye kodi ndogo iliyopo kwa muda mrefu kuliko kuua biashara za watu au kuwavunja moyo kuanzisha biashara kubwa na kujenga viwanda. Manyanyaso haya yatapunguza mapato ya serikali na yataongeza hasira za watawala (konda na babake), kwani wataogopa kuulizwa kwa nini hali ni ngumu kuliko awamu iliyopita.

Wajiangalie kutokana na hasira zao ipo siku wananchi wanaweza kusema sasa inatosha.

Mtu aliyechafuliwa jina haweze tena kujenga viwanda, ajira zitapungua, mapato yatapungua. Kwa mtazamo wa mbali kwa mchezo huu serikali itakuwa inajichafua yenyewe.

Hii vita ya madawa ya kulevya isitumike kwa malengo ya kisiasa na chuki binafsi , bali haki za raia na utawala wa sheria vizingatiwe.
 
Kweli
List 2 za awali zimejaa wapinzani tu, wachache sana watu wa upande wa mtajaji, je ni ni coincidence au ndio dhamira kuu?
  1. Mwanasiasa mkuu wa chama pinzani!!!
  2. kiongozi wa dini mpinzani!!!
  3. Mmiliki wa radio pinzani!!
  4. Mwenyekiti wa timu pinzani!!
  5. Msanii wa kundi pinzani!!
Katika maisha ya kiintelijensia ni muhimu sana kuangalia patterns, sisemi kuwa list sio sahihi ila kuna pattern ya kuitazama!
Kweli wewe ni "yaliyomo yamo"
 
Mbowe ukimtazama Kama Kiongozi wa Upinzani Bungeni au Mbunge au Mwenykt wa Chadema ni ngumu kuamini Kama anashiriki Biashara ya dawa za kulevya.

Ukimtazama Mbowe Kama aliekuwa Mmiliki Night Club ya Bilicanas na ukajikumbusha yaliyokuwa yanaendelea ndani ya ile Club ( Kama uliwahi kwenda) hasa nyakati na Usiku huwezi kushangaa hata kidogo.
 
Popoma at his best using kijani eyes
 
Popoma at his best using kijani eyes

Usiamini Mwanasiasa kwa 100%

Jipe 50% kuamini na 50% kutoamini.

Mliwahi kuamini Slaa huwa Hali Rushwa

Mkaja kutuambia kala 3 Billion za CCM kumkataa Lowassa.

Mlituambia Lowassa ni Fisadi

Mkaja kutuambia Lowassa si Fisadi

Mimi simuwekei dhamana Mwanasiasa yeyote alie hai!
 
Back
Top Bottom