n00b
JF-Expert Member
- Apr 10, 2008
- 1,006
- 2,667
Wahusika wanajulikana. Wametajwa mara nyingi na mbinu wanazozifanya kwa kutumia wasanii wa kizazi kipya na waigizaji almaarufu kama 'Bongo Movie'.
Inaudhi, inakera na inatuongezea chuki sana kwa serikali iliyo madarakani. Kaeni kimya na endeleeni kulichafua taifa, kuna siku mtatueleza yote. Au kwakuwa wahusika ni wanenu? Au kwakuwa wakuu wa juu ni wale waliowawezesha kuingia madarakani kisiasa?
Ndugu zangu, hii ni aibu kubwa kwa Taifa. Inasikitisha sana na inazidi kutuaibisha wengine tunaosafiri ng'ambo. Taifa kama halina rais, taifa kama halina Vyombo vya Dola. Ni upumbavu, ni ufedhuli na mtambue sasa tumechoka. Sasa, tunaanza kuziweka habari za kila anayekamatwa na madawa hadharani, tunaanza kuweka hadi wanaowatuma. Tutawafikia mapapa wote!
Mambo haya mlimchomekea mtoto wa Mengi, mambo haya mnawachomekea wanyonge wenye njaa kali na hadi mmeua vijana wetu kwa kuwabebesha mizigo michafu hivi!
Kwa ambao hamjasoma habari hii ya aibu, someni hapa:
Wanawake wawili raia wa Tanzania wametambuliwa kuwa ndiyo wanaodaiwa kuingiza shehena ya dawa za kulevya zenye thamani ya zaidi ya Sh. bilioni 6.8 nchini Afrika Kusini wakitokea Tanzania.
Akizungumza na NIPASHE jana, Kamanda wa Polisi Kitengo cha Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya, Geofrey Nzoa, alisema haijafahamika wanawake hao wanatoka mikoa gani.
Kamanda Nzoa aliwataja wanawake hao kuwa ni Agnes Jerald ambaye alisema hajapiga hesabu ya umri wao, ila alizaliwa mwaka 1988 kwa maana hiyo ana umri wa miaka 25 na Melisa Edward ambaye alisema amezaliwa mwaka 1989 kwa maana hiyo atakuwa na umri wa miaka 24. Wawili hao bado wanaendelea kuhojiwa na polisi wa Afrika Kusini.
Alisema Jeshi la Polisi Nchini kwa upande wake linaendelea kufanya uchunguzi kubaini kama dawa hizo walitoka nazo wapi na pia linawasaka watu ambao watakuwa ndiyo wamiliki wa dawa hizo.
Someni zaidi hapa Watanzania Wawili wakamatwa South Africa na Madawa
USHAURI KWA VIJANA WA KITANZANIA:
Hakuna mtu asiyependa utajiri lakini utajiri unaweza kupatikana bila kufanya biashara haramu au kujihusisha na mambo ya kuhatarisha maisha yako. Kwa miaka ya karibuni kumekuwa na Watanzania wengi wanajihusisha na biashara ya madawa ya kulevya na wanaofaidika ni wachache tu wengi wao wanaishia kupata pesa ndogo na wanahatarisha maisha yao kwa kufugwa, kifungo cha kifo na hata madawa kupasuka tumboni na kuwaua. Kabla hujapata utajiri wa kudumu unatakiwa kupenda maendeleo kwanza na sio sifa pekee kwenye jamii. Fanya yafuatayo na polepole utafanikiwa.
1. Tafuta mtu ambaye unataka kuwa kama yeye: Usiangalie ukabila udini wala rangi ya mtu. Kama unataka kuwa kama Mengi, Mkono, Manji, Wanasiasa, wasomi au hata wasomi wa kimataifa wanaofanya kazi kwenye UN, World bank, diasporas. Tafuta mtu mmoja au wawili na waombe wawe kama walimu wako. Usiogope kutafuta utapata mtu na fuata wanayo kuambia hata kama wewe huoni umuhimu kwa sasa.
2. Jiendeleze kielimu: Hakuna mtu ambaye hawezi kufanya hili hata kama ni polepole. Elimu sio lazima iwe ya degree kwani duniani sasa kazi zinazolipa hazifundishwi kwenye degree bali certification mfano sasa tuna gas jifunze ufundi wa machine za kuchimba mafuta, project management, computer language, database kama SAP,Oracle, dot.net. Vilevile kuna Veta tafuta kitu ambacho kinauhusiano na Gas na Oil. Kwa ujumla jiwekee utamaduni wa kujiendeleza.
3. Marafiki: Tafuta marafiki ambao wanakusaidia kujiendeleza na wanakupenda badala ya wale wanaotaka kukutumia na wanao ku support kinafiki. Kama huna marafiki wazuri tafuta uhusiano wa kuomba kama mtanzania mwenzako omba urafiki kama Watanzania walivyokuwa wanafanya miaka ya zamani. Marafiki wabaya watakupeleka jela na kukuingiza kwenye ushabiki wa kimaisha na kukutumia.
4. Acha kulalamika: Kama unataka kuendelea uache utamaduni wa kulalamika badala yake jiulize je ni kitu gani naweza kufanya kufanikiwa bila kuiba. Tabia nzuri inaweza kukupeleka mbali kuliko unavyofikiri pesa pekee sio sababu ya kushidwa kuanza bali mara nyingi ni tabia. Ukiwa na tabia nzuri na kujihusisha na watu wazuri pesa haitakuwa kigezo.
5. Nenda ugaibuni kama umeshidwa yote: Kama yote umeshidwa na mazingira uliyo nayo si mazuri labda kabla ya kujihusisha na biashara haramu jitoe kwenye mazingira uliyopo. Kama bado ni kijana na mambo hayaendi yote hapo juu tafuta njia za kwenda nje lakini hayo mambo hapo juu inabidi uyafuate hata kama uko ugaibuni.
6. Uvumilivu: Hii nitakupa mfano wa ukweli kabisa. Watanzania wengi tulikuwa USA miaka ya 1996-2000 kutafuta maisha kwenda shule n.k. Watanzania wote tuliishi pamoja na mimi nilikuwa mojawapo pale Houston, TX tulifanya kazi pamoja umri ulikwa kama sawa tu kwa ufupi tulianza wote kwenye zero. Baaada ya miaka michache Watanzania wengine walihusisha na biashara, wengine shule, wengine mission town deals. Waliopiga deal walichukua pesa na kukimbia Tanzania na hawa walienda na magari, pesa na walipata wanawake, wanaume wanaowataka nyumbani. Wengi wao walienda bila kumaliza shule au kujifunza biashara.
Waliobaki makundi mawili wanaofanya kazi na kwenda shule na wanaofanya kazi lakini hawaendi shule. Wale walioenda Tanzania wengi wao wameishiwa na hawawezi kuja kwani ni wezi. Wengine walifungwa kabla hata ya kwenda Tanzania na walirudishwa bila kitu. Waliobaki ambao hawakwenda shule ndiyo sasa wanaanzan kwenda shule wakiwa na miaka 35 au zaidi. Walioenda shule hata kama kwa shida wanafanya vizuri sana na community imekuwa na watu wenye mafanikio kiuchumi kuliko community nyingi za Kitanzania duniani. Kuna Watanzania ambao ni VP wa kampuni kuna Watanzania wengi sasa wanatengeneza $50,000 mpaka $120,000 kwa mwaka kwenye mishahara. Hivyo maisha si kuiba tu unaweza kufanikiwa bila kuiba.
Alex Masawe ni tajiri mkubwa sana wa Kitanzania laikini kwasababu kapata utajiri wake kwa kuiba na hata kuua sasa kwenye miaka karibu sabini ndiyo anaenda jela badala ya kutumia pesa alizopata anaenda jela. Serikali inaweza kutaifisha mali zake hivyo uwizi wote huo aliofanya miaka yote ameishia wapi!!. Usisikilize watu wanaokuambia huwezi kufanya kwani si ukweli
*************************************
Habari zaidi ndani ya JF:
*************************************
- CHADEMA yatoa tamko baada ya Mbowe kutajwa katika listi ya Makonda
- Vita dhidi ya Dawa za Kulevya awamu ya Pili: RC Makonda awataja Mbowe, Manji, Gwajima, Idd Azzan...
- News Alert: - Rais Magufuli apigilia msumari jeneza la wauza Dawa za Kulevya, asema si kazi ya Makonda pekee
- Mbunge wa Kinondoni umefeli kupambana na Madawa ya kulevya!
- Tuseme: Makonda, Haya hapa Majina ya Wauzaji Madawa ya Kulevya wakubwa
- MADAWA YA KULEVYA: RC Makonda na Kamanda Sirro waongea na waandishi wa habari
- Updates: Wasanii Waitikia wito wa Makonda Kufika Polisi
- DAR: RC Makonda awataja Askari 9 watuhumiwa kushirikiana na mtandao wa Dawa za Kulevya. Wamo wasanii
- Hii ndio hali ya Nando (Mshiriki wa BBA) baada ya kuathirika na matumizi ya madawa ya kulevya
- Biashara ya Madawa ya Kulevya Tanzania: Who is Pulling the Strings? [September, 2010]
- Madawa ya Kulevya Tanzania, Serikali Yetu Hamyaoni Yanatumaliza? [March, 2011]
- Madawa ya kulevya: Rais Kikwete akutana na mawaziri, wakuu wa mahakama na polisi [2013]
- Kuficha watuhumiwa wa madawa ya kulevya... Wananchi, tufanye nini? [July, 2011]
- Madawa ya Kulevya - Aina na Athari zake kwa Mtumiaji [February, 2012]
- Dawa za kulevya: Watanzania watatu wakamatwa India, mmoja afariki
- Mafia wa Italia na mihadarati Tanzania [December, 2012]
- Mihadarati (Madawa ya Kulevya) yaivuruga CCM! [November, 2006]
- Wajumbe Baraza la Wawakilishi Zanzibar watuhumiana kuhusika na Mihadarati (Madawa ya Kulevya) [June, 2011]
- Serikali kuanika vigogo wa Madawa ya Kulevya bungeni [July, 2011]
- Madawa ya Kulevya: Alivyotoroshwa Nurdin Akasha...
- Mtanzania akamatwa na madawa ya kulevya Chicago, U.S.A.
- Mtanzania akutwa na madawa ya kulevya uwanja wa ndege wa Marekani-Texas tumboni kwake
- Rais Obama amtaja mfanyabiashara wa madawa ya kulevya mwanamke wa kitanzania aishie Mbezi
- Polisi wamnasa muuza dawa za kulevya wa kimataifa aitwaye Leila...
- Kikwete 'awapakazia' viongozi wa dini biashara ya madawa ya kulevya
- Pengo: Wananipakazia madawa ya kulevya!
- Dadake mbunge Munde Tambwe (CCM) akamatwa na dawa za kulevya!
- Kangi Lugola, mbunge CCM atuhumu Mawaziri ni wauza mihadarati! Serikali yawatetea, awekwa kitanzini!
- Mtandao wa uhalifu Polisi... Wahusishwa na mauaji, biashara ya mihadarati na ulaji rushwa!
- Mfanyabiashara jamaa ya Mbunge akamatwa na Shehena ya Madawa ya Kulevya
- Mtangazaji wa redio kutoka Tanzania amekamatwa na dawa za kulevya Kenya!
- Mtoto wa Liyumba akamatwa na madawa ya kulevya yenye thamani ya Bil 9 Tsh
- Wapakistan waliokamatwa na madawa ya kulevya ya billion 6 waachiwa kwa dhamana!
- Picha: Msichana wa KITANZANIA aliyekamatwa na Unga EGYPT kunyongwa...
- Madawa ya Kulevya: Mabondia wa Tanzania wafungwa miaka 15 nchini Mauritius!
- Watanzania Wawili wakamatwa South Africa na Madawa
- Watanzania wawili wakamatwa na madawa ya kulevya Hong Kong
- Binti ashikwa na Madawa ya Kulevya JNIA; Polisi wa usalama waomba Rushwa wakataliwa...
- Mtanzania afungwa jela miaka 15 Zimbabwe kwa kukutwa na madawa ya kulevya
- Wafungwa wa Kitanzania waliokamatwa na madawa ya kulevya Hong Kong wafunguka!
- Kilumbe Ng'enda: Mbunge Azzan Anahusika na Biashara ya Dawa za Kulevya
- Mtanzania akamatwa na madawa ya kulevya US
- Mapapa wa madawa ya kulevya watajwa, wamo Morine Amatus Liyumba na mdogo wa Rostam Aziz
- Kumekucha Madawa ya Kulevya: Kina 'Masogange' wawataja waliowatuma!
- Mtambo wa Dawa za kulevya waingizwa nchini, upo Mbezi Beach!
- Serikali sasa kuanzisha mahakama ya madawa ya kulevya...!!
- Madawa ya Kulevya: Mashine mpya zafungwa JKIA
- Bungeni Live: Hoja juu ya Madawa ya Kulevya
- CHADEMA watoa tamko kuhusu madawa ya kulevya
- Vita dhidi ya madawa ya kulevya: Waziri akiri wauza unga kuifadhili CCM, Nzowa aizamisha Jambo leo
- Sakata la madawa ya kulevya: Kamanda wa polisi viwanja vya ndege ahamishwa
- Sakata la madawa ya kulevya: Viongozi wachunguzwa na kuhojiwa
- Majina ya Majaji wanaolinda wauza madawa ya kulevya yatajwa! Wamo Pendo Msuya na Dr Fauz Twalib
- Mtanzania adakwa na mihadarati China
- Mtanzania akamatwa akiwa na Madawa ya Kulevya United Arab Emirates (UAE)
- Mshambuliaji wa zamani wa Simba akamatwa na madawa ya kulevya...
- Mbwana Matumla akamatwa na madawa ya kulevya Spain
- Madawa ya Kulevya: Matumla na Kaniki wakamatwa!
- Mtanzania aliyekamatwa na madawa ya kulevya Dubai amlaumu mumewe
- Madawa ya Kulevya: Meli ya Tanzania iliyobeba unga wa Sh. Bilioni 123 yazua kizaazaa nchini Italia!
- Ripoti UN: Tanzania kinara dawa za kulevya
- Uchochoro wa kuvusha dawa za kulevya Dar huu hapa
- Baadhi ya njia zinazotumika kupitisha madawa ya kulevya uwanja wa ndege JKNIA
- Madawa ya kulevya: Mtanzania afia Dubai, wengine wadaiwa kukamatwa China na Brazil
- Madawa ya Kulevya: Aisha Bui (mke mwenza na Amina chifupa) naye akamatwa Brazil
- Mwanajeshi Rashid Mohamed akamatwa na mirungi kilo 20 huko Tanga