Madawa ya Kulevya: Mashine mpya zafungwa JKIA

Madawa ya Kulevya: Mashine mpya zafungwa JKIA

Maswala

JF-Expert Member
Joined
Feb 28, 2011
Posts
560
Reaction score
226
Serikali imefunga mashine mpya na za kisasa zenye uwezo wa kubaini aina yoyote ya dawa za kulevya na nyara za serikali kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar-es-salaam, lengo likiwa ni kudhibiti uingizwaji na upitishwaji wa mizigo uwanjani hapo, ambapo kuanzia sasa mizigo yote inayoingia na kutoka itakaguliwa.

Waziri wa uchukuzi Mheshimiwa Dk Harison Mwakyembe ameyasema hayo jijini Dar-es-Salaam,mara baada ya kutembelea uwanja huo kwa mara ya pili ili kuona zoezi la ufungwaji wa mashine za kisasa zenye uwezo kutambua dawa za kulevya na nyala nyingine za serikali.

Meneja wa usala wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Bwana Clence Jingu, amesema kuwa kufungwa kwa mashine hiyo ambayo itakuwa ikijiongoza yenyewe kwa kukagua mizigo ya abiria wanaoingia na wanaosafiri tofauti za zamani ambapo mizigo iliyokuwa ikiingia ilikuwa haikaguliwi.

Awali akiwa uwanjani hapo waziri Mwakyembe amewaagiza wasimamizi wa uwanja huo,kuhakikisha kuwa ombaomba wote wanaozagaa uwanjani hapo wanaondolewa mara moja,kwani uwanja huo ndiyo kioo na sura ya Tanzania ambapo ITV ilishuhudia baadhi ya abiria wakipita na kuwapatia ombaomba hao kitu chochote.

Katika tukio lingine waziri Mwakyembe alizuru ghafla kwenye mizani iliyopo maili moja Kibaha mkoani Pwani, mara baada ya kupigiwa simu na mawaziri wa ulinzi na wa uchukuzi wa Zambia, wakidai kuwa raia wao wamezuiliwa kuondoka kwa mabasi yao manne yaliyopitia bandari ya Dar-es-Salaam kwa madai kuwa yamezidi viwango vya urefu kwa barabara za Tanzania ambapo walitakiwa kulipa faini ya dola za marekani ishirini elfu kwa kila basi moja.


Chanzo: ITV

My Take:

Nadhani mashine ni hatua mojawapo, lakini la muhimu ni nia ya dhati ya vyombo yetu vyote vya dola na umma kwa ujumla wake kushirikiana kupiga vita uovu huu.

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Tatizo sio vifaa tatizo ni hao walipewa nafasi za kuendesha na kusimamia hvy vifaa.

Nakubaliana nawe wewe. Tunahitaji mabadiliko ya kimfumo katika utendaji.

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Mitambo haiwezi kusaidia kwa sababu dhamira haipo.

Watuhumiwa wa ufanyaji biashara ya madawa ya kulevya ndiyo wafadhili wakubwa wa CCM wakati wa uchaguzi. je watakamatwa na serikali ambayo wameiweka madarakani? Mitambo hiyo ni kupoteza hela ya walipa kodi.
 
Wengine wanaweza beba hadi kwenye ule msafara wa Rais

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
wanahitaji mashine kuona gunia moja na nusu la unga mimi naona wangenunuliwa miwani kwanza kabla ya mashine.
 
Hata kama wangefunga mitambo kiasi gani bila kufuata maadili ya utumishi wa umma ni kazi bure. Hiyo mitambo inafungwa na watu na inaendeshwa na watu na wabeba "unga" ni watu. Kwa hiyo sioni kama hilo ni suluhisho. Hizo "mechi" zinachezwa nje ya ule uwanja wa ndege na mshindi anakuwa keshapatikana kwa hiyo wanaoenda pale na "unga" ni kukamilisha ratiba tu ya ligi.
 
Mashine hizo zinaongozwa na watu, so watu wasipobadili mtazamo then tegemea madawa zaidi kuendelea kupita bila shida tu!!!!!
 
Viongozi zaifu. Kazi yao kubambikia kesi CHADEMA!
 
Kwani sembe lote lililokuwa linapita unadhani walikuwa hawalioni! Mashine sio suluhu bali nikujikosha tu. Na sembe litaendelea kupita.
 
huo ni mpango wa kitoto. maana huo mpango mzima unahitaji kitu kiitwacho, humanware( mtu mtendaj) ili huo mtambo uweze kufanya kazi.i sasa huyo humanware ndio kapewa ulaji wa kutisha kwa kusuka mipango na wabebaji. Kumbuka vita vya madawa ya kulevya havishindiki hata kwa kuwauwa wabebaji bali kwa kuziodisha soko la ajira kwa watu na kuweka adhabu ya kifo kwa wafadhili wa madawa ya kulevya. hapo utapunguza kasi ya hii biashara. hawa watu wafanyao biashara hii haramu, huwa na pesa nyingi sana majumbani mwao interms of buillions. sasa kupambana nao ni vigumu sana kwa sababu huwamiliki majina makubwa.
 
Tatizo la dawa za kulevya sio mashine ni watu. Hata zikifungwa sophisticated machine za ajabu kama wafanyakazi sio waaminifu ni kazi bure. Serikali iwachunguze tu wafanyakazi wake wala isiingie katika hasara kubwa ya kununua mitambo ya ajabu.

Suala hapa ni uaminifu na ethics zaidi. Hao wazungu wanataka tu tuwe soko ndiyo maana wanakuja na matoleo mapya ya vifaa kila wakati!
 
Tatizo Tanzania ni uwajibikaji na si mashine....Mtakuja kushangaa watakamatwa watanzania wengine majuu waliosafiri kutokea JKNIA, subirini tu. Mashine zipo iweje watu wanasafiri kutoka Dar kwenda majuu wakamatwe? Yetu macho tu.
 
mashine mpya,
wafanyaazi wa zamani,
hakuna kipya cha kutegemea!
 
Back
Top Bottom