Madawa ya Kulevya: Mashine mpya zafungwa JKIA

Madawa ya Kulevya: Mashine mpya zafungwa JKIA


Katika tukio lingine waziri Mwakyembe alizuru ghafla kwenye mizani iliyopo maili moja Kibaha mkoani Pwani, mara baada ya kupigiwa simu na mawaziri wa ulinzi na wa uchukuzi wa Zambia, wakidai kuwa raia wao wamezuiliwa kuondoka kwa mabasi yao manne yaliyopitia bandari ya Dar-es-Salaam kwa madai kuwa yamezidi viwango vya urefu kwa barabara za Tanzania ambapo walitakiwa kulipa faini ya dola za marekani ishirini elfu kwa kila basi moja.

Hivi haya si yanapita tu? yana aribu vipi barabara? kama ingekuwa ni kuzidi uzito sawa lakini Urefu?
kwani yanatumika TZ?
kwanini tuyazuie na kupiga fine? tena 20,000 Usd Duh!
Mtu si anaweza akasusa magari yenyewe mizani akakimbia.
 
Kama mbwa wa kunusa dawa za kulevya hawakupelekwa uwanjani siku tani nyingi za sembe zimepitishwa hapo,kwanini wasitengeneze mgao wa umeme kuvuruga hizo mashine!
 
Ikiwa waendesha vifaa tajwa hawana viwango (drug dealers) jee kuna kifaa kitawangika..?
 
Hivi haya si yanapita tu? yana aribu vipi barabara? kama ingekuwa ni kuzidi uzito sawa lakini Urefu?
kwani yanatumika TZ?
kwanini tuyazuie na kupiga fine? tena 20,000 Usd Duh!
Mtu si anaweza akasusa magari yenyewe mizani akakimbia.

That is very true! An attitude of change is needed urgently.

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Maadili ndio nguzo yetu
"Ex Tanzania Simper aliquid"
 
mara ya kwanza tatizo lilikua ukosemu wa vitendea kaz? Hata kama tutanunua vifaa vya gharama kubwa kama wasimamizi hawana uaminifu basi ni kazi bure
 
usishangae hivyo vifaa vimetolewa na wauza unga.
umeliongelea vizuri zaidi ya yeyote mkuu zumbemkuu. Jibu sio mashine wala robot bali ni kubadilisha mfumo na mfumo ni utawala ambao ni ccm, mbali na hapo ni dhiaka tu kwa maana hizo facilities zilizokuwepo kabla na ukuu wake zinaweza kunasa madawa kama waoperators wake wakiamua!
 
Serikali imefunga mashine mpya na za kisasa zenye uwezo wa kubaini aina yoyote ya dawa za kulevya na nyara za serikali kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar-es-salaam, lengo likiwa ni kudhibiti uingizwaji na upitishwaji wa mizigo uwanjani hapo, ambapo kuanzia sasa mizigo yote inayoingia na kutoka itakaguliwa.

Waziri wa uchukuzi Mheshimiwa Dk Harison Mwakyembe ameyasema hayo jijini Dar-es-Salaam,mara baada ya kutembelea uwanja huo kwa mara ya pili ili kuona zoezi la ufungwaji wa mashine za kisasa zenye uwezo kutambua dawa za kulevya na nyala nyingine za serikali.

Meneja wa usala wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Bwana Clence Jingu, amesema kuwa kufungwa kwa mashine hiyo ambayo itakuwa ikijiongoza yenyewe kwa kukagua mizigo ya abiria wanaoingia na wanaosafiri tofauti za zamani ambapo mizigo iliyokuwa ikiingia ilikuwa haikaguliwi.

Awali akiwa uwanjani hapo waziri Mwakyembe amewaagiza wasimamizi wa uwanja huo,kuhakikisha kuwa ombaomba wote wanaozagaa uwanjani hapo wanaondolewa mara moja,kwani uwanja huo ndiyo kioo na sura ya Tanzania ambapo ITV ilishuhudia baadhi ya abiria wakipita na kuwapatia ombaomba hao kitu chochote.

Katika tukio lingine waziri Mwakyembe alizuru ghafla kwenye mizani iliyopo maili moja Kibaha mkoani Pwani, mara baada ya kupigiwa simu na mawaziri wa ulinzi na wa uchukuzi wa Zambia, wakidai kuwa raia wao wamezuiliwa kuondoka kwa mabasi yao manne yaliyopitia bandari ya Dar-es-Salaam kwa madai kuwa yamezidi viwango vya urefu kwa barabara za Tanzania ambapo walitakiwa kulipa faini ya dola za marekani ishirini elfu kwa kila basi moja.


Chanzo: ITV

My Take:

Nadhani mashine ni hatua mojawapo, lakini la muhimu ni nia ya dhati ya vyombo yetu vyote vya dola na umma kwa ujumla wake kushirikiana kupiga vita uovu huu.

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums

Rekebisha kichwa cha habari - badala ya JKIA ni JNIA!
 
Kufuatana na maelezo yaliyotolewa baada ya kuangalia CCVT jinsi akina Masogange walivyopitisha madawa ya kulevya pale airport, hata ikiwekwa mitambo ya aina gani ni kazi bure. Tatizo lipo kwa watu wanaohusika. Kuna mtandao mkubwa inabidi upigwe vita na kuangamizwa. Mwakyembe kama kawaida yake anajaribu lakini mwisho wa siku atagundua kuwa hiyo ni ngoma nzito kuliko alivyotarajia. Labda mwaka 2015 akija Rais mwingine - awe CCM au CDM haijalishi lakini awe na nia ya dhati ya kupambana na kadhia hii. Kuwa na orodha mfukoni haitusaidii.
 
Nilishasema kuweka vifaa vipya nimuhimu .je nawatendaji ni wapya .serikali iondoe watendaji wote hasa maaskari .airport ifanyiwe reshuffle. Waziri wa mambo ya ndani na ulinzi na naibu wake wapigwe chini hakuna kazi wanayofanya.pia watendaji wote kwenye kitengo cha usalama pale airport waondolewe haraka iwezekanavyo pia itolete amri mara moja yoyote ataekutwa anasafirisha .nikuchinja tu kama china .akipelekwa mahakamani ni kifo tu .labda itapunguza hizi biashara
 
Na ile chopa ya makamanda nayo iwe inakaguliwa maana ile mizigo inayozunguka nayo nchi nzima haieleweki..
 
Back
Top Bottom