madalali wa nyumba dsm

madalali wa nyumba dsm

KayandaPM

Member
Joined
Mar 26, 2011
Posts
46
Reaction score
26
Wana jamvi naomba kuleta hoja hapa ili mwisho wa siku niwaelewe hawa watu nijue jinsi ya kushughulika nao
Julai mwaka jana nilimtuma mwenzangu kulipia kodi ya nyumba miezi sita, akafatiliwa na vibaka wakakwapua mkoba wenye hela na simu na vitambulisho mpaka vile vya benki. Wakakimbia lakini kule mbele baada ya kuchukua hela vitu vingine walivitupa. Nilipo kaa na kutafakari nikagundua palikuwa na mahusiano kati ya kibaka na dalali.
Mwezi wa nane mwaka huu ndugu tupo ofisi moja alipelekwa na dalali kulipia kodi ya nyumba, akalipa akapata dharula akasafiri amerudi akakuta dalali karudi kwa mwenye nyumba akachukua ile hela eti jamaa kaahirisha hatakuja tena. Wamepelekana polisi".halipaswi kujadiliwa lipo polisi"

Wiki mbili zilizopita mwingine tena tupo ofisi moja kapelekwa kwenye nyumba sijui ndiyo mikocheni sijui masaki lakini kalipia mwaka mmoja jana anakwenda kuhamia eti katapeliwa " mshike mshike ikaanza " wamepelekana polisi. Sasa wanajamvi nisaidieni hawa watu wakoje!
 
Kuna dalali mmoja sinza aliachiwa nyumba na mama mwenye nyumba ashughulikie kila kitu as yule mama yupo mkoan, sasa yule dalal alichofanya nyumba moja akawapangisha watu watatu tofauti, as kabla aliyelipia hajaamia akapokea na hela za wengine.. Halafu alivyokuwa mwehu wote akawapa mikataba na yeye kasaini kama agent wa mwenye nyumba.. Balaa likaja kwenye kuhamia kila mtu ana mkataba wa halal, na dalal kaingia mitini na kama million 10 hivi, as mama mwenye nyumba alimuingizia hela za mtu mmoja tu.. Na haijulikan zile hela ni za mpangaj gan alizopokea... Mpaka leo dalal hajaonekana
 
Huu ni ugonjwa mwingine wa moyo inapofika wakati wa kutafuta nyumba inabidi kuwa makini sana maana unaweza kuingizwa mjini. Nakumbuka mwaka huu jioni moja nilikuta vifaa vya ndani ya nyumba vikiwa vimerundikana nje ya nyumba ninayoishi na nikawakuta wakina mama watatu, kilichonisikitisha zaidi ni kuwa kati ya wale kina mama mmoja alikuwa mjamzito na mwingine alikuwa mtu mzima sana wa karibu miaka 75, nilipowauliza kulikoni waniambia kuwa wamepanga hiyo nyumba, nikawafahamisha kuwa mimi ndiye ninaishi na wakati huo nilikuwa na mwezi mmoja tu. Hivyo ilibidi watafute lori wabebe mizigo yao. Lakini yote hayo yanasababishwa na nchi yenyewe maana hii biashsra ni huria mno na hakuna anaye regulate, ni hovyohovyo kwa kwenda mbele.
 
du kweli kali hawa watu ni kuwa nao makini mie mwaka 2004 nilifanikiwa kumtapeli dalali mpaka leo akiniona anacheka sana
 
du kweli kali hawa watu ni kuwa nao makini mie mwaka 2004 nilifanikiwa kumtapeli dalali mpaka leo akiniona anacheka sana

mkuu .... hebu funguka zaidi kuhusu jilo
 
Wengi wao ni matapeli, na mfumo huu wa kitapeli umelelewa na kukuzwa na serikali hi hii...kama sio udhaifu wa serikali ina maana mwenye nyumba angekua anatangaza mwenyewe nauza nyumba bei sh kadhaa...au napangisha sasa nchi hii nyumba zinafanywa kuwa siri na hapo dalali anapata mwanya wa kutapeli...
 
Well said!
Wengi wao ni matapeli, na mfumo huu wa kitapeli umelelewa na kukuzwa na serikali hi hii...kama sio udhaifu wa serikali ina maana mwenye nyumba angekua anatangaza mwenyewe nauza nyumba bei sh kadhaa...au napangisha sasa nchi hii nyumba zinafanywa kuwa siri na hapo dalali anapata mwanya wa kutapeli...
 
du kweli kali hawa watu ni kuwa nao makini mie mwaka 2004 nilifanikiwa kumtapeli dalali mpaka leo akiniona anacheka sana
Ulimtapeli au alikutapeli.
Kama ulimtapeli ni vema utuelezee namna ulivyomwingiza mjini maana hawa huwa wanatapeli sio kutapeliwa.
 
du kweli kali hawa watu ni kuwa nao makini mie mwaka 2004 nilifanikiwa kumtapeli dalali mpaka leo akiniona anacheka sana

ahahahaaaaaaasaaaaaa....hii ni nzuri
 
Chunga sana Ogopa dalali wa Sinza na Kinondoni . Hasa Juma Mhaya.
 
Chunga sana Ogopa dalali wa Sinza na Kinondoni . Hasa Juma Mhaya.

Juma mhaya balaa, mpaka kenyela anamjua. Last year alimtapeli maza wangu mdogo. Yule maza kufika Oysterbay akaambiwa aende chini ya mti mmoja hivi kuna wenzake kama 6 hivi wenye same problem against Juma mhaya, jamaa ni soo!
 
Kuna dalali mmoja sinza aliachiwa nyumba na mama mwenye nyumba ashughulikie kila kitu as yule mama yupo mkoan, sasa yule dalal alichofanya nyumba moja akawapangisha watu watatu tofauti, as kabla aliyelipia hajaamia akapokea na hela za wengine.. Halafu alivyokuwa mwehu wote akawapa mikataba na yeye kasaini kama agent wa mwenye nyumba.. Balaa likaja kwenye kuhamia kila mtu ana mkataba wa halal, na dalal kaingia mitini na kama million 10 hivi, as mama mwenye nyumba alimuingizia hela za mtu mmoja tu.. Na haijulikan zile hela ni za mpangaj gan alizopokea... Mpaka leo dalal hajaonekana

As huyo dalali atakua mbumbumbu, As hela alokimbia nayo ni kiduchu mno
 
Wengi wao ni matapeli, na mfumo huu wa kitapeli umelelewa na kukuzwa na serikali hi hii...kama sio udhaifu wa serikali ina maana mwenye nyumba angekua anatangaza mwenyewe nauza nyumba bei sh kadhaa...au napangisha sasa nchi hii nyumba zinafanywa kuwa siri na hapo dalali anapata mwanya wa kutapeli...

yaani we na ujinga wako uibiwe halafu uilaumu serikali.ulitaka rais afanyeje kuhusu uzembe wako
 
Anacho sema Somoche ni kuhitajika kwa mfumo rasmi ambao unatakiwa uwe umewekwa na serikali iliyopo madarakani, yaani kama si nyerere basi ,mwinyi, mpaka na kikwete.
yaani we na ujinga wako uibiwe halafu uilaumu serikali.ulitaka rais afanyeje kuhusu uzembe wako
 
yaani we na ujinga wako uibiwe halafu uilaumu serikali.ulitaka rais afanyeje kuhusu uzembe wako

Badala ya kukujibu nakujulisha hapa ni JF sio FACEBOOK....Hapa tunajibu hoja kwa hoja na kama hujui maana ya serikali na majukumu yake ni nini subiri matokeo yako ya fm 4 yakitoka uniulize ntakujibu...
 
Ulimtapeli au alikutapeli.
Kama ulimtapeli ni vema utuelezee namna ulivyomwingiza mjini maana hawa huwa wanatapeli sio kutapeliwa.
nilimtapeli huyu bwana anaitwa j4 kule kigamboni acha tu huwa akiniona hoi
 
mimi nakumbuka 2010 kuna kademu kalinisumbua sana eti nikapangishie chumba sinza eti kana mimba yangu basi kanakuwa kakali kweli. Kenyewe kalijifanya kamepima na vyeti kuonyesha kana mimba kume kamecheza mchezo.
Basi ikabidi nikape pesa ya chumba cha 50,000 kwa mwezi ili kalipie miezi sita kwanza si kakatapeliwa na jamaa aliyejifanya mwenye nyumba.
Basi kalirudi kamefura kakaanza safari za kumtafuta huyo jamaa ndipo kalienda kumripoti polisi kijitonyama wakamwambia kuwa yule ndio zake basi kalichoka
Ilibidi kaseme ukweli nilikatandika makofi pale pale polisi
 
Back
Top Bottom