Madaktari watinga ikulu

Lakini Kikwete unaogopa nini kufukuza mawaziri, hata Mseveni anakushinda hilo! kwake wakiomba kujiuzuru tu anawasindikiza haraka sana
 
Aliyewaambia kuwa bila Ulimboka mgomo hauwezekani ni nani? Hebu muacheni kijana wa watu atulie huko aliko. Mnahangaika naye bure wakati hata hapa nchini hayupo na wala hajui kinachoendelea safari hii.
unamfahamu kamanda ulimboka?
umeangalia picha zilizotolewa hapo juu?
 
Na wamweleze inakuwaje dawa zinazotumika theater na Psychiatry clinic zinatumika Guest au Hotelini?
 
Jamani hawa madokta wajihadhari na juice za ikulu kwani ni soo na ni kiboko cha wanaharakati wote, kama mnabisha muulizeni Zitto kabwe atawaambia.
 
Safi sana Rais JK. Ikulu ni ya Watanzania wote itumie kutatua matatizo ya raia wako. Kwisha habari; nasubiri taarifa ya habari ya saa mbili kamili kupitia TBC1 ikiwa na habari ya kwanza kabisa kwamba madaktari wamkubali kuacha mgomo bila masharti yoyote baada ya kuwa wamekutana na Rais ikulu ya Dar es Salaam. Nilikuwa nataka kushangaa, kama JK aliweza kusaidia katika utatuzi wa mgogoro wa Kibaki na Raila na pia kumaliza gogoto la Zanzibar iweje ashindwe na kagogoro haka kadogo! Miaka kumi akiwaongoza mabalozi imempa uzoefu wa kutosha wa kidiplomasia. Hapa inatumika diplomasia tu.

Muongo. Jk ni muasisi wa old talk show. Sasa alitaka kurudia tena kale kamchezo kake ka kumtaja kaimu katibu wa tukta, kumbe hawa ni madaktari, na ishu hazifanani. Sasa wenye akili wakamwambia aache upumbavu. %90 si busara zake zinazotumika hapo kwani akili yake yote kaiacha angani. Tuombe tu awe na busara ya kuwakubalia hao mawaziri kujiuzulu. Na sio udhaifu bali ni busara
 
jamani mbona update haziji tena na huku kwetu Ngeleja kwa hasira ya kijana wake kuibiwa na chata ameamua kuchukua umeme wake hata taarifa ya habari ndo inanipita soon
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Jamani hivi hata techniques kidogo za majadiliano hatuna au hatuzijui? Mtu akikuita uende kujadiliana naye nyumbani kwake wewe hesabu umeumia. Amekalia kiti chake cha enzi na wewe ndio mara ya kwanza unaingia kwake tena IKULU. Haya yetu macho. Lakini yote heri tunachokata mgomo uishe watu wapate huduma za matibabu.

trend inaonyesha kuwa dhana yako si sahihi. Pale wameenda watu wengi sana kuongea na jk na hatimaye wakatoka washindi. Wa awali ni wawekezaji. Karibuni hapa cdm wameenda pale na wakatoka na ushindi. Hukusikia tetesi jk angevunja bunge kama wasingekubaliana na hoja yake (hoja ya cdm)? Na madaktari wataibuka kidedea tu
 
I guess kesho habari kuu kwenye media ni madaktari wasitisha mgomo na kurudi kazini,. anayebisha tu bet!!
 
Moderators mko wapi?
Mbona hii thread imejaa matusi tupu au ndo jadi mpya hapa JF?
 
Kimbunga siku nzima ya leo ulikuwa unaenda vyema,sijui shetani kadi maskini kakuingilia muda huu,hivi na wewe unaamini kuwa JK ndiye aliyewapatanisha Kibaki na Odinga? umekuja kama kimbunga na pumba za kutosha.

Umenifurahisha sana Madiba! Nimekuwa makini kweli: Nimeandika aliweza kusaidia...... wewe hutaki? Wakati huo akiwa Mwenyekiti wa AU!! Mengine ya Zanzibar umekubali au? Na ikulu kutumika kama fimbo vipi? Hutakaa unielewe. Kila anayenda ikulu anapoa mkuu. Ikulu inatisha; ukiangalia kando kuna bendera ya nchi mara bendera ya rais mara coat of arms, Rais anaegemea vimito vyenye coat of arms hapo bado hujapata gahawa na harubati! Unajua sharubati wewe?
 
acha ujinga wewe,inaonekana una ushabiki wa kishamba kweli.hakuna mtu aliempigia mwenzake magoti,wameomba kukutana na rais amewakubalia,sasa we unakuja kuanza kuropoka apa bana

kichaa cha mbwa ni lazima kipate tiba ya daktari (wako kwenye mgomo sijui utapona lini)
 
trend inaonyesha kuwa dhana yako si sahihi. Pale wameenda watu wengi sana kuongea na jk na hatimaye wakatoka washindi. Wa awali ni wawekezaji. Karibuni hapa cdm wameenda pale na wakatoka na ushindi. Hukusikia tetesi jk angevunja bunge kama wasingekubaliana na hoja yake (hoja ya cdm)? Na madaktari wataibuka kidedea tu


Sawa mkuu lakini Ikulu inatisha! Katika majadiliano si busara kwenda kupata ushindi bali wote muwe washindi huo ndio murua wa mazungumzo. Pamoja na hayo mgomo ukiisha washindi watakuwa ni watanzania wote nikiwemo mimi na wewe.
 
Back
Top Bottom