Madaktari watakiwa kusimamia maamuzi ya 3/3/2012; - Uongozi wa Mgomo wa Madaktari

meningitis

JF-Expert Member
Nov 17, 2010
8,349
4,674
TAARIFA YA TATHMINI YA MGOGORO WA MADAKTARI TOKA TAREHE 03.03.2012
Uongoziunapenda kutoa taarifa kwa madaktari wote nchi nzima kuwa hali ya ushirikiano na umoja miongoni mwetu imeendelea kuimarika sana, hospitali mbalimbali zimeendelea kushiriki katika kushinikiza madai yetu kutekelezwa ili madaktari waweze kutoa huduma za afya.
Ni muhimu ikafahamika kuwa mpaka sasa Serikali haijatoa jibu la msing...i juu ya utekelezaji wa hatua muhimu ya kuendelea na mazungumzo, na hilo ni juu ya Kuwajibika kwa Waziri na Naibu Wazari wa Afya na Ustawi wa Jamii kwa lengo la kupisha meza ya mazungumzo.
Pia tumepata taarifa kupitia vyanzo visivyo rasmi juu ya Mhe, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kukutana na kuzungumza na Wazee wa Dar es Salaam, hivyo basi tuna imani Mhe, Rais atatumia hekima na busara katika kumaliza mgogoro huu ambao umedumu kwa muda mrefu sasa.
Mwisho, tunapenda kutoa rai kwa madaktari wote kuendelea kusimamia maamuzi tuliyokubaliana tarehe tatu, kwa mabadiliko yoyote tutafanya sote kwenye kikao itakapobidi.

Imetolewa uongozi.
08.03.2012
 
Mkuu unaweza kutuambia hivi Waziri na Naibu Wazari wa Afya na Ustawi wa Jamii wanazuia vipi meza ya mazungumzo. Je kwa yale majibu waliyowapa ambayo hamkuyapenda, ndio msimamo wa serikali toka juu kwa nini wawajibike wao ilihali serikali imewaagiza wafanye walivyofanya?.. Kwa nini wasiwepo mezani kujibu hoja zenu ikiwa litazungumzwa ama kuongezwa neno tofauti na walivyofanya ama walivyoelekezwa!. Siku zote mazungumzoa yanahitaji pande mbili husika hata maswala ya Iraq huyo Assad hushiriki iweje swala hili liwe la madaktari na waziri mkuu tu au mnashindwa kusema mbele yao.
 
Mkuu unaweza kutuambia hivi Waziri na Naibu Wazari wa Afya na Ustawi wa Jamii wanazuia vipi meza ya mazungumzo. Je kwa yale majibu waliyowapa ambayo hamkuyapenda, ndio msimamo wa serikali toka juu kwa nini wawajibike wao ilihali serikali imewaagiza wafanye walivyofanya?.. Kwa nini wasiwepo mezani kujibu hoja zenu ikiwa litazungumzwa ama kuongezwa neno ttofauti na walivyofanya ama walivyoelekezwa!..

Mkuu,
Waziri na Naibu Waziri wa Afya wamezuia meza ya Mazungumzo kwa kitendo cha Waziri Mponda mwenyewe kutamka maneno haya kutoka kinywani mwake. Nanukuu:
Mimi nawajibika kwa Wakulima na Wafugaji wa Jimbo la Ulanga wa Magharibi. Madaktari hawanihusu.

Nchi iko kwenye auto pilot, hata Zembwela anaweza kuwa rais na waziri mkuu akawa Joti....
 
Hahaha kweli,msikilize zembwela kwenye kipindi chake east africa radio!Nimuambata waupande fulani.Leo aliwaalika madoc asubuhi wakaongeza namtangazaji mwingine anaitwa Big nini sijui maana waliona yeye na Baruti haitoshi!Inaonyesha kunamaswali waliandaliwa wakayasahu jamaa akaja nayo!Lakini wapi!
 
hivi kuna ugumu gani kwa waziri na naibu waziri kuachia ngazi kupisha mazungumzo ya amani na kutatua tatizo tunajua hatuna raisi ambaye anaelewa yupo yupo kwanini asiachie ngazi tufanye uchaguzi wa akili uongozi ni kazi kubwa sana
 
Hongera sana madaktari, mnayojenga ni signal kubwa kwa utawala tulionao, serikali ijue kuwa wafanyakazi na wananchi kwa ujumla si walewale wa zamani wa ndio mzee, na hii inapeleka ujumbe wa moja kwa moja kwa watawala wa secta zingine kuanza kuheshimu wafanyakazi wa chini yao.
 
Mkuu unaweza kutuambia hivi Waziri na Naibu Wazari wa Afya na Ustawi wa Jamii wanazuia vipi meza ya mazungumzo. Je kwa yale majibu waliyowapa ambayo hamkuyapenda, ndio msimamo wa serikali toka juu kwa nini wawajibike wao ilihali serikali imewaagiza wafanye walivyofanya?.. Kwa nini wasiwepo mezani kujibu hoja zenu ikiwa litazungumzwa ama kuongezwa neno tofauti na walivyofanya ama walivyoelekezwa!. Siku zote mazungumzoa yanahitaji pande mbili husika hata maswala ya Iraq huyo Assad hushiriki iweje swala hili liwe la madaktari na waziri mkuu tu au mnashindwa kusema mbele yao.
mkuu mazungumzo yatakua na maana gani iwapo mtekelezaji wa makubaliano ndiye aliyesababisha mgomo na alishindwa kutatua au kuepusha?
 
hivi kuna ugumu gani kwa waziri na naibu waziri kuachia ngazi kupisha mazungumzo ya amani na kutatua tatizo tunajua hatuna raisi ambaye anaelewa yupo yupo kwanini asiachie ngazi tufanye uchaguzi wa akili uongozi ni kazi kubwa sana

kuna mwananchi ameuliza kuna hasara gani mawaziri hawa wakijiuzulu?
kuna hasara gani madaktari wakigoma kurudi kazini?
 
Mkuu,
Waziri na Naibu Waziri wa Afya wamezuia meza ya Mazungumzo kwa kitendo cha Waziri Mponda mwenyewe kutamka maneno haya kutoka kinywani mwake. Nanukuu:

hata ukikubaliana na serikali usiku huu unadhani mtu mwenye hulka ya namna hii atafacilitate utekelezaji wa yale mliyokubaliana??
 
Hongera sana madaktari, mnayojenga ni signal kubwa kwa utawala tulionao, serikali ijue kuwa wafanyakazi na wananchi kwa ujumla si walewale wa zamani wa ndio mzee, na hii inapeleka ujumbe wa moja kwa moja kwa watawala wa secta zingine kuanza kuheshimu wafanyakazi wa chini yao.

Yani baada ya huu Mziki nadhani fani zote zitaamka kuanzia Manesi, Waalimu, Wahasibu, Wakaguzi, Wahandisi, Maafisa Tawala na Utumishi, Wachumi, Madereva, Masecretary, Walinzi, Wakuu wa Idara na Vitengo, Makondakta, Waendesha Pikipiki, nk.
 
Kuna hasara gani madaktari wakigoma kurudi kazini?

Madaktari wakirudi kuna hati hati ya kuendelea kututibu chini ya Kiwango. Si unajua Mponda na wenzake wamenunua Vitendanishi feki, hawanunui dawa, vitanda vichache, hakuna ofisi za madaktari, madaktari hawana magari, nk. Yani madaktari endeleeni kukomaa. Huu mgomo hadi sasa umefanikiwa kuliko ulivyotarajiwa!
 
Yani baada ya huu Mziki nadhani fani zote zitaamka kuanzia Manesi, Waalimu, Wahasibu, Wakaguzi, Wahandisi, Maafisa Tawala na Utumishi, Wachumi, Madereva, Masecretary, Walinzi, Wakuu wa Idara na Vitengo, Makondakta, Waendesha Pikipiki, nk.
Hofu ya serikali ndipo ilipo.
 
Hofu ya serikali ndipo ilipo.

Na ndipo tunapotaka tuwafikishe! Tuliwaambia hii nchi haiwezi kutawalika, wakadhani tunatania. Ona sasa walivyonywea. Ari, Nguvu na Kasi zaidi ya JK vimeliwa na nini? Kasi na Viwango vya Samwel Sitta vimepotelea wapi??
 
Back
Top Bottom