mandela1
JF-Expert Member
- Dec 17, 2013
- 837
- 600
bla blaaaaaaaaaa bshxxgxbjshsgssfsgsbvsbsgsgsvsvsvsbsbsbsbsbsbHabari ndugu zangu udaktari ni kazi ngumu sana na inahitaji moyo kuifanya ninawapongeza waliofanikisha na wanaofanya mpaka sasa maana kuna muda inatia stress sana hivyo huwa nao kuna muda huchoka. Licha ya hayo katika madaktari kuna ambao wana jiheshimu na wanao yapeleka mambo wajuavyo bila heshima na kufuata ethics za udaktari.
Kuna matukio mengi sana ya madaktari kutembea na wake za watu ( hapa naongelea madaktari wa kiume na hasa upande wa uzazi) bila mume kujua na kuelewa kwa kweli ukiachana na swala la wadada kujipendekeza wao wenyewe ila hata hawa watu hutumia nafasi zao kuwarubuni.
Mfano kuna mmoja ya binti jirani yangu aliwahi patwa na tatizo la uzazi hivyo alilazimika kwenda kusafishwa kizazi baada ya maelezo mafupi kuhusu hali yake kilichotokea ni kwamba daktari alimwambia kaa kitandani kama ilivyotaratibu kilichofuata akaambiwa toa nguo akatoa zilizo sehemu ya siri akafanya hatua za mwanzo "akamwongopea yule dada kwamba haiwezikani kusafisha njia mpaka kulainishwe basi dada akakubali basi wakati anasubili mara bwana mkubwa anataka kuweka rungu dada akastuka akakataa " kwa kweli hii habari imenisikitisha sana.
Pili kuna wake za watu wanawekewa vikwazo mpaka waweze kushiriki tendo na wataalamu wetu licha ya hilo kuna wale wakipewa huduma kwa sababu wamewachungulia basi madaktari hutumia nafasi hizo kuwatafuta na kuwatafuna.
Lengo langu je kwa nini? Madktari wakike hawafanyi hizi kazi kwa kulinda heshima na kuepuka unyanyasaji wa kisaikolojia kwa mwanamke ? Hata kama ni wachache lakini kwa nini kusiwe na jitihada ili kupunguza hili janga.
Je, haya mambo yapo kwa kiasi gani? Kama unajua sema kidogo juu ya hili na sisi kama jamii hili swala ni sawa?
Je, kuna kuna sheria za kulinda haki ya mgonjwa kati ya daktari (haswa wakiume kwa wakike na kivipi wakati wanakua wawili tu), (daktari wa kike kwa wakiume tusemezane pia kama ipo) ikiwa imebainika kuna unyanyasaji?
Malalamiko yako mengi nimetoa mifano kidogo ili kuelewesha wapi nalenga ila hapa nataka tujadili kwa upana hili swala hivyo nakarbisha mawazo yenu kwa uliyosikia na kushuhudia ili kuona namna ya kulikabili hili tatizo.
Mungu awalinde madaktari wawe na moyo mwema wa kujituma bila tamaa bila kwenda nje ya kanuni zao.
Amina.