Ndugu zangu,
Mkutano wa Rais na Wazee wa Dar es Salaam haukufanyika jaan Ijumaa saa kumi kama ilivyopangwa. Na hautafanyika leo Jumamosi saa tano. Utafanyika Jumatatu saa kumi jioni.
Tafsiri yangu;
Matukio ya saa 48 zilizopita yamebadilisha mwelekeo wa mambo. Kuna hekima iliyotangulizwa. Inaonekana , kuwa Serikali imeamua kuitafuta suluhu ya mgogoro na madaktari kwa kuzungumza na madaktari moja kwa moja na kwa kujifungia- closed door dialogue.
Na safari hii, Bwana Mkubwa ndiye anayeongea na wawakilishi wa madaktari kwa kuwakaribisha Ikulu ya Magogoni. Na yaliyojadiliwa Ikulu hayajawekwa hadharani hadi ninavyoandika tafsiri hii. Ndivyo inavyotakiwa iwe, kuacha kupambana hadharani wakati fursa ya kukutana na kuongea kwa kujifungia chumbani ingalipo.
TBC1 imeripoti jana usiku kuwa mgomo wa madaktari kwa kiasi kikubwa umekwisha. Hapana, yumkini hiyo ni tafsiri ya TBC1, maana, kwa yanayoendelea sasa, yawezekana kabisa kuwa mgomo umesitishwa 'over a week- end' kupisha mazungumzo.
Kwenye ukuta wa facebook wa chama cha madaktari wametangaziwa kuwa leo Jumamosi kunako saa tatu kuna mkutano pale Don Bosco. Bila shaka kutakuwa na kupeana feed-back. Na kesho Jumapili wawakilishi wa madaktari wanakwenda tena Ikulu kuzungumza na Mkuu wa Nchi. Kuna kila dalili watafikia makubaliano katika mambo ya msingi. Hivyo basi, kumaliza mgogoro wao na Serikali na mgomo pia.
Je, ndio kusema Mponda na Nkya watajiuzuru?
Hapana, hilo halitawezekana , na JK ana uwezo wa kuwaambia madaktari na wakamwelewa kuwa hilo haliwezekani. Hawezi kuwaondoa mawaziri hao kwa sasa na ikatafsiriwa kuwa ni kwa shinikizo la madaktari. Naam, mambo ya uendeshaji wa nchi lazima yaende hata baada ya Nkya na Mponda kuondoka. Na ili mengine yaende, hatma ya Mponda na Nkya itabaki mikononi mwa JK.
Na Jumatatu itafika, ama wataanza madaktari wenyewe kutangaza kumaliza rasmi mgomo baada ya kuwa na mazungumzo na Rais na kukubaliana kwenye mambo ya msingi juu ya madai yao, au watasubiri kwanza Rais akutane na Wazee wa Dar es Salaam pale Diamond Jubilee. Alihutubie Taifa, na mbali ya mambo mengine, atangaze rasmi kumalizika kwa mgomo wa madaktari.
Na tusubiri tuone...
Maggid Mjengwa,
Iringa, Jumamosi, Machi 9, 2012