Nafikiri environmental health ya Muhimbili inawahusu zaidi mabwana/ mabibi afya na wanahusika zaidi na usafi wa mazingira ili kuzuia milipuko ya magonjwa kama kipindupindu n.k. Unayoiongelea wewe ya Ardhi, ni uhifadhi wa mazingira kutokana na uchafuzi unaosababishwa na viwanda n.k.
Ni kweli kabisa umefafanua
Mkuu, alichofafanua nadhani nimekiongelea na kusema environmental ni issue pana mno na haimhusu mtu mmoja au section moja tu. Kwa ujumla ni kwamba bila pollution hakuna aspect yoyote ya environmental, iwe health, mechanical, environmental.
GEneral concept ni kwamba hawana kazi na si kwamba hawana kazi bali ni kwamba kila mtu akielimishwa pollutants wa eneo lake basi ni kweli hawahitajiki. Hivi lile vumbi la pale WAZO HILL linahitaji mtaalamu kutoka ARDHI au MUHIMBILI. Hivi Mercury inapounguza miili ya watu kule migodini inahitaji wataalamu hawa.
Hata huko maofisini kuna vumbi unapopekua mafaili. HIli ni suala la kumwelimisha mtu kwamba weka mask puani
Ukicheza utakuwa unafyatua degree za environmental kutoka kila sekta yaani medicine, engineering, geology, aeronautics, marine.
NImeeleza jinsi mizozo ilivyo kazini na kampuni zenye department inayohusika na environmental imekuw aikigombana na section nyingi maana ni kweli hazijulikani zinaongeza nini ambacho wewe usiyesomea hukijui.
OK. Jamaa mmoja hapa chini anasema ilifikia Makamu wa Rais, hayati Omar Ali Juma aliwaondoa. Utaona muelekeo ni uleule yaani kichwani kuna question mark inauliza "
hivi hawa kazi yao ni nini wakati kazi wanazofanya zinaweza kufanywa na wengine".
Kama magonjwa ya mlipuko yalitokea eti kwa sababu walifukuzwa hawa, hivi ni nani hajui kwamba usitupa takataka karibu na nyumbani au karibu na chanzo cha maji.
Achilia mbali huyo Makamu wa Rais aliyefariki miaka mingi iliyopita. Mwaka juzi (2015), Waziri wa Mazingira, yaani Ummy MWalimu alipozidiwa alitoboa siri na kusema suala la "mazingira" ni suala "mtambuka". Mimi nilikuwa sijui maana ya neno "mtambuka" na kwa sababu mimi ni mfuatiliaji wa environmental issues nikafunua dictionary na kuona kumbe anasema kama mawazo yangu, kwamba "environmental is a cutting cross issue" yaani huwezi kusema iwe specific kwa fani fulani tu.
Huhitaji mtaalamu kutoka Muhimbili aje akufundishe kufagia uwanja wako asubuhi. Shuleni tulikuwa tunawahi kila siku kufagia uwanja. Huhitaji mtaalamu wa mazingira kukufudisha kuosha vyombo au kunawa mikono kwa sabuni baada ya kula.
Huhitaji mtaalamu huyo kuweka malori ya kusomba takataka mitaani. Huhitaji mtaalamu kukataza mtu kukojoa ovyo au kutupa karatasi huku na huko. Hizo ni tabia ambazo zikisisitizwa ni kweli hawa watalaamu hata hawahitajiki. Kwa ujumla mazingira ni usafi tu na kila kitu kiko humo.
Mie siamini kwamba hao mabwana/bibi Afya hawana kazi, ukitaka kujua umuhimu wao patokee magonjwa ya milipuko (outbreaks ) na pia wanahusika zaidi na viashiria vyote vya milipuko ya magonjwa na usafi wa mazingira.Kuna mwaka mmoja,makamu wa rais Omary Ally Juma (marehemu)aliwaondoa kazini kisa hakuna walichokuwa wanafanya,haikumaliza wiki 2,milipuko Dar kila kona ikabidi huyo huyo atangaze tena kuwarudisha kazini na malipo juu.Mchango wao upo japo matokeo yake ni ya mda mrefu (long term impacts) ndo maana Mchango wao hauonekani kwa walio wengi.pia miji yetu inaboreka katika usafi kwa sababu wako kazini. Nimefika Arusha wiki 2 zilizopita nimefurahi sana kwa usafi wake.