Madaktari wa China Wawazawadia Watoto wa Zanzibar Tabasamu Jipya Kupitia Upasuaji wa Mdomo

Madaktari wa China Wawazawadia Watoto wa Zanzibar Tabasamu Jipya Kupitia Upasuaji wa Mdomo

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,242
Reaction score
1,212
微信图片_20250512103940.png



Timu ya 34 ya Madaktari wa China waliopo Zanzibar hivi karibuni imekamilisha upasuaji mitano ya midomo iliyopasuka juu na upasuaji 19 ya matatizo ya kaakaa kwa watoto ndani ya siku tano tu, huku kila upasuaji ukifanywa bila shida yoyote na hatimaye kurejesha afya na kuwapatia zawadi ya tabasamu watoto hao.

Upasuaji huo ulikuwa sehemu ya " Wiki ya Upasuaji wa Midomo iliyopasuka Juu na Kaakaa," iliyoendelea kwa siku tano, ambayo ilipewa kauli mbiu ya "Safari ya Tabasamu,". Wiki hii imeandaliwa na Timu ya Madaktari wa China ili kuboresha afya za watu, kutoa utaalam wa matibabu na kuimarisha ushirikiano na wenzao wa Tanzania.

Kati ya wagonjwa watoto alikuwepo Ibrahim Abdulnassir Ramadhan, mtoto wa kiume wa mwaka mmoja kutoka Zanzibar. Akiwa amezaliwa na mdomo uliopasuka juu, Ramadhan alikabiliwa na ugumu wa kula na mara kwa mara alilia kwa sababu ya usumbufu. Wazazi wake walikuwa wakihaha kutafuta msaada lakini walihofia kuwa hawataweza kumudu matibabu.

"Wakati nilipomshika kwa mara ya kwanza, nililia. Sio kwa sababu ya hali yake, lakini kwa sababu niliogopa walimwengu hawatakuwa wema kwake," alisema Raya Rashid Omar, mama wa mtoto huyo. "Watu wanamwangalia sana. Wengine hata waliniambia kwamba nimfiche. Sikutaka kuonewa huruma, ila nilihitaji msaada tu."

Matumaini yao yalibadilika kuwa hali halisi baada ya kupata taarifa juu ya "safari ya tabasamu inayoongozwa na Wachina." Baada ya uchunguzi wa awali, mtoto huyu alichaguliwa kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji katika Hospitali ya Lumumba.

"Nilikuwa na woga. Yeye ni mdogo sana," alisema Abdulnassir Ramadhan Suleiman, baba wa mtoto, huku akiingalia timu ya madaktari ikimchukua mtoto wake na kumpeleka kwenye chumba cha upasuaji. "Hatahivyo madaktari walimwangalia kama tunavyomwangalia sisi. Walimwona mtoto ambaye anastahili kuwa na siku njema baadaye."

Ukiongozwa na Fang Jin, daktari wa upasuaji wa mdomo, taya na uso kutoka timu ya madaktari wa China, upasuaji uliendelea vizuri. Fang alifanya kazi pamoja na madaktari watatu wa Tanzania wanaotoka mjini Dodoma. Kwa pamoja, waliunda timu ya wataalamu iliyoratibiwa vizuri.

Katika kipindi chote cha siku tano, timu ilifanya kazi bila shida, ikifanya kila upasuaji kwa usahihi na umakini. Baada ya kufanya upasuaji, waliwakagua wagonjwa kila siku ili kuangalia kama wanapona vizuri na kuhakikisha wanapata matokeo bora.

Wakati Ramadhan alipoamka baada ya upasuaji, wazazi wake hawakuweza kuzuia hisia zao.

"Kwa mara ya kwanza, nilimuona akitabasamu bila kuwa na maumivu," alisema mama huyo, huku akizuia machozi. "Alionekana kama vile alikuwa akisubiri kwa hamu kuwa mtoto mwenye hali hii nzuri."

Mabadiliko hayo sio tu kwamba yaliwagusa moyoni watumishi wa afya bali pia watu wanaojitolea katika Hospitali ya Lumumba. Watoto wengi, ambao awali walikuwa na aibu au wakimya, walianza kucheza na kucheka kwa uhuru wakiwa na sura zao mpya zilizoponywa.

Fang alikumbuka wakati mama huyo alipomshika mkono wake barabara baada ya upasuaji. "Hakusema maneno mengi. Ila tu 'Daktari wa China, asante.' Lakini macho yake yalisema kila kitu, "alisema.

Wataalamu bingwa wenyeji pia walielezea juu ya uzoefu huo. "Ushirikiano huu na timu ya Wachina umekuwa ukitufungua macho. Sio tu kwamba tumejifunza mbinu za hali ya juu bali pia tuliona macho ya huruma wakati wa kufanya upasuaji," alisema Seseja, mmoja wa madaktari watatu wa Tanzania.

"Madaktari wa China hawakuleta utaalam tu bali pia uaminifu na matumaini," alisema Sumaiya kutoka kitengo cha meno cha Hospitali ya Lumumba. "Uadilifu huu wa kuvuka mpaka unagusa kweli."

Hadi wiki ya upasuaji inamalizika, watoto 24 walikuwa wamefanyiwa upasuaji wa kuwabadilisha. Kwa familia kama za Ramadhan, matokeo hayo yalikuwa ni zaidi ya matibabu.

"Hukurekebisha mdomo tu," alisema Suleiman huku akimwangalia mtoto wake akiwa amelala mikononi mwake. "Umempa nafasi ya kuukabili ulimwengu kwa ujasiri. Hiyo ni zawadi ambayo hatutakuja kuisahau."
 
Back
Top Bottom