Madaktari saidia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Madaktari saidia

Discussion in 'JF Doctor' started by Baija Bolobi, Oct 17, 2009.

 1. B

  Baija Bolobi JF-Expert Member

  #1
  Oct 17, 2009
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 931
  Likes Received: 697
  Trophy Points: 180
  Mke wa jirani yangu kalazimika kumwachisha mtoto kunyonya akiwa na umri wa miezi mitatu kwa sababu anakwenda shule. Maziwa yanazidi kutiririka na kumletea homa. Je atumie dawa gani ili kuyakausha? Madaktari saidia.
   
 2. Visenti

  Visenti JF-Expert Member

  #2
  Oct 17, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 1,031
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 133
  Mkuu Baija, hili si jambo rahisi kihivyo ukizingatia maamuzi yanahusisha kiumbe ambaye kunyonya ni haki yake ya msingi kwa ustawi wa afya yake, pili hizo dawa zinahitaji cheti cha daktari baada ya kuzingatia mambo ya kitaaluma na miiko ya fani (ethics), kitaaluma si sahihi kumshauri mhusika kuhusu dawa za kukata maziwa katika jamvi hili.

  Kwa maoni yangu huyo mtoto ana bahati mbaya sana. Kuna sababu za msingi za kutonyonyesha mtoto, kwenda shule si sababu tosha. Kuahirisha shule ili kumnyonyesha mtoto ni maamuzi ya busara zaidi kwa ustawi wa mtoto huyo, hata kama familia inauwezo wa kununua chakula bandia/mbadala (artificial infant feeds).
   
 3. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #3
  Oct 17, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Siyo busara kumwachisha mtoto kunyonya katika umri huo. Labda kama ni lazima sana tena sana. Lakini naamini angeweza kuomba akaahirisha shule ili amlee mtoto wake na kurejea shule mwakani. Kama hiyo imeshindikana basi itabidi ayakamue hayo maziwa na kuyamwaga kwa siku za mwanzo. Baada ya muda yataacha yenyewe. Sidhani kama daktari atampatia dawa ya aina yoyote. Hata hivyo kama anaanza kupata homa akamwone daktari haraka kwa sababu anaweza kuwa amepata maambukizi yanayosababisha kuvimba kwa matiti na kusababisha maumivu makali sana (mastatis). Kama kashepata mastitis basi atapewa antibiotics.
   
 4. MNDEE

  MNDEE JF-Expert Member

  #4
  Oct 17, 2009
  Joined: Jul 10, 2009
  Messages: 494
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  Mie sio daktari, but I will give you my two cents. Wako akina mama wafanyakazi na wanafunzi na wananyosha watoto wao kama kawaida. Hiyo sio sababu ya msingi kuachisha mtoto kunyonya maziwa ya mama.

  Mama anaweza kukamua maziwa kwa kufumia vifaa vya kukamulia maziwa au kukamua kienyeji na kuyatunza vizuri kwenye chupa za kunyonyea mtoto na kuweka frijini. Muda wa mtoto 'kula' ukikaribia chemsha maji kwenye chombo simamisha chupa ya mtoto maziwa yapate joto nyonyesha mtoto.

  Mama akamue maziwa asubuhi kabla ya kuondoka, na mchana akiwa huko 'shule' provided anaweza kupata friji ya kutunzia maziwa hadi arudi nyumbani.
  • Kwa afya ya mtoto hakikisha hii shughuli inafanyika kwa usafi wa hali ya juu, kuanzia kusafisha ziwa, vyombo vya kukamulia na kutunzia maziwa.
  • Mara mtoto amalizapo kunyonya chupa isafishwe na kutunzwa vizuri, kama maziwa yamebaki baada ya mtoto kunyonya mwaga na safisha chombo.
  • Maziwa kama ni mengi au hayatatumika siku yamekamuliwa tunza kwenye freeza.
   
 5. m

  mchajikobe JF-Expert Member

  #5
  Oct 17, 2009
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 2,366
  Likes Received: 661
  Trophy Points: 280
  Huyo mi simsaidii kingine zaidi ya kumwambia kuwa yakitoka awe ananyonya mwenyewe,si anataka chakula ya toto?
   
 6. J

  Justin Dativa Member

  #6
  Oct 17, 2009
  Joined: Oct 11, 2008
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  I am impressed by all the very matured and informed responses to the lady who wants to stop breast feeding and attend school. She should definetly see a Doctor and I mean a Doctor with capital D and not a doctor for advise although of course if she cares she has almost had 90% of the dvice she needs from the gentlemen and gentleladies on this forum.
  Kama baba yako ni mwizi na wewe ni mwizi tu, hadi utakapo mkana na kutengana naye. Ah! basi wewe siyo mwanae maana hata baba ana kilema gani humkani, huachani naye. Unamsaidia(siyo kwa kuiba) kwa mfano hapa kubadilisha tabia!
   
 7. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #7
  Oct 17, 2009
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  roho inaniuma sana coz nina mdogo wangu wa kike ambaye hakunyonya wakati akiwa mdogo sababu mama alipojifungua kwa operesheni miaka ya 1979 kidonda kilimpa tabu sana kupona takriban miezi 7 alikuwa mzito sana kuelewa darasani moja ya sababu ma dr walio sites ni kutokunyonya maziwa ya mama lkn aliyefuata alinyonya full huyu naye wakike darasani alikuwa first hasa hesabu anazikokotoa balaa sasa kutomnyonyesha huyo mtoto ni kumnyima haki ya msingi na hata kumbaribia future yake
   
Loading...