madaktari muhimbili WACHAFU

kupe

JF-Expert Member
Jul 26, 2012
1,035
326
Naongelea madaktari mnaishi kwenye hizi flats hapa nyuma ya kituo cha daladala super star upanga njia ya kwenda muhimbili karibu na hii super market mpya ya ETNS . Nyumba zimezungukwa na majalala ya uchafu , ma sim tank yanajaa maji hadi yanamwagika usiku kucha (DOKTA UNASHINDWA KU CONTROL MAJI UNAYOFUNGULIA MWENYEWE). Majani yameota hadi milango ni mwa nyumba zenu. Miti imeota kwenye kuta hadi juu ya nyumba . Hivi dokta unashindwa kusafisha nje tu ya nyumba yako. jirekebisheni acheni mambo ya SIASA, KULEWA , KUGOMA NA KUBADILISHA WANAWAKE. usafi kwanza.
 
waqdai nyumba wakati nyumba walizopewa wakae ni wachafu kwenda mbelee... na kufanya usafi kwako unangoja serikali ije ikufanyie ...watz
 
Hawea jamaa ni wachafu na watata sana kwani wanajiona ni bora kuliko watu wa fani ingine, ndio maana wanajifanya hata muda wa kulima ka-bustani au usafi wa mazingira hawafanyi ila kwa kilaji huwakosi katika kaunta, wakihadithia wagonjwa wao na siasa aa mm sina hamu nao angalieni hata wawakilishi ambao ni Wabunge kaliba zao
 
Madaktari wanahadithia habari za wagonjwa wao?
 
Utawaona wanapita na makoti yao meupeeee. Hata aibu hawaoni mazingira wanayoishi. Wanajiona bora kuliko hata wazazi wao
 
Harafu wanaongoza kwa kutoa siri za wagonjwa bar . Wapo kaunta Utawasikia usimuone vile yule demu usimuone vile mzuri alikuja hospital ana ukurutu kwenye mapaja. Mara utawasikia KIBONGE ana ngoma nimempa leo ARV
 
Zile nyumba kweli ni chafu na pananuka haswaa! Mvua ikinyesha panajaa maji wanaweka mawe unarukaruka mpaka mlangoni. Ujumbe uwafikie wakazi wa zile flats
 
Harafu wanaongoza kwa kutoa siri za wagonjwa bar . Wapo kaunta Utawasikia usimuone vile yule demu usimuone vile mzuri alikuja hospital ana ukurutu kwenye mapaja. Mara utawasikia KIBONGE ana ngoma nimempa leo ARV
Mh!wewe hiyo sentensi ya mwisho umezuga ila tumekuelewa!
 
Jamani msikurupuke. Hiizo flats ni za NHC. Zimepangishwa kwa Muhimbili National Hospital ambayo nayo imepangisha madaktari wanaosomea degree ya pili ya udaktari bingwa. Miaka nenda rudi, wamiliki (NHC), MNH, pamoja na wahusika wa maji taka (DAWASCO) wameshindwa kutatua shida ya mfumo wa maji safi na taka. Sasa nyie mnataka hao madaktari wazibue na kujenga mfumo wa taka kwa mikono yao? Kumbuka, wanaoishi kwenye hizo flats hupangishwa kwa muda usiozidi miaka mitatu tu na kupangishwa watu wengine tena.
 
Utawaona wanapita na makoti yao meupeeee. Hata aibu hawaoni mazingira wanayoishi. Wanajiona bora kuliko hata wazazi wao

Bado tu una uchungu wa kushindwa kuwa daktari? Maksi hazikutosha ndugu, punguza hasira.
 
Harafu wanaongoza kwa kutoa siri za wagonjwa bar . Wapo kaunta Utawasikia usimuone vile yule demu usimuone vile mzuri alikuja hospital ana ukurutu kwenye mapaja. Mara utawasikia KIBONGE ana ngoma nimempa leo ARV

kupe wanaompa Dr. Slaa siri za serikali nao pia ni madaktari?
 
Last edited by a moderator:
hii thread kweli inamaana ya uchafu kweli au mmetumwa? mambo ya siasa na migomo yametoka wapi? acheni mambo yenu.
 
mhhhh! Hapa kuna tabu naona!

mleta mada ana lake. Sidhani kama ishu ni 'uchafu' peke yake, utakuwa una agenda yako nyingine. Mara mgomo, mara siri za wagonjwa, mara walevi, mara kubadilisha wanawake. Kwa nini ndugu una chuki kubwa na madaktari kiasi hichi.

Ujumbe wako ni mzuro ya kwamba nyumba za muhimbili ambazo by the way ni za NHC ni chafu. Na mdau hapo amekujibu si DAWASCO wala MNH wala NHC walio na utayari wa kurekebisha hilo tatizo japo wanapewa taarifa mara kwa mara. Tenants wa hizo nyumba ni 'wanfunzi' ambao hawana permanent residence pale:

otherwise thread yako ina-aminisha watu kwamba madaktari ni wachafu na wana sifa zingine zisizofaa.....

Kweli una hamu ya kuwa daktari naona baada ya kushindwa sasa unakandia tuu, pole sana
 
hivi ukipanga nyumba kwa miaka mitatu ndio hao hao NHC wakufanyie usafi? Wakufungie maji ukifungulia? Wakuchimbie mashimo ya taka? HIVI MKIACHA KUNYWA BIA MOJA MOJA KILA MMOJA TU KWA WEEK 1. hamuwezi kujichangisha na kuchimbisha shimo la taka . Maana hata wanawake hamuhongi mnawapata bure kwa kupitia u dokta wenu
 
Duh nimecheka sana kweli ma dokta wa sasa vilaza. Sasa dokta SLAA ameingiaje hapo kwenye uchafu wenu? Kuna mwingine ndio hana upeo kabisa bado ana idea za kizamani anadhani watu wote wenye ni lazima wawe madaktari. Lets mimi nilienda kusomea mambo ya acounts au tax. Sasa hivi nafanyakazi BOT au nipo supervisor MIZANI KIBAHA. huo mshiko wangu hunipati hata robo utaishia kuniomba bia tu bar. Na siku nikuguliwa nikakupigia simu utakuja unakimbia kama kuku wa kienyeji kuja kunitibu upate hela ya kula
 
Dharau za namna hii hazifai...
 
Jamani msikurupuke. Hiizo flats ni za NHC. Zimepangishwa kwa Muhimbili National Hospital ambayo nayo imepangisha madaktari wanaosomea degree ya pili ya udaktari bingwa. Miaka nenda rudi, wamiliki (NHC), MNH, pamoja na wahusika wa maji taka (DAWASCO) wameshindwa kutatua shida ya mfumo wa maji safi na taka. Sasa nyie mnataka hao madaktari wazibue na kujenga mfumo wa taka kwa mikono yao? Kumbuka, wanaoishi kwenye hizo flats hupangishwa kwa muda usiozidi miaka mitatu tu na kupangishwa watu wengine tena.

mhhhh! Hapa kuna tabu naona!

mleta mada ana lake. Sidhani kama ishu ni 'uchafu' peke yake, utakuwa una agenda yako nyingine. Mara mgomo, mara siri za wagonjwa, mara walevi, mara kubadilisha wanawake. Kwa nini ndugu una chuki kubwa na madaktari kiasi hichi.

Ujumbe wako ni mzuro ya kwamba nyumba za muhimbili ambazo by the way ni za NHC ni chafu. Na mdau hapo amekujibu si DAWASCO wala MNH wala NHC walio na utayari wa kurekebisha hilo tatizo japo wanapewa taarifa mara kwa mara. Tenants wa hizo nyumba ni 'wanfunzi' ambao hawana permanent residence pale:

otherwise thread yako ina-aminisha watu kwamba madaktari ni wachafu na wana sifa zingine zisizofaa.....

Kweli una hamu ya kuwa daktari naona baada ya kushindwa sasa unakandia tuu, pole sana

Wakati mwingine ni bora mkae kimya kuliko kueteta vitu visivyo na msingi. Kuota majani mpaka mlangoni waje wafyeke NHC? Maji kumwagika toka kwenye simtank waje wazuie DAWASCO?
I think our biggest problem as a nation is the way we think...
 
Man umemaliza kila kitu! na mimi kuongezea tu ni kwamba sisi ni wavivu sana na sijui tatizo ni lakibailogia (genetic) au sijui tumelikuta hapa hapa Duniani, na siku zote huwa tunapenda kulaumu mtu mwingine bila ya kujiangalia sisi kwanza , kwa maana katika hali ya kawaida mimi nilitegemea kwamba hawa jamaa (wanaoitwa madaktari bingwa) wanafundishwa mambo ya Afya hivyo mazingira yao kuwa machafu ina contradict kila kitu kuhusu hii fani ya Udaktari, kwa hali ya kawaida na kwa mtu ambaye kweli ameiva kwenye fani yake nilitegemea awe wa kwanza kuandanama na kushinikizika hao Dawasco basi warekebishe au wenyewe wajitolee kusafisha hata mara moja tu mwezi basi!
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom