Madaktari jiepusheni na genge la kina Mwaipopo.

Kiby

JF-Expert Member
Nov 16, 2009
6,899
4,623
Kuna genge moja jijini DSM limejivika cheo cha jopo la viongozi wa kidini. Sii kweli kwamba watu hawa ni viongozi wa kidini bali ni genge la wajanja fulani ambao wamekuwa wakihaha kila kona ya nchi kutafuta watoke vipi. Walianza na mihadhara ya kukashifiana kwa tofauti za kidini, kujiingiza katika kuwatapeli watu mashuhuri ama tajiri kama kina Mengi, Manji nk. Sasa wanatumiwa na Ikulu dhaifu ya Jk kuwavuruga wananchi kwa propaganda. Nilishangaa Madaktari ni wapi walitaimiwa na mpaka kunasa ktk mtego wa kina Mwaipopo ambae ni form for failure na genge lake kina msopa darasa la saba. Hivi MDr's hamkuweza kuwabaini hawa watu kuwa hawana uwezo wa wazo lao wenyewe ila kile walicholishwa? Angalieni sasa jinsi wanavyowananga kuwa watawapeleka mahakamani baada ya ushauri wao wa kuwataka kuandika barua ya kumwomba radhi Kikwete kukataliwa. Kama MDr's mnabisha jaribuni kukutana na Mwaipopo na mutake ku-sam up mazungumzo yenu muone kama ana uwezo wa kuyakumbuka. Hapo ndio mtajiridhia kuwa mlikuwa mnajadiliana na mtu aliyekuwa analishwa cha kujadiliana na ninyi kutoka chanzo kingine na wala sii wao kama wao kwa jinsi walivyojinasibu. MDr's p/se hamjawa cheap kiasi hicho.
.
 
mkuu, umetumia lugha ya kishairi,ngumu mi kuelewa

.
Bana nina mengi sana kichwani yaliyonipa uchungu jinsi madaktari walivyokuwa na dhamira pana ya kuhakikisha usalama wa afsa ya mtanzania inazingatiwa kwa miundo mbinu kuboreshwa. Sasa badala yake serikali imetumia propaganda kupitia vilaza(vibaraka) ninavyovifahamu fika. Imeniuma sana hata nimeshindwa nianzie wapi na nimelizie wapi.
.
 
sipati picha mkristo atakaposhika nchi 2015!! Sijui hawa jamaa wataongelea nini? Maana kila anayesema uovu wa serikali ya jk hawa jamaa wanakuja na mapovu mengi kweli!! Hivi makao makuu yao wamehamishia ikulu?
 
Hapana! Mi kwangu bado nina hofu na mleta thread!

Mapofu yanamtoka utafikiri anatumiwa!

Hakuna fara hapa nyakati hii ya uwazi na ukweli!
 
Back
Top Bottom