Madaktari: Hiki ndicho kilichomuua Kanumba

mkuu hao madaktari naona wanazungumzia mtikisiko wa ubongo,ambao hawajaeleza unasababishwa na nini?na kipi kilisababisha ukatokea kwa huyu marehemu.
 
Kama sio Lulu basi kuna mwingine mwenye kesi ya kujibu. Concussion haitokei bila kugongwa ama kujigonga. Ila ile story ya Kanumba alilegea akaanguka inaweza kumtoa (after walau 3 years). Akitoka huko atakuwa mkubwa, anaweza kugombea ubunge wa vijana ccm

Akitoka atataja umri wake wa kweli au atadanganya tena tumpe cheo UVCCM.
 
jamani someni muelewe sio kukimbilia kujandika pumba,

mbona ilivyoelezwa kesi bado ipo? au mnadhani wanaongelea nini?

ukishindwa kuelewa na kuamini wanaoeleza humu nenda ka google.
 
So kama haki itatendeka Lulu atakuwa huru ahame nchi..bt yule mdogo wa SK,mzito mzito flan hata mdomo yan kalegealegea,hakuwa seriouz tangu bro aanguke et ad doc wake aje!je kama asingepokea cmu?kwan alishndwa kupiga kelele majiran waje,au hata fasta fasta wangemuwahisha hosptal ya karibu af ndo ampgie doc wake,kwamba tupo sehem flan coz kwa nlivoelewa hiyo brain concussion angeweza kuomba hata maji,bt walilichukulia tatizo ki-star zaidi! Af pili kutokana na causes za tatizo,lazima kuna reason behind the scene! It is very confussing lakini! May his soul Rest in peace!
 
......madokta tuelezeni vizuri....nini husababisha hyo concusion...
Na hamjatuambia hali ya sehemu yake ya kichwa alipodondokea....

....shaur yenu kama mwamlinda Lulu.....watu wana hasira nae mtaani.
 
Huyu dogo sina imani nae kabisa, ndo ivo walikua wawili tu chumbani lkn pana siri kubwa hapa.
Na km watmwachia huru, basi ni kweli wamhamishe nchi la sivo maisha yake yapo hatarini.
Km biggie baada ya kifo cha tupac.
Pumzika kwa amani SK, kufa kumeumbwa lkn kutangulia kunauma hasa kwa kijana mdogo km Kanumba.
 
Kama sio Lulu basi kuna mwingine mwenye kesi ya kujibu. Concussion haitokei bila kugongwa ama kujigonga. Ila ile story ya Kanumba alilegea akaanguka inaweza kumtoa (after walau 3 years). Akitoka huko atakuwa mkubwa, anaweza kugombea ubunge wa vijana ccm

hahahahahahaha!
 
So kama haki itatendeka Lulu atakuwa huru ahame nchi..bt yule mdogo wa SK,mzito mzito flan hata mdomo yan kalegealegea,hakuwa seriouz tangu bro aanguke et ad doc wake aje!je kama asingepokea cmu?kwan alishndwa kupiga kelele majiran waje,au hata fasta fasta wangemuwahisha hosptal ya karibu af ndo ampgie doc wake,kwamba tupo sehem flan coz kwa nlivoelewa hiyo brain concussion angeweza kuomba hata maji,bt walilichukulia tatizo ki-star zaidi! Af pili kutokana na causes za tatizo,lazima kuna reason behind the scene! It is very confussing lakini! May his soul Rest in peace!
Kwa kifupi kabisa kama yaliyoripotiwa yote ni kweli basi Huyu mdogo wake Kanumba anapaswa kubeba lawama nzito na ninashauri baada ya mazishi ya leo huyu mdogo wake Marehemu Kanumba akamatwe na kuhojiwa kwa uzembe wa kutaka kuficha skendo la ufuska kati ya Lulu na Kanumba, hakuna Mtanzania mwenye utaratibu wa kuita daktari nyumbani panapotokea ugonjwa wa dharura.
Simply i don't buy this story. Dr wa Michael Jackson yuko jela kutumikia kifungo kwa uzembe unaofanana na huu uliyogharimu maisha ya Steven Kanumba.
 
concussion (kənˈkʌʃən)

— n
1.Pathology . injury to the brain or spinal cord due to jarring from a blow, fall, or the like.
2.shock caused by the impact of a collision, blow, etc.
3.the act of violently shaking or jarring.
4.a jarring of the brain, caused by a blow or a fall, usually resulting in loss of consciousness
5.any violent shaking; jarring

jar
   [jahr] Show IPA verb, jarred, jar·ring, noun
verb (used without object)
1.to have a harshly unpleasant or perturbing effect on one's nerves, feelings, thoughts, etc.: The sound of the alarm jarred.
2.to produce a harsh, grating sound; sound discordantly.
3.to vibrate audibly; rattle: The window jarred in the frame.
4.to vibrate or shake.
5.to conflict, clash, or disagree.
6.to cause to rattle or shake.
7.to have a sudden and unpleasant effect upon (the feelings, nerves, etc.): The burglary violently jarred their sense of security.
8.to cause to sound harshly or discordantly.
9.a jolt or shake; a vibrating movement, as from concussion.
10.a sudden unpleasant effect upon the mind or feelings; shock.
11.a harsh, grating sound.
12.a discordant sound or combination of sounds.
13.a quarrel or disagreement, especially a minor one.
 
MSANII nyota wa filamu nchini, Steven Kanumba amefariki dunia kutokana na tatizo la mtikisiko wa ubongo linalojulikana kitalaamu kama Brain Concussion, taarifa za kitabibu zimeeleza.

Taarifa hizo za ndani, zilizopatikana jana baada ya jopo la madaktari bingwa watano wa Hospitali ya Taifa Muhimbili kuufanyia uchunguzi mwili wa marehemu huyo, zimeeleza kuwa tatizo hilo linaweza kumfanya mtu apoteze maisha mara moja au baada ya siku kadhaa. Mmoja wa madaktari hao ambaye aliomba jina lake lisitajwe gazetini alisema waligundua tatizo hilo baada ya kumfanyia uchunguzi huo kwa zaidi ya saa mbili.

“Tulianza kuufanyia uchunguzi mwili wa marehemu kuanzia saa 4:00 asubuhi hadi saa 6:45 mchana na tukagundua kuwa marehemu alifariki kutokana na mtikisiko wa ubongo kwa kitaalamu, Brain Concussion,” alisema daktari huyo. Alisema Kanumba alipata mtikisiko wa ubongo ambao husababisha kufeli kwa mfumo wa upumuaji (
cardio-respiratory failure) “Kilichomuua hasa ni mtikisiko wa ubongo, ambao endapo unatokea katika sehemu ya nyuma ya ubongo (cerebrum), huua kwa haraka” alisema daktari huyo na kuongeza kuwa mtikisiko wa ubongo wa nyuma, husababisha matatizo ya mfumo wa upumuaji na hilo limeonekana katika mwili wake.

“Baada ya ubongo wake kutikiswa kwa nguvu, mfumo wa upumuaji ulifeli na ndiyo maana tumekuta kucha za Kanumba zikiwa na rangi ya bluu, huku
mapafu yake yakiwa yamevilia damu na kubadilika kuwa kama maini, hizo ndizo dalili za kufeli kwa mfumo wa upumuaji.”

“Mtu aliyepata mtikisiko wa ubongo huweza kutokwa na
mapovu mdomoni na hukoroma kabla ya kukata roho na ndivyo ilivyokuwa kwa Kanumba kabla hajafariki.”

Daktari mwingine aliyeshiriki katika uchunguzi huo ambaye pia aliomba jina lake lisitajwe alisema
ubongo wa mwigizaji huyo ulikuwa umevimba na kushuka karibu na uti wa mgongo na hivyo kuathiri mfumo wa upumuaji.

Dalili zinazoonyeshwa na madakatari hawa kutokana na autopsy zinaonyesha kuwa Kanumba alikuwa na kitu kinachoitwa "epidural hematoma." Kutokana na kuanguka kwa kawaida tu na kujigonga kwenye ukuta au sakafu, tatizo hili lisingejitokeza mara moja mpaka baada ya muda mrefu kidogo. Ndiyo maana wapigana ngumi na wacheza futiboli ya kimarekani hupata head trauma sana lakini dalili zake zinakuja kujitokeza miaka mingi baada ya wao kustaafu. Watu wote walioripotiwa kufa kutokana na tatizo hili kwa kuanguka, hasa kwenye michezo ya kwenye barafu, huwa wamaunguka kutoka kima cha juu kidogo, na huanza kupata kizunguzungu na mwishoni kufa baada ya muda mrefu kidogo kati ya nusu saa (severe impacts) hadi hata siku nzima tangu wapate hiyo impact ya kichwa. Ili tatizo hili likue ghafla na kusababisha kifo, inabidi impact ya kichwa iwe ni kubwa sana kwa ama kuanguka kutoka kwenye ngazi, accident ya gari lilikuwa katika mwendo wa kasi, au kupigwa kwa nguvu sana na kitu kigumu kama rungu.

Kwa hiyo kuna mambo mawili ya kuangalia:

(a) Je kulikuwa na silaha yoyote kama vile rungu au nondo iliyopatikana chumbani kwa Kanumba ambayo ilitumiwa na Lulu kumpigia Kanumba kichwani? Kama ipo, finger prints zinaweza kusaidia kuonyesha ni mtu gani aliyetumia silaha hiyo, unless kama crime scene imekwisha kuwa contaminated.

(b) Je Kanumba aliwahi kupata trauma ya kichwa ama mchana huo au jana yake halafu trauma hiyo ikaja kutoneshwa na impact nyingine wakati tayari ubongo ulishaanza kuvimba?.

Vile vile kutokana na ukweli huo wa tatizo linaloweza kuwa limemuua Kanumba, inaonyesha pia kulikuwa na uzembe uliofanyika katika kujaribu kuokoa maisha yake. Muda mwingi sana ulipotea kabla hajafikishwa hosptilai na kupata huduma; alikufa kabla hajapata huduma yoyote. Iwapo angewahishwa emergency room na kufanyia CT scan ya kichwa, ni dhahiri kuwa madakatri wangeliona tatizo hilo kabla halijwa fatal na hivyo wangemfungua kichwa chake kuruhusu uvimbe uishe kwanza kusudia ubongo usiharibike kabla ya kukifunika tena.
 
labda niulize,SO lulu is innocent mpaka apo
 
labda niulize,SO lulu is innocent mpaka apo

Sheria zetu zinasema kuwa yupo innocent until proven guilty.

Akipata wanasheria wazuri, anaweza kuachiwa huru kwa sababu kadhaa. (a) Inawezekana kanumba alianguka kwa bahati mbaya, ingawaje impact ya kuanguka kutoka kwenye upright position haiwezi kusababisha madhara makubwa kama hayo. (b) Inawezeka kanumba alipata impact kubwa siku za nyuma kidogo na hivyo tatizo lilikuwa linakua pole pole mwilini; madakatari hawakueleza kiundani kuhusu muda wa concussion kutokea. (c) Inawezekana Lulu alimpiga kanumba na kitu kigumu kichwani kwa nguvu sana; lakini kwa vile polisi hawaku-secure crime scene, kukawa hakuna ushahidi wa kutosha kuonyesha kuwa Lulu alifanya hivyo. (d) Na hata iwapo Lulu alimpiga Kanumba na kusababisha kifo chake, bado Lulu anaweza kuachiwa huru iwapo upande wa mashitaka ukishindwa kuonyesha kuwa alifanya hivyo kwa makusudi akiwa amenuia ama kumdhuru au kumuua Kanumba.

Tuache sheria ichukue mkondo wake, lakini ifanye hivyo kwa kuangalia haki ya marehemu kanumba na haki ya mtuhumiwa Lulu kwa uzito sawa.
 
Labda kweli alianguka kwa bahati mbaya au alijigonga sehemu, Lulu nae apewe sehemu ya kujieleza, asionewe bure mtoto wa watu. Kama Lulu ni kicheche kwa nini marehemu alitembea nae..

Apewe nafasi ya kutueleza yaliyojiri siku hiyo.
 
Kwa aina ya ripoti hii, inamtoa mojakwamoja kwenye jinai huyu binti!

Nasubiri DPP atalifikisha mahakamani au???
 
Labda kweli alianguka kwa bahati mbaya au alijigonga sehemu, Lulu nae apewe sehemu ya kujieleza, asionewe bure mtoto wa watu. Kama Lulu ni kicheche kwa nini marehemu alitembea nae..

Apewe nafasi ya kutueleza yaliyojiri siku hiyo.

Lulu hawezi kisheria kuja kuelezea hapa/vyombo vya habari kama ushahidi wa kilichotokea, bali yeye maelezo yote yapo polisi na tayari DPP anasubiri jalada lake!

Hadithi zoooooote zinazopigwa huku hazina nguvu kisheria ikiwa sisehemu ya ushahidi uliopo pilisi!
 
Kwa mujibu Wa mpiga Picha mkuu Wa marehemu kumbe kuna filamu ambayo haijatoka kanumba ameigiza amekufa kwa kusukumwa na mpenzi wake.. Kama ilivyotokea kiuhalisia.. Pia hata Ule wimbo wake unazungumzia Kifo chake.

Source. TBC habari usiku huu.
 
Back
Top Bottom