Matatizo sio hayo tu, tazama Kikwete anavyohangaika kuleta wawekezaji, anahangaika kuwaomba waweke vitivo vya sayansi Dodoma, amewaomba wachina waweke kituo cha utafiti wa kilimo (nadhani Morogoro kama sikosei). Nna uhakika wakiondoka, sisi hatutoweza, kwa sababu bado, bado, bado.
Tunahitaji tukakae sana na Mzee Mahathir Muhammad kabla hajafa atuelezee aliwezaje? tena tuwe serious kweli kweli. La sivyo? maendeleo tutayasikia tu katika kizazi chetu hiki.
Ikiwa lei Kikwete kafanya kuliko Rais yeyote wa kabla yake na tunamuona hajafanya unafikiri nani ataeweza? just kwa kuwa ni wa tabaka fulani tu, chuki, uhasidi, kejeli, "sabotages", kwa kuwa tu hajatoka katika kundi fulani. Huu ni ugonjwa mbaya sana tulipkuwa nao.
Leo ukimuuliza mtu akwambie nioneshe ambacho walifanya Marais waliopita ambacho Kikwete hajakifanya zaidi yao, hakuna anaeweza, kwani kafanya kweli, sasa kama rais aliyefanya kuliko Rais mwingine yeyote wa kabla yake mnashindwa kukubali aliyoyafanya kwa sababu tu hajatoka kwenye tabaka lenu, huo kama sio uchawi ni nini? Unafikiri uchawi mpaka uende ukatazame nyota? hao watazama nyota wamejaa dunia nzima, lakini uchawi wa kweli ni huu, wa kutothamini mtu kwa tabaka lake tu na si zaidi ya hapo.