Madaktari 50 toka India kutua nchini kesho

thatha

JF-Expert Member
Apr 29, 2011
15,340
1,566
29 August 2012
Madaktari 50 kutoka India kutoa tiba Dar

Na Salim Nyomolelo

JOPO la madaktari 50 kutoka nchini India, wanatarajia kufanya maonesho ya matibabu katika ukumbi wa Diamond Jubilee Agosti 30 hadi 31, mwaka huu, kuanzia saa nne asubuhi hadi 11 jioni.


Taarifa iliyotolewa kwa waandishi wa habari Dar es Salaam jana na Balozi wa India nchini, Bw. Debnath Shaw, ilisema maonesho hayo yameandaliwa na Taasisi ya Shirikisho la Biashara nchini India la Medical Tourism Destination (IMTD).

Aliwaomba watu wenye matatizo mbalimbali ya kiafya wajitokeze katika maonesho hayo ili waweze kupata huduma ya matibabu ambayo itatolewa katika ukumbi huo kwa gharama za chini.

"Gharama zao zitakuwa za chini na zitamwezesha kila mwananchi mwenye matatizo ya kiafya kuzimudu na kupata huduma, India inaongoza duniani kwa kutoa huduma bora za tiba.

"Nchi yetu pia ina madaktari bingwa wanaoaminika katika utoaji huduma, mwaka huu IMTD inawaleta watoa huduma kutoka hospitali kubwa za India ambazo ni Fortis na Medanta," alisema.

Alizitaja hospitali nyingine kuwa ni Asian Heart, Seven Hills, SRM Hospital, Vasan Eye Care na Idara ya Aayush ili kuja kuwasaidia wagonjwa waliopo nchini.

Alisema maonesho hayo pia yamelenga kutoa fursa ya wataalamu wa sekta hiyo kufahamiana wakiwemo wasomi na wadau ili kuweka jukwaa kwa mashirika na taasisi kati ya India na Tanzania waweze kushirikiana kuimarisha huduma ya afya.

Alisema watakuwepo wawakilishi kutoka hospitali na vituo vya afya vilivyopo nchini humo kikiwemo kitengo cha upasuaji, hospitali za macho, ortho care, bidhaa za afya, huduma za kiasili, utalii wa kiafya, kampuni za dawa na vituo vya physiotherapy.

"Zaidi ya nchi 30 duniani ikiwemo Marekani, Canada, Uingereza, Urusi, Uarabuni, Uganda, Tanzania, Sri Lanka na nchi za Bara la Asia, huwa wanakwenda India kupata matibabu," alisema.

Bw. Shaw aliongeza kuwa, nchi hiyo pia inaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya watalii wanaokwenda kufuata matibabu.
 
Sisi tukienda nchi nyingine ujue ama ni Maonesho ya Sarakasi au Ngoma za asili.. Thats all!..
 
Nilipoona heading, haraka nikafikiri wanakuja kuchukua nafasi za madaktari waliogoma.
 
wanamuonyesha nani maonyesho ya udaktari ili iweje au nao wamekuja kubeba twiga
 
muwaambie waje na CT SCAN zao, XRAY zao, sindano, gloves, vitanda vya hao wagonjwa, uniforms maana huku hatuna hivyo vifaa ndio maana kama walisikia juzi juzi tumefukuza madaktari wetu kwa sababu ya mgomo
 
Nani alikudanganya kuwa India ndiyo nchi yenye huduma bora za afya duniani? Inahuduma bora ukilinganisha na africa na wala si duniani, tena Tz ndiyo ya kuilinganisha siyo kama S.A.
 
Ni vyema wenye matatizo mbalimbali wajitokeze waweze kusaidiwa.
 
Nani alikudanganya kuwa India ndiyo nchi yenye huduma bora za afya duniani? Inahuduma bora ukilinganisha na africa na wala si duniani, tena Tz ndiyo ya kuilinganisha siyo kama S.A.

India ,Bazil, Thailand etc waliingia katika hii biashara ya medical tourism..ila hao jamaa wa mataifa makubwa walianzisha makusudi hiyo huduma kwa hizo nchi kwa kukwepa sheria za nchi zao.Hakuna tofauti na Guantanamo ilivyoanzishwa kukwepa sheria za US ambazo hazikuwa zikifanya kazi kwa watu ambao hawaogopi kifo wala kuthamini uhai kwa kiasi chochote cha kuridhisha.

Nchi hizo zina urahisi wa kupata watu wanaojitolea organs kwa bei chee sana, na pia majaribio makubwa na ya kinyama yakifanyika huko huwa sheria haipo sana .Na ukubwa wa population yenye masikini kiasi hicho kinawapa sample space kubwa.Na pia wanafunzi wa nchi kubwa huwa wanapata mahali pa kuwekezwa kam interns kirahisi kabla ya kwenda weka mikono juu ya mabilionea wa dunia.Sasa kuachia hiyo elimu kwa wazawa wa hizo nchi ni danganya toto ili wakija toa sababu waseme kuwa ni unafuu za bei.

katik hizo nchi zote Brazil na Agentina wamefanikiwa hamisha hiyo taaluma vizuri sana kiasi cha kufanya hata watu dunia ya kwanza kwenda bila shida na makampuni yao ya bima yapo tayari uza bima za afya kwa hizo nchi.Sijui kwanini JK kashindwa mtumia Maximo vizuri kuliko hata wabrazil walivyomtumia ku lobby kwa maslahi ya makampuniya kibrazil hapa nchini.Soon Brazil watamfanya Balozi hapa kwetu.naye aje kuwa Balozi wa kudumu kama si fisadi.
 
Nyie mfukuze mlio wasomesha kwa pesa za walala hoi,halafu kaombeni Wahindi waje kututibu. Hii ni deal ya nani? Mganga mkuu wa serikali, katbu mkuu afya, waziri wa afya au ikulu?? Watanzania bwana? Kila siku afadhali ya jana
 
"Gharama zao zitakuwa za chini na zitamwezesha kila mwananchi mwenye matatizo ya kiafya kuzimudu na kupata huduma, India inaongoza duniani kwa kutoa huduma bora za tiba."

Unataka kuniambia huduma ya hospitali na technologia inazidi ya USA!! labda unaota au haujui USA walivyo advance kwenye medical!! labda una maana huduma ya bei rahisi
 
Back
Top Bottom