Kitaja
JF-Expert Member
- Jun 14, 2011
- 2,836
- 1,382
Habari zenu wadau wa JF,
Hivi karibuni tulishuhudia udhalilishaji uliopitiliza wa dada mmoja aliyedaiwa kuwa ni msukule maeneo ya kibamba ambapo picha zika zilisambaa kwenye mitandao mbalimbali zikimonyesha akiwa mtupu. Kwa taarifa nilizosikia leo hii kupitia kituo cha radio cha Clouds, hayo madai ni uongo na huyo mtu sio msukule.
Ndugu wamehojiwa akiwemo mumewe na wote wameshangazwa na udhalilishaji huo na kusambaza habari kuwa ndugu yao ni msukule wakati si kweli. Huyo dada imethibitika kuwa ana matatizo ya akili na hiyo hali hata yeye mwenyewe aliijua na alikuwa akihudhuria matibabu muhimbili ambako alikuwa akipewa dawa kila mara na alikuwa akienda mwenyewe kuchukua.
Hadi hivi sasa familia yake inamtafuta huyo dada na tafadhali tuwasaidie familia hii kwa kutoa taarifa polisi mahali atakapoonekana.
Wito: Jamii iepuke kusambaza habari za kutunga kuhusu misukule kwani hili suala linakuzwa zaidi na watu ambao bila shaka hunufaika na imani hizo. Uchawi upo lakini suala la misukule linakuzwa zaidi na matapeli wanaotumia uganga wa kienyeji na wengine hutumia hata dini.
Pia jamii iwe makini kuchuja taarifa zinazoletwa kwenye mitandao mbalimbali kwani taarifa zingine zinakuwa na malengo hasi ya wanaozituma.
Wenu Kitaja wa JF.