Madai ya Hela za mafao wafanyakazi TRC

Sep 10, 2013
76
21
Habari!
Natumai mu wazima! Leo nataka kutumia jukwaa hili kuwakilisha kilio cha wastaafu wa shirika la reli Tanzania (TRC) ambao kwa zaidi ya mwaka sasa wamekuwa wakifatilia mafao yao kwenye mashirika ya hifadhi za jamii bila ya mafanikio, sababu kubwa ikiwa ni kuwa shirika halikuwa likipeleka fedha walizokuwa wanawakata wafanyakazi kwenye mifuko hiyo.

Inasikitisha kwa sababu fedha hizi walikuwa wakiwakata wafanyakazii.. hili ni shirika kubwa na lenye kurudisha kiasi kikubwa hazina kila mwezi, lakini cha kushangaza hawataki kulipa stahiki za hawa wazee waliolitumikia shirika hili kwa uadilifu na uaminifu mkubwa! Hii ni dhambi!

Najua kuna uwezekano mkubwa hoja hii ikamfikia Mh. Rais kupitia hapa... Baba, Mh Magufuli, hawa wazee wamekosa namna ya kukufikishia ujumbe, naomba unisamehe labda hii sio sehemu nzuri kuitumia kufikisha ujumbe, lakini nakuomba uwasaidie wazee hawa!
Ahsante!
 
Poleni Sana
Haki Huinua Taifa Bali Dhambi Ni Aibu Kwa Watu Wote
Haki Itachelewa Ila Mtaipewa!!

Tunakumbushana Watanzania Wote Popote Walipo
Iwe Una Chama Ama Huna Ujue Wazi Kuwa
Leo Hii 01,January 2021 Ndiyo Tumeianza Rasmi Miaka Mitano Ya
Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania
 
Ingekuwa ni kampuni ya mchaga sasa hivi hayo madai yangeisha kwa mkuu
 
Kiukweli hilo swala linaumiza sana kuna wazee TRC mpaka wanafariki bila kupewa stahiki zao.
 
Habari!
Natumai mu wazima! Leo nataka kutumia jukwaa hili kuwakilisha kilio cha wastaafu wa shirika la reli Tanzania (TRC) ambao kwa zaidi ya mwaka sasa wamekuwa wakifatilia mafao yao kwenye mashirika ya hifadhi za jamii bila ya mafanikio, sababu kubwa ikiwa ni kuwa shirika halikuwa likipeleka fedha walizokuwa wanawakata wafanyakazi kwenye mifuko hiyo.

Inasikitisha kwa sababu fedha hizi walikuwa wakiwakata wafanyakazii.. hili ni shirika kubwa na lenye kurudisha kiasi kikubwa hazina kila mwezi, lakini cha kushangaza hawataki kulipa stahiki za hawa wazee waliolitumikia shirika hili kwa uadilifu na uaminifu mkubwa! Hii ni dhambi!

Najua kuna uwezekano mkubwa hoja hii ikamfikia Mh. Rais kupitia hapa... Baba, Mh Magufuli, hawa wazee wamekosa namna ya kukufikishia ujumbe, naomba unisamehe labda hii sio sehemu nzuri kuitumia kufikisha ujumbe, lakini nakuomba uwasaidie wazee hawa!
Ahsante!
Mkuu hata watu wanahangaika kuchukua mafao yao NSSF, inafika mahali mtu anakosa mpaka nauli ya kufuatilia mafao yake maana kila siku wanwazungusha utadhani ile pesa wanawapa fadhila wakati ni pesa yao wamekatwa kwa miaka yote.
Kuna mambo yanasikitisha sana
 
Inakatisha tamaa kwa kweliii
 
Back
Top Bottom