Madai ya ‘gharama ya kesi’ ni yapi kisheria? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Madai ya ‘gharama ya kesi’ ni yapi kisheria?

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by sulphadoxine, Nov 11, 2011.

 1. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #1
  Nov 11, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  MARA nyingi katika mashauri ya madai, jaji au hakimu huamuru katika uamuzi au hukumu yake kwamba aliyeshindwa amlipe aliyeshinda gharama zote za kesi husika. Au wakati mwingine Mahakama huamua huwabebesha gharama wahusika wote kwa kutamka: “Kila mhusika abebe mwenyewe gharama ya kesi hii.”

  Inapotokea aliyeshinda kesi amepewa pia nafuu ya gharama kwa mana ya upande uliopoteza kutakiwa kumlipa, aliyeshinda hurudi mahakamani na kufungua madai ya hizo gharama, ambapo mara nyingi kama ni Mahakama Kuu ni mbele ya Msajili wa Mahakama na kama ni katika Mahakama ya Wilaya au ya Mkoa (Mahakama ya Hakimu Mkazi), ni mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo.

  Anayedai gharama ya kesi anadai kitu gani? Hii ndiyo mada yetu ya leo katika safu hii maridhawa ya “Ijue Sheria”. Hivi karibuni Mahakama Kuu ilitoa maelezo kuhusu suala hilo katika Shauri la Madai la Rufaa Namba 168 ya Mwaka 2007 kati ya Shabani Jafari na Hifadhi ya Wanyama Pori ya Mikumi. Shauri hilo la rufaa lilikuwa limesikilizwa na Mheshimiwa Jaji Augustine Shangwa.

  Kesi hiyo ilikuwa imeamuliwa awali katika Mahakama ya Wilaya ya Morogoro ambapo mrufani alikuwa ameshinda ikiwa ni pamoja na kulipwa gharama ya kesi. Hata hivyo, katika malipo ya gharama ya kesi alipinga kutolipwa kodi ya nyumba ambayo alikuwa amepanga wakati wote wa kusikilizwa kesi yake, chakula, usafiri na gharama zingine zilizojitokeza alipokuwa akisubiri kurudishwa kwao Kigoma baada ya kuachishwa kazi.

  Katika rufaa yake, mrufani Shabani Jafari, akiwakilishwa na Wakili Msomi Said El-Maamry ambaye alieleza jinsi alivyotumia gharama ya usafiri wa teksi na daladala kwenda na kurudi mahakamani ingawa mara chache alipewa tiketi kutokana na mazoea ya wahusika kutokutoa tiketi. Kuhusu suala la kutiliwa mashaka na Mkadiriaji wa Gharama ya Kesi, Hakimu Mfawidhi wa Mahakma ya Wilaya ya Morogoro kwamba baadhi ya tiketi zilikuwa za kughushi na hivyo kuzikataa, Wakili El-Maamry alipinga akitetea tiketi hizo kuwa za halali.

  Mahakama ya Wilaya ilikuwa na mashaka pia kwa risiti ambazo zilionesha kwa za teksi moja tu na ambazo namba zake hazikufuatana vizuri ikiwemo tarehe. Wakili El-Maamry alitetea kwamba ni kawaida mtu kuzoea kutumia teksi ya mtu mmoja tu kutokana na kuvutiwa na huduma yake. Wakili huyo alitetea pia kodi ya nyumba wakati kesi ikisikilizwa kwa miaka miwili. Hivyo Wakili Msomi El-Maamry alisema kodi hiyo ilikuwa ni sehemu ya gharama ya kesi. Gharama za wakili na za yeye mwenyewe mrufani kuhudhuria mahakamani, nazo zilidaiwa.

  Upande wa mjibu rufaa, Hifadhi ya Wanyama Pori ya Mikumi, iliyowakilishwa na Wakili Msomi R. K. Nsimba, ulisema kwamba Afisa Mkadiriaji Gharama wa Mahakama (Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya Morogoro) alikuwa sahihi katika uamuzi wake wa gharama ya kesi kwani kanuni inayotumika ni ile iliyoelezwa katika Shauri la Madai la Zuberi dhidi ya Msimamizi wa Uchaguzi (1973) E. A. 33. Uamuzi wa kesi hiyo ulisema kwamba madai ya gaharama ya kesi lazima yawe yana risiti au hati sahihi za malipo na kwamba gharama ya kesi huhusu “gharama ya wakati kesi ikiendelea mahakamani” tu na sio gharama zingine kama za chakula, malazi au biashara zingine.

  Jaji Shangwa alisema kwamba shauri hilo lilitokana na hukumu ya Jaji Laurean Kalegeya katika Shauri la Madai Namba 127 la Mwaka 2005 ambapo alitamka kwamba: “Mrufani alipwe pia gharama”. Kwa kuwa Jaji Kalegeya hakufafania gharama zipi, inawezekana mrufani alidhani ni gharama zote alizotumia kipindi cha kesi mahakamani hata pale alipokuwa haendi mahakamani.

  Mheshimiwa Jaji Shangwa katika hukumu yake ya tarehe 29 Juni 2011 alisema mtazamo huo wa mrufani ulikuwa sio sahihi kwani “gharama ya kesi” kisheria haina maana ya kila gharama aliyopata mrufani wakati wa kesi yake. Gharama ya kesi inahusu tu gharama ya kuhudhuria vikao vya mahakama wakati kesi ikitajwa, ikisikilizwa, ikitolewa uamuzi au hukumu, nauli ya kutoka nyumbani kwenda mahakamani, gharama ya wakili, uandaaji nyaraka za mahakama yaani uchapaji na utoaji nakala kwa nukushi.

  Mahakama Kuu ilisema kwa mfano ilikuwa sahihi Mkadiriaji wa Gharama (Hakimu wa Wilaya) kukubali gharama ya wakili, uhudhuriaji mahakamani (Mahakama ya Wilaya na Mahakama Kuu). Kuhusu gharama ya kutumia teksi bila risiti sahihi, Jaji Shangwa naye alikubaliana na Mkadiriaji Gharama kwa msingi ule wa kesi ya Zuberi ya Mwaka 1973 ya Mahakama ya Afrika Mashariki tuliyoitaja awali kwamba madai yoyote ya malipo au gharama lazima yaambatane na risiti au hati halali za malipo. Ni wajibu pia wa kila mpewa huduma yoyote hususan ya usafiri kupewa risiti au tiketi kwa tarehe husika ikionesha huduma iliyotolewa.
   
 2. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #2
  Nov 12, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Hizi ndiyo "court costs"? Kama ndiyo hizo basi ni njia tu mojawapo za mahakam kujipatia vipato. Mfumo wa mahakama ni biashara tu kama zilivyo biashara zingine.
   
 3. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #3
  Nov 12, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Halafu hii ya "wakili msomi" kutangulia jina la wakili ndiyo nini sasa? Kwani lazima neno "msomi" liwekwe nyuma ya jina la wakili? Bila kuwekwa hilo neno hatutajua kama huyo wakili ni msomi au?
   
 4. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #4
  Nov 14, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 180
  duniani kuna mambo mengi sana ya kujifunza. shukrani wakuu
   
 5. N

  Nyamanoro JF-Expert Member

  #5
  Nov 21, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 575
  Likes Received: 234
  Trophy Points: 60

  Kimahakama zinaitwa bill of cost
   
 6. K

  KIBONGOMKUTI JF-Expert Member

  #6
  Nov 21, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 1,415
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  Learned Advocate = Wakili Msomi
   
 7. C

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #7
  Nov 21, 2011
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,200
  Likes Received: 3,810
  Trophy Points: 280
  Angalia pia kesi ya Arobogast Fundi v Masudi Zaid (Lugakingira, J) High court of Tanzania at Mwanza Civil appela 189 of 1977. Itakupa principles governing assessment of bill of costs
   
 8. MKUNGA

  MKUNGA JF-Expert Member

  #8
  Nov 27, 2011
  Joined: Dec 10, 2009
  Messages: 443
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Wacha kupotosha watu wewe. Court costs ni zile fees unazolipa wakati wa kufungua shauri. Topic hii inaongelea 'costs' zilizotumika katika kuendesha shauri mf. gharama za wakili,stationary,usafiri, court fees, ambazo mtu aliyepewa hukumu with costs atafile BILL OF COSTS before a TAXING OFFICER (msajili, au hakimu mfawidhi). Kasome tena G.N 515 of 1991 The Advocates' Remuneration and Taxation of Costs Rules
   
Loading...