MADAI: Wanaume wa Tanzania Bara Hawana Mapenzi Kama Wanaume wa Zanzibar"Baby J"

MaxShimba

JF-Expert Member
Apr 11, 2008
35,772
4,054
MSANII wa ngoma ya ‘Bwashee’, Baby J, amedai kuwa wanaume wengi wa Tanzania Bara si wapendaji bali wengi ni wale wanaotaka kumchezea mwanamke na mwisho wa siku wanamtema tofauti na wanaume wa Visiwani ambao hupenda na huwa na mapenzi ya dhati kwa mwanamke.

Mtandao wa DarTalk ulifanya mazungumzo mafupi na msanii huyo juu ya muziki wake pamoja na maisha kwa ujumla ndipo alipoitoa ishu hiyo, kwa madai kuwa wenaume wengi Bara wanapenda kutoka na mwanamke mrembo mwenye kila aina ya mvuto na ndiyo maana wanakuwa na tabia ya kuacha acha hovyo.

Alidai kuwa Zanzibar wanawake wengi ni wale ambao wanaovaa baibui muda wote na hawana tabia ya kuonyesha miili yao na ndiyo maana unakuta hata wanaume hawana tamaa ya kutamani kila mwanamke wanayemuona mbele yao.

“Hakuna wahalibifu kama wanaume wa Dar yani ukicheka tu umekwisha, unajua hii ni tofauti sana na wanaume wa Visiwani na nahisi inatokana na wadada wenyewe kuvaa nguo za mitengo mno ambazo huacha sehemu kubwa za mwili zikiwa wazi hivyo humfanya mtoto wa kiume atumie kila njia kukupata,” alidai.
 
Sijui alisha kuwa na uhusiano na wabara wote!
Ana shindwa kujua binadamu hawa fanani?

Hata hivyo ni maoni yake ngoja ni yaheshimu!
 
Sijui alisha kuwa na uhusiano na wabara wote!
Ana shindwa kujua binadamu hawafanani?


Hata hivyo ni maoni yake ngoja ni yaheshimu!

Ina mana angepima uwezo wa kila mmoja?
Hapo kwenye Bold kwa kweli tafuta sababu nyingine Rutta ila sio hyo.
Na ndomana kuna ule msemo samaki mmoja akioza.....
 
Yeye mwenyewe ametulia mpaka mtu atulie nae?
Huo msemo wako hauna maana na uhalisia kabisa!

Kama yeye si wife material hata akienda bara, na akumbuke yeye ni msanii ni vigumu mtu kuamini kama ana weza kutulia ndani.

Maana tunaona mifano kwa wasanii wenzie!

Hawa wote ni pasua kichwa hivyo kumpata wa kumpenda kwa dhati lazima apige magoti na kuomba sana.

Ina mana angepima uwezo wa kila mmoja?
Hapo kwenye Bold kwa kweli tafuta sababu nyingine Rutta ila sio hyo.
Na ndomana kuna ule msemo samaki mmoja akioza.....
 
Na wale wanaume mixture , baba bara mama visiwani , na anaishi kwa interval huku kiasi na kule kiasi atakua kundi gani?
 
Mbona ye mwenyewe anajichanganya?

Labda ameongea kwa uzoefu wake binafsi! Amekutana na wabara wanaopiga na kuacha kutokana na tabia zake, namely anavyovaa nusu uchi na anavyobehave
 
Hebu tumwangalie Baby J kwa karibu

baby_j_stejini.jpg
 
hili swala la wanaume wa kitz-bara kutokujua kupenda limekuwa likizungumzwa na baadhi ya wanawake wa ktz.Je kuna ukweli katika hilo? Kama ni kweli nini chanzo? Nini kifanyike?kama si kweli nani anasambaza habari hii na kwanini?
 
hili swala la wanaume wa kitz-bara kutokujua kupenda limekuwa likizungumzwa na baadhi ya wanawake wa ktz.Je kuna ukweli katika hilo? Kama ni kweli nini chanzo? Nini kifanyike?kama si kweli nani anasambaza habari hii na kwanini?

Ni kweli kbs kuwa wanaume wa bara hawana mapenzi kbs.
Nadhani inatokana na uwingi wa wanawake tuliopo.
Ila Wanaume wenyewe wanabisha sijui kwa nini.
Na si kwa mastaa tu,hata madada wasio mastaa wanalalamika sana kuhusu upendo wa wanaume wa Kitanzania kuwa F+ kwa wanawake wao.
 
yeye kachezewa na nani kwani?

labda alichezewa na mimi mkuu, manake huwa sina tabia ya kuweka kambi. Nikila mzigo tu, nasepa kama mwewe hahaaaaaaaa!
Wanawake jihadharini na Mungi siyo mpenzi wa dhati kabisa!
 
Ina mana angepima uwezo wa kila mmoja?
Hapo kwenye Bold kwa kweli tafuta sababu nyingine Rutta ila sio hyo.
Na ndomana kuna ule msemo samaki mmoja akioza.....
Angalau Angeeleweka kama angekuwa na ushahidi wa kuwa na mwanaume anayependana nae atokae huko. pili athibitishe kuwa huko hakuna matatizo yatokanayo na mahusiano ya kimapenzi
 
ok shosti Madame B nimekupata, sasa kama ni kweli kwanini hawataki kulifanyia kazi hlo swala au ndo ile tabia ya watz kutokujali na kutake advantage?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom