Gwangzu
JF-Expert Member
- Dec 21, 2017
- 2,457
- 3,819
Wakati wanasayansi duniani wakihangaika kupata chanjo na tiba ya virusi vya corona, rais wa Madagascar Andry Rajoelina amezindua dawa ya mitishamba ''inayotibu'' Covid-19 .
Hata hivyo Shirika la Afya Duniani (WHO) linasema kuwa hakuna ushahidi wa tiba ya Covid-19 baada ya Bwana Rajoelina kutangaza dawa yake.
Taasisi ya taifa ya tiba nchini Madagascar (Anamem) pia imeonyesha wasiwasi wake juu ya ufanisi wa dawa hiyo inayoelezewa na Rais Andry Rajoelina kama yenye uwezo wa kuzuwia na kupona corona.
Taasisi hiyo imesema kuwa mitishamba inaweza kudhuru afya ya mtu kwani "hakuna ushahidi wa ufanisi wake kisayansi".
Mmea huo unatarajiwa kutolewa bure kwa watu wenye uwezekano mkubwa wa kuathiriwa na na virusi vya corona.
Ikizinduliwa kwa jina Covid-Organics, dawa hiyo imetengenezwa kutoka kwa mmea artemisia (pakanga)-ambao ni mojawapo ya miti ambayo huchanganywa pamoja na mimea mingine ya Madagascar kama tiba ya ugonjwa wa Malaria.
Dawa hiyo ambayo imepakiwa kwenye chupa na kutangazwa kama chai ya miti shamba baada ya kujaribiwa kwa watu chini ya 20 kwa kipindi cha wiki tatu, katibu wa rais Lova Hasinirina Ranoromaro ameiambia BBC.
"Vipimo vimefanyika-watu wawili wamekwishapona kutokana na tiba hii," Bwana Rajoelina alisema katika uzinduzi wa Covid-Organics uliofanyika katika taasisi ya utafiti ya Madagascar- Malagasy Institute of Applied Research (Imra), abayo ndiyo iliyotengeneza dawa hiyo ya mitishamba.
"Kinywaji cha dawa hii ya mitishamba huonesha matokeo katika kipindi siku saba," alisema rais huyo mwenye umri wa miaka 45, ambaye aliwataka watu kuitumia kama hatua ya kujikinga na ugonjwa wa corona.
"Watoto wa shule wanapaswa kupewa kinywaji ... kidogo kidogo kwa siku nzima," aliwaambia mabalozi na watu wengine waliokua wamekusanyika kwa ajili ya uzinduzi wa kinywaji hicho.
Dkt Charles Andrianjara, Mkurugenzi mkuu wa taasisi ya utafiti ya Imra, anaafiki kuwa Covid-Organics inapaswa kutumiwa kama kinga.
Lakini alijihadhari zaidi kuzungumzia zaidi juu ya matumizi ya dawa hiyo kama tiba, lakini akasema kwamba uchunguzi wa kimatibabu umeonyesha "dalili ya ufanisi wake kama tiba", shirika la habari la AFP lilimnukuu akisema.
Kisiwa hicho cha Bahari ya Hindi kimekwisharekodi hadi sasa wagonjwa 121 wa virusi vya corona, na hakuna vifo kutokana na ugonjwa huo.
Chanzo: BBC Swahili