Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,720
- 215,790
Habari za weekend wakuu,
Nimeona kheri niwaletembelee leo Ijumaa, maana J'mosi huku kwetu Kwamtogole maandazi na chapati vinauzika sana. Inawezekana nisipate nafasi ya kusabahi kesho na keshokutwa.
Shost huyu aliajiriwa na bank moja hapa mjini, lakini shost mambo yake tena, anataka kuonekana wa mjini kuliko hata sie tuliozaliwa Kwamtogole. Shost huyu kwa mshahara wa bank lakini lazima aende Dubai mara moja kwa mwaka, China na South Afrika. Shost kila handbag ina wallet yake, na vyote ni big names.
Shost huyu sijui ana asili ya Congo? Kwa kuweka status sawa mjini, shost ana mabwana wanne, wote anawapanga yeye. Mmoja yuko South Afrika, huyo anatembelewa akijua yuko mwenyewe ndiye anaelipa kodi ya nyuba. Mmoja yuko China, ndiyo mwenyeji wake akiwa anakwenda kule na wawili wako mjini hapa.
Shost ni wale wa dada wanaojua make-up zote, perfume zote, lakini kiwanja cha kujenga nyumba ni msamiati. Sasa bwana imetokea shost amepitiwa na fagio la chuma kule kibaruani. Amepiga mabomu mabwana mpaka nao wameanza kuzima simu. Shost kuona anaadhirika mjini, si ameanza kuwatembelea mashost zake wale level, akifika kule anaomba kwenda kujisaidia ndiyo anapita chumbani na kukomba make-up.
Hivi madada kukubali kuwa hali imebadilika ni dhambi? Alafu na nyinyi wanaume, mkiona mizinga inazidi ndiyo nini kuacha kupokea simu? Mjini jamani ni shule.