MADA: Tatizo la Watoto kuchelewa kuongea. Ni kipi chanzo chake? Je, nawezaje kutatua tatizo hili?

Mwanangu wa sita kuzaliwa alikua anasubiri nikirejea anaanza kutoa mashtaka...
Aaa baba.....
Kisha naitika, then anasema
Aaa mama akuma chini...🤣🤣
Kisha namuuliza, ikawaje
Then anajibu, akuma aaamimi achafuka sana....😂😂
Then baada ya hapo, namuuliza tena unasemaje??😆😆
Wakati huo alikua anaumri wa mwaka mbili na nusu....😅😅
😂😂😂Huyu alikupenda ulikuwa unamsikiliza na kumjibu! Wengine hawana time na watoto!!

Hongera sana
 
mwanangu alikuwa na miaka 2.5 akawa hajui kuongea yani Zaidi ya kuita mama ishu kubwa alikuwa anashinda na dada wa kazi tu ndani lakini baada ya kumpeleka baby care aisee ni chiriku japo anachoongea hakipo straight so umri bado sana kuongea ni moja ya matendo yanayohusisha long time learning na ubongo hasa so sio simple tu kuweza kuamza kuomgea mapema hasa kama hashindi na kucheza na watoto wenzie.
Unanishawishi nimpeleka day care labda atabadirika
 
Inategemea NZANZI na NZANZI Mkuu 😂
mkuu bak 😅 😅 😅 😅 😅 😅 nzanziii mwingine anadhani mtoto ataanza tu kuongeaa aaha baaa...wacha wutani huoo
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Sio dalili mbaya kama anaweza sema aaah eee.....ni improvements kubwa sana....sehemu yangu ya kazi watoto wengi hadi 4 years huwa wanakuja wanashindwa kuongea, wazazi huwa wanaleta majibu ya madaktari kisha sisi huwa tunawabadilishia lugha kutoka kiswahili kwenda kiingereza

Baada ya muda huwa wapo vizuri sana, pia mtoto akae mazingira yanayomruhusu kujifunza lugha kwa kusikia both sauti na milio, awe anasikia maneno mengi na sauti nyingi kwa siku zile ndizo zinamsaada katika kujifunza lugha....i mean mchanganye na mazingira ya waongeaji na watoto wenzie wanaocheza na kutamka maneno mengi ile inastimulate ubongo wake na mdomo kukaza mwisho ataweza kuanza kutamka.....

NB: nimetumia taaluma ya elimu ya cambridge na maelekezo yake kwaujumla, mimi sio daktari ni mwalimu.
 
Mama yake anamsomeaga moja, mbili... Hadi 10
Kuna wakati tunamsikia anayarudia kwa tabu ila ni mara chache sana ukitaka arudie harudii hadi wakati mwingine tunakua wala hatutarajii
Vuta msuli hakikisha kila siku unatumia nusu saa asubuhi na nusu saa jioni ni wewe na yeye tu. imba nae nyimbo za chekechea, tafuta vitabu vya watoto mzoeshe simple words. Chair, spoon, tea, cup.

Inawezekana Kiswahili ubongo kimekua mgumu kwake jaribu maneno ya Kiingereza. Kiswahili atajua baadae.
 
Mwanangu wa sita kuzaliwa alikua anasubiri nikirejea anaanza kutoa mashtaka...
Aaa baba.....
Kisha naitika, then anasema
Aaa mama akuma chini...
Kisha namuuliza, ikawaje
Then anajibu, akuma aaamimi achafuka sana....
Then baada ya hapo, namuuliza tena unasemaje??
Wakati huo alikua anaumri wa mwaka mbili na nusu....
Hahahahahahaha hadi raha
 
mkuu mm wangu ana miaka mi 4na miez miwili n wa kike.. lakin anaongea mambo ambayo ata hayaelewek. kuunganisha maneno hawez kabixa. lakin baba mama dada kaka bibi anajua kila kitu
Mungu amsaidie aweze kuongea kabisa, hapo ni kumuweka mazingira ya watoto wenzie wanaojua kuongea ajifunze maneno mengine, watoto huwa walimu bora wa watoto wengine kuliko sisi wakubwa ambao mtoto anaweza asijifunze kutokana na sababu nyingi ikiwemo uoga.
 
Sina uzoefu sana na hili ila jaribu kumpeleka shule za vidudu akachanganyike na wenzie, wataalam wanadai inasaidia

Nilimpeleka shule mwalimu akamtandika sababu mtoto haongei ila mtundu!! Inakuwa kama anafanya kile anataka yeye, baada ya kutandikwa na mwalimu aligoma shule!! Hakwenda tena mpaka umri ulipofika wa kuanza shule, tukamuanzisha upya!!

Walimu wa kibongo ni tatizo sana, wanapiga watoto!!!
 
Unahisi atakua bubu?
Muangalieni kama ulimi unanyanyuka hauna kinyama kwa chini,
Lakini nikutoe hofu tu miaka miwili bado mdogo sana kuweza kupata wasi wasi kua haongei, watoto wa ndugu zangu waliongea na miaka minne, wao walikua wanaongea lugha wanazozijua wao tunasema makorokocho,

Daycare inasaidia pia, mpeleke lakini usiwe na haraka nae ataongea tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Akisomewa 1,2....5.. 10 na mama yake inaweza pita muda utakuta anayarudia peke yake kwa tabu
 
Mama yake anamsomeaga moja, mbili... Hadi 10
Kuna wakati tunamsikia anayarudia kwa tabu ila ni mara chache sana ukitaka arudie harudii hadi wakati mwingine tunakua wala hatutarajii

Huku mbali sana, anatakiwa asemeshwe!! Unampa chakula unamwambia 'njoo ule', 'unakula' unamuona anajisaidia unamwambia 'mtoto anapuu'.

Hizo moja tatu hazimjengi kwa sasa
 
Achana na maneno ya majirani kwenye malezi, watakupoteza! Lea mtoto vile waona sahihi kwako.

Nyanyua ulimi kama hana uzi au peleka kwa daktari wa watoto amkague! Kama hana shida ataongea tu! Mie nilikuwa na wazee (bibi na babu zake) walimkagua wakasema yupo poa. Siyo madaktari ila uzoefu wa wazee, wengi tunawazarau ila wanajua mengi sana.

Kama hana shida, nunulia mtoto michezo mbalimbali kuvuta watoto rika lake kuja kucheza nae, watoto wakija andaa kama kisherehe wanaimba, kuongea na kucheza!! Unawapa popcorn na biscuits tu + juice labda na vipipi!!

Muda mfupi tu! Ataongea! Sometimes hana watoto wenzie wanaomchangamsha. Unakuta anashinda na watu wazima ambao mtoto akiongea hawana time nae ya kumsikiliza, kumjibu au kumuongelesha!! Anaacha kuwa na hiyo bidii. Mwisho wa siku anachelewa kuongea
Hapa home naishi na mke wangu na hatoki nae nje mara nyingi wanashinda ndani kuna mtoto wa jirani ucheza pamoja nae anajifunza kuongea ila Nazani nimpeleke daycare
 
Anajikojolea tu hasemi chochote, maji anaenda kuchukua kikombe anakuletea, ukimwambia njoo anakuja
Hakuna tatizo hapa, inaonekana huyo mtoto mda mwingi anakaa peke yake au anaishi na watu wazima, tafuta watoto wanao endana nae kiumri au walio mzidi kidogo mchanganye nae au tafuta watoto viongeaji sana mchanganye nao, fasta tu mzee...

Kuna mtoto wa ndugu yangu wa kike yaani miaka mitatu hajui kuongea, bahati nzuri kwa jirani kukawa na katoto kamehamia dah haikuchukua mwezi
 
Naskia eti watoto wakila nyama za utumbo wanachelewa kuongea.

Ila huyo ataongea bado ni mdogo. Mtoto wa mdogo wangu aliongea akiwa na 3yrs. Alivyoanza kuongea tulifurahi sana simu zilipigwa kila kona tukipewa hiyo habari.

Na alivyoongea neno moja alianza kunganisha maneno ndani ya mwezi tulishangaa.

Kwa sasa anaongea hadi kero tunajiuliza analipizia ule muda aloupoteza bila kuongea. Maswali, nyimbo, kelele ni yeye.

N.b muangalie chini ya ulim kama kuna dadude wakakate hospital. Kama hakapo kuwa na subira ataongea.
Mkuu unanitamanisha ni raha sana mtoto akianza kuongea
Nitajaribu kumchunguza ulimi wake ila kuhusu nyama ya utumbo sina ujuzi labda wadau waongezee
 
Pia katika kutumia english hebu maneno magumu asiyajue kukojoa ajue Susu na kujisaidia haja kubwa aseme pupu. mimi susu (anataka kukojoa)
 
Hapa home naishi na mke wangu na hatoki nae nje mara nyingi wanashinda ndani kuna mtoto wa jirani ucheza pamoja nae anajifunza kuongea ila Nazani nimpeleke daycare
Labda upate day care nzuri!! Si recomend! Hizi changamoto zako nilipitia, day care aliishia kutandikwa na waalimu na nililipa hela mingi!

Then kumbuka mtoto haongei, so waalimu wanam-treat wanavyojisikia!! Mtoto alipokataa shule nikafanya uchunguzi ndiyo nagundua tatizo, namfikishia malalamiko mwenye shule akafukuza bure wadada wa watu, nikabaki naumia roho tena!!

Fanya niliyokuelekeza, ndicho nilishuriwa na mtaalam wa saikolojia nikafanya hivyo na improvements zikaja fasta sana!!
 
Back
Top Bottom