MADA: Tatizo la Watoto kuchelewa kuongea. Ni kipi chanzo chake? Je, nawezaje kutatua tatizo hili?

Mama akuma chini 🤣🤣🤣🤣🤣🤣
Mwanangu wa sita kuzaliwa alikua anasubiri nikirejea anaanza kutoa mashtaka...
Aaa baba.....
Kisha naitika, then anasema
Aaa mama akuma chini...🤣🤣
Kisha namuuliza, ikawaje
Then anajibu, akuma aaamimi achafuka sana....😂😂
Then baada ya hapo, namuuliza tena unasemaje??😆😆
Wakati huo alikua anaumri wa mwaka mbili na nusu....😅😅
 
mwanangu alikuwa na miaka 2.5 akawa hajui kuongea yani Zaidi ya kuita mama ishu kubwa alikuwa anashinda na dada wa kazi tu ndani lakini baada ya kumpeleka baby care aisee ni chiriku japo anachoongea hakipo straight so umri bado sana kuongea ni moja ya matendo yanayohusisha long time learning na ubongo hasa so sio simple tu kuweza kuamza kuomgea mapema hasa kama hashindi na kucheza na watoto wenzie.
 
Unahisi atakua bubu?
Muangalieni kama ulimi unanyanyuka hauna kinyama kwa chini,
Lakini nikutoe hofu tu miaka miwili bado mdogo sana kuweza kupata wasi wasi kua haongei, watoto wa ndugu zangu waliongea na miaka minne, wao walikua wanaongea lugha wanazozijua wao tunasema makorokocho,

Daycare inasaidia pia, mpeleke lakini usiwe na haraka nae ataongea tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuwaongelesha watoto wachanga kila mara na wanavyoendelea kukua husaidia sana katika kuharakisha kuongea kwao kwa wengi wao. Usikute huyo dada wa kazi alikuwa hamuongeleshi kabisa.
mwanangu alikuwa na miaka 2.5 akawa hajui kuongea yani Zaidi ya kuita mama ishu kubwa alikuwa anashinda na dada wa kazi tu ndani lakini baada ya kumpeleka baby care aisee ni chiriku japo anachoongea hakipo straight so umri bado sana kuongea ni moja ya matendo yanayohusisha long time learning na ubongo hasa so sio simple tu kuweza kuamza kuomgea mapema hasa kama hashindi na kucheza na watoto wenzie.
 
Kuwaongelesha watoto wachanga kila mara na kardinaal wanavyoendelea kukua husaidia sana katika kuharakisha kuongea kwao kwa wengi wao. Usikute huyo dada wa kazi alikuwa hamuongeleshi kabisa.
hata wazazi wengi hwawaongeleshi watoto wao wanaongea maneno mara chache sana kuwakataza labda na kuwaambia waseme majina ya vitu.
 
Huyu Mwanangu Wa Kiume , Ana Umri Wa miaka miwili na Miezi Miwili, lakini Ajabu Hadi Sasa hajui kutamka Mama Wala baba Yeye Akishamka Ni kuguna Tu Na Kuimba hadi Siku Inaisha Ni Mhhh..... Aahhhh
.... Eeeeh.......!!!

Majirani Wanamsema Vibaya Kuwa Mtoto Mkubwa lakini Anazidiwa Hata Na Wadogo wenzie yaani Hajui kuongea chochote, hii Inanipa Stress Mimi Kama Mzazi Najisikia Vibaya Sana Na Sijui Nifanyeje Ili Mwanangu Aongee

Naombeni Mnisaidie Jinsi gani Nitamfanya mwanangu Ajue Kutamka Maneno kama baba n.k
Achana na maneno ya majirani kwenye malezi, watakupoteza! Lea mtoto vile waona sahihi kwako.

Nyanyua ulimi kama hana uzi au peleka kwa daktari wa watoto amkague! Kama hana shida ataongea tu! Mie nilikuwa na wazee (bibi na babu zake) walimkagua wakasema yupo poa. Siyo madaktari ila uzoefu wa wazee, wengi tunawazarau ila wanajua mengi sana.

Kama hana shida, nunulia mtoto michezo mbalimbali kuvuta watoto rika lake kuja kucheza nae, watoto wakija andaa kama kisherehe wanaimba, kuongea na kucheza!! Unawapa popcorn na biscuits tu + juice labda na vipipi!!

Muda mfupi tu! Ataongea! Sometimes hana watoto wenzie wanaomchangamsha. Unakuta anashinda na watu wazima ambao mtoto akiongea hawana time nae ya kumsikiliza, kumjibu au kumuongelesha!! Anaacha kuwa na hiyo bidii. Mwisho wa siku anachelewa kuongea
 
Yes say care inasaidia lakini ukipata muda ongea nae Kiingereza, daddy, mummy, soap evt. Aliweza kuunganisha manemo mawili kama daddy soap ni dalili ataweza sentence.
Mama yake anamsomeaga moja, mbili... Hadi 10
Kuna wakati tunamsikia anayarudia kwa tabu ila ni mara chache sana ukitaka arudie harudii hadi wakati mwingine tunakua wala hatutarajii
 
mkuu mm wangu ana miaka mi 4na miez miwili n wa kike.. lakin anaongea mambo ambayo ata hayaelewek. kuunganisha maneno hawez kabixa. lakin baba mama dada kaka bibi anajua kila kitu
Wewe mwenyewe hujui Sasa mtoto utamsaidiaje maana uandishi wako ni wa ajabu mwanao atajifunza kwa Nani?
 
Naskia eti watoto wakila nyama za utumbo wanachelewa kuongea.

Ila huyo ataongea bado ni mdogo. Mtoto wa mdogo wangu aliongea akiwa na 3yrs. Alivyoanza kuongea tulifurahi sana simu zilipigwa kila kona tukipewa hiyo habari.

Na alivyoongea neno moja alianza kunganisha maneno ndani ya mwezi tulishangaa.

Kwa sasa anaongea hadi kero tunajiuliza analipizia ule muda aloupoteza bila kuongea. Maswali, nyimbo, kelele ni yeye.

N.b muangalie chini ya ulim kama kuna dadude wakakate hospital. Kama hakapo kuwa na subira ataongea.
 
Back
Top Bottom