Mada Star TV: Mitandao ya kijamii ifungwe?

Mada Star TV: Mitandao ya kijamii ifungwe?

NADHANI KWAKUWA CLOUDS NYONGO IMEINGIA, WANATAKA KUMVUTIA MKUU KWAO.
 
Issue ya mitandao ya kijamii inataka kabisa kufanana na habari za bodaboda, Bodaboda zilipoanza kuchukua kasi kuingia Tanzania vijana wengi waliamua kuanza kuendesha hizo pikipiki bila ya hata kuwa na mafunzo ya usalama barabarani, bila ya hata leseni, yaani ilikuwa ni kama kujitoa mhanga. Nakumbuka hata shamba boy wangu alitoweka ghafla na kujongomea huko ingawa nilipokutana naye siku za mbele nilimwambia afanye mafunzo ya kuendesha pikipiki, na pia ya usalama barabarani na atafute leseni, alinisikia lakini hakutimiza ushauri wangu. Yeye kama walivyo wahanga wengine wa bodaboda alipoteza maisha badaye kwa ajali mbaya na trafiki report ilionyesha kuwa makosa yalikuwa ya bodaboda - Ilinihuzunisha sana

Sasa social media nazo kwa kiasi kikubwa zimeingiliwa na jamii ambayo haikutayarishwa na kupata maelekezo ya kufahamu kwa undani matumizi yake, umuhimu wake, taratibu na sheria za mtumiaji kama zilivyokuwa bodaboda na matokeo yake watu wengi sana wamekuwa na wanaendelea kuwa waathirika wa kisaikolojia na hata wengine wamepoteza maisha sababu ya tabia zetu za kiafrika za kugeuza lengo zuri la matumizi yake halali na kugeuza kuwa kama silaha ya kuwakosesha amani watu wengine kama vile kutukana, kueneza picha chafu, kudharau, kuchonganisha, kutoa habari za uwongo, kwa ujumla kuleta mazingira hatarishi kwa wana jamii wengine.

Mtu yeyote akiwa na simu yenye uwezo wa kuwa na facebook, whatsap, Instagram.... basi ameshajiona amehitimu anajisajili na kuanza matumizi ya hizo social media hata terms of application hazisomi, hata kama ni mgonjwa wa akili ama ana matatizo ya kisaikolojia ni kanyaga twende. Hili ni jambo la hatari sana kwa jamii ingawa wengi hawalioni

Kwa wenzetu Ulaya na America social media zinatumika kwaajili ya kuwarahisishia mawasiliano ya kukuza biashara, kama kuna janga ama hatari fulani, kielimu, kufuatilia usalama wa familia zao nk Lengo likiwa ni kumrahisishia mtu katika harakati zake za kimaisha na kumfanya awe na furaha kwa kiasi fulani maishani, kueneza upendo nk

Sasa sijui sisi waafrika tuna laana gani jamani.... Social media zimegeuzwa silaha za kuwaumiza wengine, kuwafanya wengine wasiwe na amani na maisha yao.. zimekuwa ndo dampo za mapicha machafu - Shame on us
 
Sahara media mmepoteza radhaaaa
Hamna utofaut na samak aliye china
 
Hii ndio mada inayojadiliwa star tv muda huu katika kipindi cha "tuongee asubuhi" na iko katika mtindo wa swali.e

Kipindi ndio kinaanza hivyo mwenye kupenda kufuatilia afuatilie.

Binafsi najiuliza ni nini kiko nyuma ya mada hii au nini kimewasukuma kuja na mada ya aina ya aina hii kwakweli sielewi.
Nilipita kwenye kipindi hicho asubuhi. Kulikuwa na mtangazaji aliyeshirikisha waalikwa wawili. Wote walikubaliana kuwa hakuna sababu ya kufunga mitandao ya kijamii. Issue kubwa waliozungumzia ni Makonda na Clouds TV. Mmoja wa waalikwa (Mr. Bituro kama sijakosea) aliegemea upande wa Makonda na yeye hakuona tatizo kwa yale yaliyotokea. Kikubwa alichosema kama watu wameudhika wasubiri hadi 2020 wafanye maamuzi, haoni sababu ya watu kupiga kelele na alifikiri Makonda alikwenda pale kama rafiki wa Clouds kufuatilia kitu ambacho walikubaliana na clouds wakazira. Akasisitiza hakuna aliye lengwa bunduki wala kupigwa.Wa pili alikuwa mwandishi wa habari ambae kwa kujiamini alisisitiza kuwa kitendo kile si halali na watu wanahaki ya kupiga kelele. Akasema hakuna anayelazimisha mkulu achukue hatua lakini kama kosa limetendeka ni sahihi mkuu kuchukua hatua na watu wanategemea hatua zichukuliwe na si sahihi biashara kuendelea kana kwamba hakuna lililo tokea.
Sasa cha ajabu hapa JF ndiyo watu wanasema STAR TV sio ya kuangalia. Mnasema mada ni ya kipuuzi lakini hapa (JF) 24/7 toka majuzi maudhui ya kipindi kile ndio yanayobishaniwa hapa. Waandishi wa habari pia hupenda vichwa vya habari chokonozi bahati mbaya wengi wetu wanafikiri ya kuwa nia ya Star TV ilikuwa kufunga mitandao ya kijamii kama yule alieomba malaika ashuke siku moja nakuifunga.Yule mwandishi alitoa madini safi sana. Vipindi vya maongezi hutegemea nani kaalikwa na mwenyekiti ni nani. Doto anafanya vizuri, cha leo pia kilikuwa kizuri.
 
Nahisi [HASHTAG]#mangekimambi[/HASHTAG] anawanyima usingizi ndo maana wanajidai wanajadili na baadae waifungie mitandao ya kijamii
 
Leo magazeti yote habari ya mjini makonda na jpm kasoro gazeti la serikali
 
Hivi ilikuaje had ukaweka star tv ? Me hata nkiwa nachagua chanel nairuka, sitakag hata kujua wanachoonesha, yan mm na makada wa lumumba hatuchangamanagi kabsa, hilo limada wajibu makada wenzao, kwanza ikifungwa mitandao wao ndo wataumia coz wanapenda kutafuta attention kwenye media
hata mimi sikumbuki mara ya mwisho kuiangalia,
 
Back
Top Bottom