Mada Moto: Tundu Lissu live Channel Ten

RingaRinga

JF-Expert Member
Jul 10, 2015
1,043
513
Mada inayoongelewa ni siasa, sheria na wajibu wa kila Mtanzania:-

Tufuatilie kisha tuchambue,

UPDATES:
Anasema mahakama ya mafisadi illianzishwa tangu 1985 na si jambo linalohitaji kuanzishwa sababu lipo.
 
Last edited:
Nasikia Lissu anajiuma uma tu kwenye hicho kipindi...Sifatilii kipindi...Naomba mtupe updates.
 
Tundu lisau anazidi kupoteza credibility, swali la lowassa na muhongo kalijibu kisiasa kabisa, kasahau kabisa kuwa pale mwembeyanga walikuwa wakimuita lowassa fisadi na ripoti ya mwakyembe ilikuwa imeshatoka! Leo anasema lowassa alibeba mzigo wa walio chini yake, ila hakuwa na hatia!
SITOMWAMINI KAMWE!
 
Bwege linamtetea Lowassa wakati lilimuita fisadi
kuna mtu kaniambia ametoa utetezi wa kijinga sana katika kumlinganisha Lowassa na Muhongo...Lissu hiyo ripoti ya Mwakwembe aliipata 2015!? Mbona bado waliendelea kumuita Lowassa fisadi pamoja na ripoti kuwa mitandaoni tangu 2008?
 
Tundu lisau anazidi kupoteza credibility, swali la lowassa na muhongo kalijibu kisiasa kabisa, kasahau kabisa kuwa pale mwembeyanga walikuwa wakimuita lowassa fisadi na ripoti ya mwakyembe ilikuwa imeshatoka! Leo anasema lowassa alibeba mzigo wa walio chini yake, ila hakuwa na hatia!
SITOMWAMINI KAMWE!
wewe kutokumwamini mtu haimaamishi haaminiki!
 
Kuna watu mnajidhalilisha. Upeo wa kujieleza wa Lissu ni mkubwa sana na ni wanasiasa wachache au wanasheria wanaomfikia. Issue ya ma DC wa mfano wa Makonda kaieleza vyema sana na kumbe hata Makonda afanyayo siyo mamlaka aliyopewa na katiba au sheria.
Leo kaonyesha wazi kuwa nini maana ya kumhoji hata rais bila woga wa kinafiki kwani kuwa citizen ni cheo kikubwa kuliko urais, ndio mwajiri kwa nini uogope kuhoji?
 
What I know ,maisha yataenda bila lissu,, kwa kifupi nmemtoa na kum'delete akilini kwangu.
Naomba msinishangae mm Nina allergy na mtu mnafiki. Mtu mnafiki hawezi kutufikisha popote na sio kipenzi cha mungu
 
Nimeshangaa sana kwa huo utetezi wa tundu lissu, kadai lowassa aliwajibika kutokana na ripoti ya Mwakyembe ambayo eti ilimtaka lowassa aachie ngazi kama kubeba msalaba wa waliokuwa chini yake ambao walikuwa watano ktk ripoti ya mwakyembe ila lowassa hakuwa na kosa, PUMBA KABISA KWA MTU ANAYEJIITA MSOMI NA MWANASHERIA MATATA, Tundu lissu anasaliti fani yake na credibility aliyoitengeneza kwa nguvu sana!
Huu utetezi sio wa msomi hata siku moja!
Huo utetezi angeutoa mzee wa elimu ya hapa na pale ningeelewa...Ila Lissu kajidhalilisha sana. Nafikiri ndio sababu hata ya Chadema kumtupa nje kwenye usimamizi wa kesi zake...Mfano ile ya kugombea maiti.
 
Kuna watu mnajidhalilisha. Upeo wa kujieleza wa Lissu ni mkubwa sana na ni wanasiasa wachache au wanasheria wanaomfikia. Issue ya ma DC wa mfano wa Makonda kaieleza vyema sana na kumbe hata Makonda afanyayo siyo mamlaka aliyopewa na katiba au sheria.
Leo kaonyesha wazi kuwa nini maana ya kumhoji hata rais bila woga wa kinafiki kwani kuwa citizen ni cheo kikubwa kuliko urais, ndio mwajiri kwa nini uogope kuhoji?
Kuwa jasiri kujaribu kutumia na akili yako kifikiri, sio lazima akisema hivyo ndo kweli!
Kakiri kuwa tunatumia mfumo wa DC toka uingereza na kaelezea majukumu ya DC kwa uingereza, ila kadai hiyo ilikuwa ni ya chama kimoja, kwa lugha nyingine afanyacho Makonda ni ndani ya mamlaka yake, ila yeye kadai kuwa U-DC wa namna hiyo ni wa mfumo wa chama kimoja, SASA NIKUULIZE, BAADA YA KUINGIA MFUMO WA VYAMA VINGI HAYO MAMLAKA YA DC YALIBADILISHWA KTK KATIBA ILI KUENDANA NA MFUMO WA VYAMA VINGI?
Jifikirishe ndugu, sio kuwa eti 'msomi' kasema basi ndivyo!
 
Lowasa aliwajibika ili kuilinda serikali..... Sawa alivyowajibika Muhongo & Maswi
 
Bora ata ya Muhongo hajaonekana Direct katika kashfa Tegeta Escrow lakini kwa Lowassa ni wazi kabisa ilijionuesha maana yeye ndie akitoa maamuzi, aliumda kama maalumu yeye ya kuchuja tenda, alitoa maagizo yeye katika nyanja mbalimbali mpaka mchakato wa kupata msambazaji kupatilana… Chanel iliyopo kati ya mmiliki wa Kampuni hewa ya Richmond na Lowassa mwenyewe nk
 
Leo unamuita mtu fisadi halafu kesho asubuhi unaenda ofisini kwake ukiwa na makabrasha yako, kwa ajili ya kupeleka taarifa kwa bosi wako (ambaye ulimuita fisadi jana!). Chochote atakachokwambia mwanasiasa kitilie shaka, hata jina lake pia.
 
wki ijayo mada moto atakuwepo kati ya said kubenea
jonh mnyika
jonh heche
ama mh mbilinyi
 
Kuna watu mnajidhalilisha. Upeo wa kujieleza wa Lissu ni mkubwa sana na ni wanasiasa wachache au wanasheria wanaomfikia. Issue ya ma DC wa mfano wa Makonda kaieleza vyema sana na kumbe hata Makonda afanyayo siyo mamlaka aliyopewa na katiba au sheria.
Leo kaonyesha wazi kuwa nini maana ya kumhoji hata rais bila woga wa kinafiki kwani kuwa citizen ni cheo kikubwa kuliko urais, ndio mwajiri kwa nini uogope kuhoji?
Uwezo wa Lissu katika kueleza na kutetea uongo ni mkubwa sana.
Na anapotosha sana sheria na tafasiri yake.
Kama umeamini hayo maneno ya Lissu kavu kavu kama yalivyo kwenye hiyo post nakuonea huruma.
 
Back
Top Bottom