Mada moto: Humphrey Polepole aongelea Miaka 50 na kilichofanyika

Mada moto: Humphrey Polepole aongelea Miaka 50 na kilichofanyika

“Ni jamii iliyochoka na kuchakaa; ni jamii iliyooza na kuchoma pua kwa harufu ya uvundo wa rushwa na kujaza nzi wakubwa wa rangi ya Kijani, Ni jamii yenye ufisadi na ukandamizaji; ni jamii isiyojua mbele wala nyuma, ni jamii iliyokosa dira”. Bunge lipo kwa jina tu kwa sababu limewekwa kwapani na watawala; Madaraka ya Rais ni makubwa kwa kiwango cha kupora demokrasia: Utajiri wa nchi upo mikononi mwa kikundi kidogo cha “wateule” na watawala kilichowageuza wananchi wadunda kazi wasiofaidi jasho lao. Na pale maandamano ya wanawake, wanaume na vijana wenye njaa yanapopita karibu na Makazi ya Wenye nacho,Malodilofa husimama ghorofani, wakawatazama na kuuliza, “kulikoni?”. Na walipoambiwa kwamba yalikuwa ya “malofa” wenye njaa waliokosa mkate wa kila siku, wao walijibu: “Kama ni hivyo, kwa nini wasile nyasi na mihogo?”Vijana wanaangamia kwa kukosa maarifa mashuleni na wanaishia kubwia "unga" ambao ni biashara pendwa ya Malodilofa,vijana wasanii wenye vipaji mbalimbali wanageuka ombaomba na wakati wa Kampeni wanakuwa "lulu" kwa kutumika kujaza “nyomi” katika mikutano,wakulima wanazeeka kwa kazi ngumu mashambani na kukosa pembejeo za kisasa na mazao yao yanaishia kukopwa kwa bei ndogo ajabu,wavuvi wanachomewa nyavu zao walizonunua kwa wafanyabiashara wajanja wenye meno,wawindaji wa vitoweo wanaambiwa ni majangili huku tembo wakiuwawa kwa tama ya meno yao na twiga wakipandishwa ndege kwenda ulaya na Asia..Dah! wagonjwa wanakufa huku wamelala mzungu wanne sakafuni mahospitalini kwa kukosa madawa,wakina mama wanajifungulia vichochoroni kwa ubovu wa barabara, Na wanapoona malofa wanawapigia kelele kwa madai yao sahihi wanaamuru majeshi ya ndugu zao wanyonge wawapige mabomu ya machozi na kuwaua na kuwasababishia vilema vya maisha na kuwatesa waandishi wa habari zao za kilofa.Watawala wetu hivi leo wanatuhumiwa kumiliki mabilioni ya fedha wanayomiliki huku wakiyaita ni “vijisenti”, au “fedha ya mboga”, wakati kipato cha Watanzania walio wengi ni chini ya shilingi mia nane kwa siku. Wananchi wanapopiga kelele kugugumia bei kubwa ya kivuko wanaambiwa “Wapige mbizi” na pale ndege ya Rais na rada chakavu inaponunuliwa kwa pesa nyingi zenye asilimia kumi za wajanja wanaambiwa “Ni heri wale nyasi”…Pamoja na mikakati mikubwa na yakutumia fedha na rasilimali nyingi za walala hoi kwa ajili ya kuvuruga "Mabadiliko" kwa kuwanunua wanasiasa uchwara na kuwakashfu kuwa ni “wapumbavu,amlofa na mbumbumbu”. Wakati umefika,chama kilichokuwa na dhamana ya haya yote kipumzishwe,ili kijitafakari,kitakapokuja kwa mara nyingine (MUNGU akikijaalia) kije kikiwa kamili....Kwa wakati huu,nathubutu kusema,Naichagua UKAWA,...sio kwa sababu za uimara wa CDM,CUF,NLD,NCCR MAGEUZI ama Uimara wa UKAWA la hasha!!Ila ni kwa sababu ya udhaifu wa CCM na ahadi ilizoshindwa kuzitekeleza kwa miaka 54 mfululizo.“ALUTA Continua, Victoria Ascerta”.... “The Struggle Continues, Victory is Certain”; ...Mapambano yanaendelea, Ushindi unakuja!! ≠HapaNimakwenziTu!!
 
Sasa hivi mambo ni huria na ushindani. Kama mnaona Polepole ni strategist wa CCM wekeni Dr. Lwaitama awe strategist wa UKAWA, halafu wasikie pumba au mchele kutoka kila upande. Pia Television Stations ni nyingi, kama CCM wako channel ten UKAWA nendeni ITV. Anayetaka kumsikiliza Dr. Lwaitama sawa, anayetaka kumsikiliza Polepole sawa pia. Lengo liwe kuwshawishi wapiga kura kwa hoja hai na siyo hoja mfu. Kawaida ya ILANI huwa inaeleza ukipewa madarak uaifanyia nini nchi yako. Chama kinaweka mkataba na wananchi juu ya mambo mazutri kitayowafanyia wananchi wake. Kuzungumza mabaya juu ya mpinzani wako siyo mambo ambayo wananchi wanayahitaji sana kwa maana hayo hayamo kwenye mkataba na hayawezi kudaiwa. CHADEMA haitahojiwa kama kilisema CCM haijaleta maendeleo kwa muda wa miaka 50
Eti huyo Pole pole ndiye strategist wa ccm kweli waafrica hususani watanzania tuna safari ndefu sana
 
Kumbe humphrey polepole anayeitwa kweny TV na kuanza kuijibia serikali iliyoko madarakani kuhusu kitu gani imefanya kwa miaka 50s kitu gani hakijakamilika, nani fisadi nani sio FIsadi, idadi ya mafisadi kama vile yeye ni Chanzo cha uhakika wakati si Kweli. Polepole hana sifa za kueleza hayo yote kwa nafasi yake kama Mwananchi wa kawaida. Ingetakiwa Aletwe mtu ambaye ni Mtaalamu wa fani hiyo kutoka ofisi ya Umma Mfano Takukuru, JAji wa mahakama, Waziri, ama Kiongozi yoyote wa serikali atolee ufafanuzi hayo kuliko kumwacha Polepole akipotosha Umma.KWa taarifa zake za radio MBAO.
Mfano hoja ya yeye kusema Mgombea fulani sio MSafi wakati hakuna report yoyote toka kwa Mahakama wala uwepo wa case dhidi yoyote kuwahi kuripotia kumtia nguvuni mwanasiasa, ni kielelezo tosha kua anafanya kampeni za majitaka.
polepole amekua akikiri mwenyewe kua yeye ni mtu tu wa kawaida tena mdogo. na hii inatosha kum-disqualify kwenye vigezo vya kumtumia kuijibia serikali.
 
Kweli Mkuu huyu dogo zwazwa
 
"Ni jamii iliyochoka na kuchakaa; ni jamii iliyooza na kuchoma pua kwa harufu ya uvundo wa rushwa na kujaza nzi wakubwa wa rangi ya Kijani, Ni jamii yenye ufisadi na ukandamizaji; ni jamii isiyojua mbele wala nyuma, ni jamii iliyokosa dira". Bunge lipo kwa jina tu kwa sababu limewekwa kwapani na watawala; Madaraka ya Rais ni makubwa kwa kiwango cha kupora demokrasia: Utajiri wa nchi upo mikononi mwa kikundi kidogo cha "wateule" na watawala kilichowageuza wananchi wadunda kazi wasiofaidi jasho lao. Na pale maandamano ya wanawake, wanaume na vijana wenye njaa yanapopita karibu na Makazi ya Wenye nacho,Malodilofa husimama ghorofani, wakawatazama na kuuliza, "kulikoni?". Na walipoambiwa kwamba yalikuwa ya "malofa" wenye njaa waliokosa mkate wa kila siku, wao walijibu: "Kama ni hivyo, kwa nini wasile nyasi na mihogo?"Vijana wanaangamia kwa kukosa maarifa mashuleni na wanaishia kubwia "unga" ambao ni biashara pendwa ya Malodilofa,vijana wasanii wenye vipaji mbalimbali wanageuka ombaomba na wakati wa Kampeni wanakuwa "lulu" kwa kutumika kujaza "nyomi" katika mikutano,wakulima wanazeeka kwa kazi ngumu mashambani na kukosa pembejeo za kisasa na mazao yao yanaishia kukopwa kwa bei ndogo ajabu,wavuvi wanachomewa nyavu zao walizonunua kwa wafanyabiashara wajanja wenye meno,wawindaji wa vitoweo wanaambiwa ni majangili huku tembo wakiuwawa kwa tama ya meno yao na twiga wakipandishwa ndege kwenda ulaya na Asia..Dah! wagonjwa wanakufa huku wamelala mzungu wanne sakafuni mahospitalini kwa kukosa madawa,wakina mama wanajifungulia vichochoroni kwa ubovu wa barabara, Na wanapoona malofa wanawapigia kelele kwa madai yao sahihi wanaamuru majeshi ya ndugu zao wanyonge wawapige mabomu ya machozi na kuwaua na kuwasababishia vilema vya maisha na kuwatesa waandishi wa habari zao za kilofa.Watawala wetu hivi leo wanatuhumiwa kumiliki mabilioni ya fedha wanayomiliki huku wakiyaita ni "vijisenti", au "fedha ya mboga", wakati kipato cha Watanzania walio wengi ni chini ya shilingi mia nane kwa siku. Wananchi wanapopiga kelele kugugumia bei kubwa ya kivuko wanaambiwa "Wapige mbizi" na pale ndege ya Rais na rada chakavu inaponunuliwa kwa pesa nyingi zenye asilimia kumi za wajanja wanaambiwa "Ni heri wale nyasi"…Pamoja na mikakati mikubwa na yakutumia fedha na rasilimali nyingi za walala hoi kwa ajili ya kuvuruga "Mabadiliko" kwa kuwanunua wanasiasa uchwara na kuwakashfu kuwa ni "wapumbavu,amlofa na mbumbumbu". Wakati umefika,chama kilichokuwa na dhamana ya haya yote kipumzishwe,ili kijitafakari,kitakapokuja kwa mara nyingine (MUNGU akikijaalia) kije kikiwa kamili....Kwa wakati huu,nathubutu kusema,Naichagua UKAWA,...sio kwa sababu za uimara wa CDM,CUF,NLD,NCCR MAGEUZI ama Uimara wa UKAWA la hasha!!Ila ni kwa sababu ya udhaifu wa CCM na ahadi ilizoshindwa kuzitekeleza kwa miaka 54 mfululizo."ALUTA Continua, Victoria Ascerta".... "The Struggle Continues, Victory is Certain"; ...Mapambano yanaendelea, Ushindi unakuja!! ≠HapaNimakwenziTu!!
I wish polepole angesoma hapa na yeye.. manake sijui amekula maharage ya wapi yule...
 
Kumiliki simu, usafiri, hahaha nakuokota makopo ccm ndo maana wananchi wanatuona marofa kweli maana hatuoni mwaka huu ccm ikirudi madarakin hata mavi wananchi mtakula maana saivi chakula hamna
 
Hata uwezo wa kuchangia Jamii forum Ni Maendeleo. Miaka 10 iliyopita Hali ya umaskini ilikuwa kubwa kuliko sasa. Pato la Taifa limeongezeka kutoka milioni 19,112,830 mwaka 2005 hadi kufikia shilingi milioni 79,442,499 mwaka 2014 sawa na ongezeko la sh. 60,329,669.
Pato la wastani la Mtanzania limeongezeka kutoka shilingi 360,000 mwaka 2005 hadi shilingi 1,725,290 mwaka 2014 na ndiyo maana unaweza kununua bundle na kuingia Jamii forum na kupata taarifa usibeze maendeleo yapo.
Mapato ya ndani ya serikali yameongezeka kutoka sh. Bilioni 2,124.8 mwaka 2005 hadi sh. Bilioni 10,510.56 Juni 2014 kama Watu maskini kodi wanalipaje zinaongezekaje pato la Serikali.

jumla ya benki zilizosajiliwa na kusimamiwa na BOT na kuanza kutoa huduma zimefikia 57 zenye Matawi 660 Nchi nzima. Wateja wa benki hizo ni sisi pamoja na wewe unajua miaka 50 iliyopita Nchi ilikuwa na benki ngapi?

Takwimu zinaonyesha kuwa thamani ya mitaji ya uwekezaji kutoka NJE FDI imeongezeka kutoka dola za marekani milioni 1,229.4 mwaka 2011 hadi milioni 2,142 mwaka 2014 sawa na ongezeko la asilimia 74.2. Kote huko kunachangia kutoa ajira na kupunguza umaskini kwa watz.

uzalishaji wa CHAKULA umeongezeka kutoka tani9.66 milion mwaka 2005 hadi gani 16 milioni 2014 Sababu ya kuwepo mazingira mazuri kwa Wakulima kupata pembejeo kwa wakati pamoja na factors nyingine.

idadi ya watalii imeongezeka kutoka watalii kutoka NJE 612,754 mwaka 2005 hadi watalii 1,140,156 mwaka 2014.

mapato ya utalii yameongezeka kutoka dola milioni 823.03 mwaka 2005 hadi dola za marekani milioni 1,853 mwaka 2014.

mapato ya Taifa yanayotokana na MADINI yameongezeka kutoka dola milioni 727.45 mwaka 2005 hadi dola milioni 1,744.5 mwaka 2014.

jumla ya vijiji 4,718 katika mikoa 22 Tanzania Bara vimepelekewa umeme.
makao makuu za wilaya 125 kati ya 135 zimefikishiwa umeme.
ujenzi wa babra bara, nyumba bora, shule, hospitali etc si semi yote hayo Ni MAENDELEO.
Tusiwe walalamishi kwa kusukumwa na kauli za wanasiasa wasakatonge tunafuata mkumbo tu hakuna Maendeleo miaka 50 umezaliwa lini. Unajua kwenda Mtwara ilikuwa ina chukua Siku ngapi mwaka 70? Je unafananisha TZ na Nchi gani Uganda, Burundi, Kenya, DRC? Msiwe wepesi wa kudanganywa Someni data zote zippo mitandaoni na ktk vitabu ila tumezoea udaku wa JF mkidanganywa mnakubali na hao wasakatonge . Jiulize miaka 10 iliyopita kulikuwa na boda boda hiyo unayoipanda leo? Hayo Si mabadiliko?
 
.Huyu naye vipi.Wee unaongelea pato la taifa huku deni linapanda kila dakika.Pato la taifa kuongezeka wakati watoto wetu wanakalia vipande vya tofali madarasani.Pato la taifa kuongezeka huku hospitalini hakuna dawa na wagonjwa watatu wanatumia kitanda kimoja.Hizo hesabu za Ndulu mkulima anayekopwa mazao yake zinamsaidia nn.Unaandika msg ukiwa serena unakula juice.Msilete utani na maisha yetu.
Huyo Harakaharaka. katika kuharibu akili yenu leo Tcra wamemfuta huko alipokuwa anakashifu watu labda kama anamuujiza wa kukubaliwa na tume agombee udiwani kunduchi.Vinginevyo labda muwasiliane fb.
Tunazidi kusema Mabadiliko ni muhimu hayaepukiki. Kura zote kwa Lowasa.
 
Kati ya Lowassa na Magufuli nani wa kuleta mabadiliko? Wewe unadhani Lowasa ana mabadiliko ya kumnufaisha MTZ au kulipa madeni ya wahindi walomzunguka kipindi cha uchaguzi? Acha mzaha Maendeleo ndani ya miaka 50 ya uhuru Ni mengi pamoja na changamoto zilizopo. Muulize Mzazi wako ilikuwa ina chukua Siku ngapi kufika Kwao kwenye asili yao na sasa Hali ikoje? Wewe una simu ya mkono muulize mzazi wako alikozaliwa alikuwa na simu hata ya mezani? Hao unaowaita maskini wana simu za mkono sasa. Acha jazba huyo Lowassa mlombatiza jina la Fisadi ambalo sasa mnaona Haya kulitamka mpaka mnafuta list of shame ktk website yenu akileta mabadiliko yatakuwa ya staili mpya ya ufisadi wa Nchi labda
 
Polepole mji.nga,kilichofanyika ni kidogo ukilinganusha na mali zilizotumika na muda wenywe.

Pia kilichofanyika kingeweza kufanywa na bandari tu bila kusasambua mali zetu nyingi.
 
​

Leo channel Ten kipindi kinahusu kilichofanyika baada ya miaka 50 na mgeni mualikwa ni Humphey Polepole

Polepole: Ni miaka 51, inasemekana hakuna kilichofanyika na kusema hawa sasa wameshindwa katika miaka 50. Kukubali mafanikio ambayo umeyafikia ni ustaarabu pia changamoto.

Sifa moja ya binadamu ni kujikubali, Tangu tunaanza sidhani kama mwaka 2000 watu wengi tulikuwa tunamiliki kama sasa, leo hadi bibi yangu Nundu anamiliki simu. Kutoka Tabora hadi Iringa ilikua lazima ufike Dodoma kwa Treni ndio uanze kuunganishe mabasi kwa muda mrefu.

Nakumbuka mama akiandaa maandazi ya kula njian kwa sababu tulikuwa tunalala safari ya Tabora, leo tunasema miaka 50 hakuna kilichofanyika! Tujitendee haki kama taifa.

Ukiangalia hali ilivyokuwa zamani na ilivyo leo kuna tofauti kubwa, Mwalimu Nyerere ameliongoza taifa hili nusu ya miaka baada ya kupata uhuru ambapo maneno yake yanatumika kwenye kampeni za UKAWA na CCM.

Toka mwaka 64 inazaliwa Tanzania na tukawa na katiba ya mpito mpaka 67 linazaliwa Azimio la Arusha mpaka 77 na tunaingia vita vya Uganda baada ya hapo. Vita ambayo iliturudisha nyuma kabisa. Vita za ukombozi pia zilitugharimu kwa sababu ilibidi tuvunje uhusiano na Uingereza. Tukajenga reli ya Tazara ikiwa ndio reli ya kwanza ya standard Gauge.

Mzee Mwinyi anaingia kuja kureebisha uchumi, uchumi wa soko huria kila mtu ashiriki kwenye uzalishaji, Mkapa akajenga uchumi imara na kazi ya Jakaya ikaja kuimarisha na kutengeneza sheria kuhakikisha uchumi wtu unaratibiwa na sheria.

Maendeleo ni hatua, tulikuwa na mainjia wawili na leo ni zaidi ya 10,000. Tunazungumza kilometa 1300 za lami leo tunazungumzia 20,000. Viwanda vitakuja kujibu tatizo la ajira, ndio viwanda anazungumza Magufuli, kama ulichukua kiwanda na ukashindwa utarudisha kiweze kuendelezwa.

Maswali na maoni

  1. Kaka amenikata kauli, katika miaka 50 najua kuna mazuri yamefanyika lakin pia kuna mabaya. Kwa asilimia kubwa hakuna kilichofanyika lakini sio hakuna kilichofanyika. Viwanda vilikuwepo, kwa nini vinakufa, matatizo ni mengi kuliko mafanikio.
  2. Asante kwa kipindi na mada hii nzito, nina respect kubwa kwa Polepole lakini sasa anaenda kushoto, nashangaa anasema tusijilinganishe. Huwezi kusema sekondari tumejenga aafu ndio tutrain walimu, huwezi kujenga hospitali wakati huna wauguzi. Tulikuwa na viwanda vimekufa, barabara zilikuwepo, kilichofanyika ni kuweka lami.
  3. Nikushukuru, Polepole kidogo anatuchanganya, angekuja kwetu sisi wananchi kwenye uhalisia uone watu wanavyopata shida. Tulinganisha maendeleo kulingana na rasilimali tulizonazo na miaka tuliyonayo.
  4. Niungane na Polepole, mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni, wanasiasa wajaribu kuwa wakweli. Kigoma leo kijijini sana naangalia channel ten na sio kwa kutumia solar bali umeme kwa huduma ya REA. Watanzania tujaribu kuwa wakweli.
  5. Ukweli ni kwamba tunarudi nyuma kama viwanda vinakufa, ukifika hapa Tanga viwanda vyote utafikiri magofu.
  6. Shida ya Polepole anaegemea upande mmoja, Nyerere viwanda aliacha vinafanya kazi, alivyokuja Mkapa alileta ubinafsishaji, Je! Ulisaidia! Miaka 50 Dar es Salaam hamna maji!
  7. Watanzania tunapaswa kuacha ushabiki wa vyama na kuangalia zaidi mtu anaegombea ni wa namna gani. Kusema miaka 50 hamna kilichofanyika wakati matibabu yameongozeka, mashule yameongezeka, miondombinu imeongezeka. Watu waangalia mtu gani anastahili kuongoza taifa letu, UKAWA hata wakipata madaraka kuna mambo hawataweza kufanya kwa asilimia 100.

Polepole: Kuna hii dhana ya mabadiliko, CCM imeweza kuiishi kwa rushwa kutokuwa kigezo cha kupata madaraka, matajiri pia wameshindwa kuhodhi utawala. Amekuja kuibuka mtu kwa vigezo, mabadiliko ya mwalimu Nyerere aliyoysema mwaka 1995 yamedhihirika miaka 20 baadae.

Viwanda vyetu vilikufa si kwa sababu ya uzembe wetu na ubadhilifu pekee bali madiliko kwenye dunia dhidi yetu, kila kitu ni hatua na wananchi ni vizuri kuzifahamu. Ni bora kuwauliza kwani wewe ulivyokuwa madarakani ulifanya nini?

Polepole: Video ya Lowassa, kama mimi nahusika na video! Juma Mwapachu amesema Lowassa ameteleza, mimi nasema ameanguka chini.

Hapana mimi nilitaka kuwaambia watanzania kuwa mimi ni Mlutheri lakini haiwezekani kumchagua mtu kutokana na dini yake, vipi Waislamu na madhehebu yao. Mimi sihusiki na hio video na hatufanyi siasa makanisani.

ACHA UNAFIKI LAKINI PIA HATUTAMKATAA MTU KWASABABU YA DINI YAKE HATA KAMA NI MLUTHERI TUTAMCHAgua ilimradi atatufaa kama kiongozi wa hatma ya taifa hili
 
Last edited by a moderator:
Kwani si nimeskia tcra imepiga marufuku kualikwa kwny TV radio kuongelea siasa Km ww si mgombea
 
Kati ya Lowassa na Magufuli nani wa kuleta mabadiliko? Wewe unadhani Lowasa ana mabadiliko ya kumnufaisha MTZ au kulipa madeni ya wahindi walomzunguka kipindi cha uchaguzi? Acha mzaha Maendeleo ndani ya miaka 50 ya uhuru Ni mengi pamoja na changamoto zilizopo. Muulize Mzazi wako ilikuwa ina chukua Siku ngapi kufika Kwao kwenye asili yao na sasa Hali ikoje? Wewe una simu ya mkono muulize mzazi wako alikozaliwa alikuwa na simu hata ya mezani? Hao unaowaita maskini wana simu za mkono sasa. Acha jazba huyo Lowassa mlombatiza jina la Fisadi ambalo sasa mnaona Haya kulitamka mpaka mnafuta list of shame ktk website yenu akileta mabadiliko yatakuwa ya staili mpya ya ufisadi wa Nchi labda

alafu nyinyi mnajigamba na mabarabara wakati hata fedha za hizo barabara asilimia 80 ni misaada ya nje.sasahivi tunakaribia kutokukopeheka na nch ina raslimali kibao sijui kwanini tunadaiwa?ccm ni janga
 
Hata uwezo wa kuchangia Jamii forum Ni Maendeleo. Miaka 10 iliyopita Hali ya umaskini ilikuwa kubwa kuliko sasa. Pato la Taifa limeongezeka kutoka milioni 19,112,830 mwaka 2005 hadi kufikia shilingi milioni 79,442,499 mwaka 2014 sawa na ongezeko la sh. 60,329,669.
Pato la wastani la Mtanzania limeongezeka kutoka shilingi 360,000 mwaka 2005 hadi shilingi 1,725,290 mwaka 2014 na ndiyo maana unaweza kununua bundle na kuingia Jamii forum na kupata taarifa usibeze maendeleo yapo.
Mapato ya ndani ya serikali yameongezeka kutoka sh. Bilioni 2,124.8 mwaka 2005 hadi sh. Bilioni 10,510.56 Juni 2014 kama Watu maskini kodi wanalipaje zinaongezekaje pato la Serikali.

jumla ya benki zilizosajiliwa na kusimamiwa na BOT na kuanza kutoa huduma zimefikia 57 zenye Matawi 660 Nchi nzima. Wateja wa benki hizo ni sisi pamoja na wewe unajua miaka 50 iliyopita Nchi ilikuwa na benki ngapi?

Takwimu zinaonyesha kuwa thamani ya mitaji ya uwekezaji kutoka NJE FDI imeongezeka kutoka dola za marekani milioni 1,229.4 mwaka 2011 hadi milioni 2,142 mwaka 2014 sawa na ongezeko la asilimia 74.2. Kote huko kunachangia kutoa ajira na kupunguza umaskini kwa watz.

uzalishaji wa CHAKULA umeongezeka kutoka tani9.66 milion mwaka 2005 hadi gani 16 milioni 2014 Sababu ya kuwepo mazingira mazuri kwa Wakulima kupata pembejeo kwa wakati pamoja na factors nyingine.

idadi ya watalii imeongezeka kutoka watalii kutoka NJE 612,754 mwaka 2005 hadi watalii 1,140,156 mwaka 2014.

mapato ya utalii yameongezeka kutoka dola milioni 823.03 mwaka 2005 hadi dola za marekani milioni 1,853 mwaka 2014.

mapato ya Taifa yanayotokana na MADINI yameongezeka kutoka dola milioni 727.45 mwaka 2005 hadi dola milioni 1,744.5 mwaka 2014.

jumla ya vijiji 4,718 katika mikoa 22 Tanzania Bara vimepelekewa umeme.
makao makuu za wilaya 125 kati ya 135 zimefikishiwa umeme.
ujenzi wa babra bara, nyumba bora, shule, hospitali etc si semi yote hayo Ni MAENDELEO.
Tusiwe walalamishi kwa kusukumwa na kauli za wanasiasa wasakatonge tunafuata mkumbo tu hakuna Maendeleo miaka 50 umezaliwa lini. Unajua kwenda Mtwara ilikuwa ina chukua Siku ngapi mwaka 70? Je unafananisha TZ na Nchi gani Uganda, Burundi, Kenya, DRC? Msiwe wepesi wa kudanganywa Someni data zote zippo mitandaoni na ktk vitabu ila tumezoea udaku wa JF mkidanganywa mnakubali na hao wasakatonge . Jiulize miaka 10 iliyopita kulikuwa na boda boda hiyo unayoipanda leo? Hayo Si mabadiliko?

hizi bodaboda zimekuja baada ya mtoto wa mkubwa kukamatwa china na madawa ikabidi wachina wapewe uwekezaji nchn ili aachiwe.pili pamoja na hayo yote uliyoeleza hapo hayo ni ya kwenye makbrasha kiuhalisia hakuna kitu.huwezi kuniambia pato la mwananc limepanda wakati wapo watanzania wanakula mlo moja.huwezi kuniambia uchumi umekua wakati maden yanaongezeka.
 
Pole pole ni wa kumchunga sana, nilimuona kama mentor flani nikawa nafuatilia mada zake wakati wa kuchambua katiba pendekezwa, ila sasa kateleza vt anavyoongea havina uhalisia kbs sijui katishwa au kashanunuliwa simweli kbsaaaa
ANYWAY akili kichwani
 
Toeni data kuna Watu asilimia ngapi wanakula Mlo mmoja kwa Siku na miaka 50 Hali ilikuwaje? Tusidanganywe NA wasakatonge wanaomiliki hisa vodacom, mashule makubwa kama Alpha, mashamba makubwa makubwa Morogoro, kibaha na kwingineko , ranch za MIFUGO maelfu kwa maelfu. Vyote hivyo wamevipata ndani ya miaka 50 ya uhuru. Watoto wao hawapandi boda boda Wala dala dala leo wanajiita maskini pamoja na wewe unashabikia usichokijua. Semeni hoja za ukweli kuhusu hali ya Nchi sio kusukumwa kama misukule vile ya hao mnaowaita vinara wa Mageuzi kwa kusema uongo. Wazazi wao hawakuwa na Mali walizonazo wao sasa. Miaka 50 iliyopita kusingeweza kuwa na MTZ anamiliki nyumba London lakini leo Fred Lowasa ana nyumba London.
 
Back
Top Bottom