Mada moto: Humphrey Polepole aongelea Miaka 50 na kilichofanyika

Mada moto: Humphrey Polepole aongelea Miaka 50 na kilichofanyika

Mbona ujinga wako wewe umegoma kufutika? Hiyo USIJALI ni kwa faida yangu au ya Twiga? Utandawazi haujaharibu vijana bali umeiweka wazi CCM na ndio ugomvi unapoanzia.

Siku ujinga ukiisha, wananchi wa kijijini wakaelewa kwamba wanaposikia Bilioni 1 inamaanishwa milioni ziwe ELFU MOJA, hutapata muda wa kuandika utumbo mtandaoni.

twiga mwenyewe mmoja lakini unaongea utadhani twiga elfu kumi.
huyo twiga asingeenda arabuni angebadili nini?
 
masharti ya IMf Ndo yalipelekea ubinafsishaji,nchi duniani zilitakia kufuata sera ya uchumi huria na serikali kujitoa katika kufanya biashara.
ikabidi vibinafsishwe kwa wenye uwezo wa kuviendesha,mpaka sasa viwanda ni vingi tu,lakini havimilikiwi na serikali.

hata huko marekani kwa mfano serikali haimiliki viwanda ndo maana hata viwanda vikahamia china,,huwezi mpangia mtu binafsi akawekeze wapi
 
Siasa ya ujamaa na kujitegemea kama vile wenzetu wa china, tukijaribu kujilinganisha nao tuko sawa? Kama ndiyo basi miaka 50 niyafaida chanya!
 
Bw. Humphrey Polepole leo alikuwa kwenye ubora wake Channel 10.
Licha ya kufafanua kwa kina kuhusu dhana na nadharia ya 'maendeleo' na jinsi Tanzania ilivyopitia hatua na changamoto mbalimbali za maendeleo hadi kuifikisha nchi tulipo, alihitimisha kwa kusema kuwa Chama chake kimeishi falsafa ya Baba wa taifa mwaka huu kwa 1. Kuirejesha kwa wenyewe yaani wakulima na wafanyakazi ( na si kukiweka rehani kwa matajiri na mafisadi), 2. Kumpata mgombea Urais ambaye hakutumia nguvu ya fedha ama rushwa kununua kura za kumpeleka ikulu, 3. kusimamia kudumisha na kuimarisha muungano kwa hali na mali,4. na kulinda na kudumisha amani na utulivu nchini.

Big up! Endelea kutoa Mchango wako usiokengeushwa na ghirba na ulaghai wa wanasiasa uchwara na wachumia tumbo, pamoja na vijana waliokengeuka kwa kudhani kuwa maendeleo yao binafsi hayatokani na juhudi binafsi na uwezo wao wa kutumia fursa zilizopo, bali kwa kujazwa mapesa na wanasiasa!
 
Leo tena masikio yangu yameendelea kuamini kiwa hp ana aliki za kawaida mno.......ni aibu kwa taifa kuwa na aina hii ya vijana,........ kama yeye ni kichwa naomba ajibu hili swali;pesa zinazokopwa benk za nje kwa ajili ya miradi,pesa za nchi wahisani kila mwaka,mapato ya rasilimali zetu kama madini ,mbuga samaki nk,pamoja na kodi zetu vinaringana na maendeleo yaliyopo?..........
 
Eti huyo Pole pole ndiye strategist wa ccm kweli waafrica hususani watanzania tuna safari ndefu sana

mkuu siunajua unaposombwa na maji ya mafuriko hata nyasi ikikukaribia unaikamatia kudhani itakuokoa!
 
Wanajamvi ningependa kushiriki kwenye vipindi hivyo na huyo pole pole.Naomba ushauri na uwezeshaji angalau niweze kumjibu pole pole kupitia luninga
 
Leo tena masikio yangu yameendelea kuamini kiwa hp ana aliki za kawaida mno.......ni aibu kwa taifa kuwa na aina hii ya vijana,........ kama yeye ni kichwa naomba ajibu hili swali;pesa zinazokopwa benk za nje kwa ajili ya miradi,pesa za nchi wahisani kila mwaka,mapato ya rasilimali zetu kama madini ,mbuga samaki nk,pamoja na kodi zetu vinaringana na maendeleo yaliyopo?..........

Kijana gani,, huyo babu wa miaka 70 unamuita kijana?
 
Me nadhani polepole ameanza kuwa mwanasiasa zaidi. Huu ni uongo wa wazi yaani hata Leo anatudanganya na uongo aliopaswa kuusema mwaka 1995
 
Mahaba ya ukawa yanawanya mnajibu badala ya kutumia akili mnatumia makalio kujibu mkapa alikuwa sahihi
 
Mahaba ya ukawa yanawanya mnajibu badala ya kutumia akili mnatumia makalio kujibu mkapa alikuwa sahihi

Teh teh teh.Heri yako wewe uliyejaza haja kichwani badala ya akili.
 
Yeye anaongea alichomezeshwa na akina Warioba.
 
Kumiliki simu nayo ni maendeleo? Tena masimu ya kichina.
 
Muungano wa muundo gani ambao Chama cha Polepole kitaudumisha?Huyu jamaa si ndo muumini wa serikali tatu zilizopendekezwa na wananchi kwenye tume ya Warioba?Kijana gani anashindwa kusimamia anachokiamini anatumika tu kwa maslahi ya wachache?Kwa msimamo alokuwa nao kwa kuinadi katiba mpya alitakiwa achague chama kitakacho simamia katiba mpya inayotokana na rasimu ya Warioba.Kwa Kweli inasikitisha hii nchi haina watu wenye misimamo thabiti wasioyumbishwa .Mtu ili awe na uhuru thabiti inalazimika atoke CCM kama ni Mwana CCM. Polepole,Warioba mwenyewe na hata wengine wengi hawawezi kuwa huru ndani ya CCM.Bora Lowassa na Sumaye wamejitambua na kutoka CCM na sasa wako huru kusimamia wanayoyaamini .
 
Kusema hakuna maendeleo yoyote tangu Uhuru wakati hata tunafanya mjadala kwenye electronic media ni upofu wa kishabiki....., mengine yanayolalamukiwa na matokeo ya maendeleo... Km msongamano wa magari... Leo watu wengi zaidi wanataka na wana uwezo wa kuingiza gari barabarani ...etc

hivi sisi wa tanzania tumerogwa wewe ukitaka kujua kama umepiga hatua ni rahisi sana jilinganishe na mtu mliokuwa nae sawa kiuchumi wakati mnaanza yeye yuko wapi saivi na wewe uko wapi saivi ila kwa kukupa tu taharifa nikwabie kwamba wale tulikuwa nao uchumi sawa wametuzidi mara mia zaidi sisi tupo alaf ww unaona tubarabara twa lami twa mbavu za mbwa unasema maendeleo ebu tokeni usingizini hatukupaswa kuwa hapa
 
utakua ulizaliwa miaka ya 2000 asee,,umasikini uimepungua sana kwa taarifa yako kuliko miaka ya 60 au 70 ama hata 80,,,,
saa hizi watu wenye maisha ya kati ni wengi sana.

masikini wa kijijni leo anamiliki pikipiki,smartphone,etc..
Nimezaliwa miaka ya 70 na nimeishi vijijini ndani kabisa katika mikoa zaidi ya nane (Njombe,Arusha,Kagera,Morogoro,Iringa,Rukwa,Mbeya,Pwani na Tanga) mijini pamoja na nje ya nchi.Kati ya mataifa yaliyokuwa na rasilimali ambazo asilimia 90 ya watu wa Nchi hiyo hawanufaiki nazo ni Tanzania.Tuna kila ina ya madini.tuna gesi na makaa ya mawe,tuna mbuga na misitu.ardhi safi na vyanzo vya maji,bahari,milima na mabonde yenye rutuba.Wananchi wa Tanzania ni "maskini wa kutupwa" kuna watu kesho yao ni kitendawili kigumu na wengine wapo hata jiji maarufu la Dar es Salaam. Maisha yamekuwa maigizo. Takwimu zinaonesha ujinga umeongezeka kwa asilimia za kutisha,vijana wengi hawajui kusoma wala kuandika.Wanaendelea na masomo ya Vyuo Vikuu ni wale wenye uwezo wa fedha na mali.Wengi wameshindwa kuendelea kwa sababu hawana uwezo ni mikopo ina utata mwingi..Mpaka leo tunavyoandika magonjwa ambayo yametokomea duniani Tanzania ndio mahala pake.Jiji la Dar limekumbwa na ugonjwa wa aibu wa kipindupindu na wengi wameaga dunia kwa sababu ya uchafu.Mahospitalini wagonjwa wamelala mzungu wa nne kwa magonjwa mbalimbali na wakina mama wakijifungulia mitaroni ama vichochoroni!!!..Upande wa pili,watoto wa vigogo wanasoma nje ya nchi ama katika shule ambazo ada ya mwaka ni Milioni 80.Matibabu yao ya mafua na kikohozi ni ulaya na Marekani.Mavazi yao yamedizainiwa na Madizaina maarufu duniani.Mapumziko yao ni Vegas ama London.Benki zao ni Uswisi na Visiwa vya Uingereza. Vyakula vyao vinaagizwa kutoka Italy na Singapore,Usafiri wao ni ndege za kukodi na magari ya kifahari.Barabara za vumbi hawazijui asilani...Kuing’angania CCM ni miongoni wa matatizo yetu Watanzania.Wakati umefika ni LAZIMA IONDOKE ili kama itakuwa na Jipya IJITAFAKARI….
 
Back
Top Bottom